BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

CONGRATULATIONS NAKAAYA!! January, 29, 2009

Filed under: Burudani,Muziki,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 8:28 PM

nakaayabc112

Nilipomuuliza kwamba nini mipango yake ya baadaye kisanii au katika sanaa bila kusita Nakaaya alinijibu kama ifuatavyo; To be better and better and the best there ever was in Tanzania and in Africa. Hiyo ilikuwa takribani mwaka mmoja uliopita katika mahojiano yetu na Nakaaya ambayo unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

Leo hii,Nakaaya anakuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kupata mkataba na kampuni ya SONY MUSIC yenye makao yake makuu jijini New York nchini Marekani.

Kwa habari zaidi soma ujumbe huo mahsusi kutoka kampuni ya SONY MUSIC kama ulivyosambazwa leo kwenye vyombo vya habari.Hongera sana sana Nakaaya.Keep doing ya thing!

Nakaaya’s Photo/Stephen Freiheit

TANZANIAN SONGBIRD NAKAAYA SIGNED TO SONY MUSIC ENTERTAINMENT

An icon of contemporary Tanzanian music, Nakaaya, has been signed to Sony Music

Entertainment. Among the record label’s well-known subsidiaries are Columbia

Records, RCA Records and Epic records, just to mention a few. Nakaaya, who has

acquired a large following and growing fan base across the region, now makes

history by being the first East African artist ever to be signed to the second largest

record company in the world. The company’s roster includes internationallyacclaimed

artists such as Alicia Keys, Beyonce, Britney Spears, Celine Dion, Chris

Brown, Sean Kingston and many more.

The signing took place when Nakaaya was attending the “Music’s Relevance in Third

World Countries” Conference, in Copenhagen, Denmark, in late 2008. (more…)

 

HAINA NGWASU-INSPEKTA HARUNI

Filed under: Bongo Flava,Bongo Fleva,Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 7:43 PM

inspektabc1

Bila ubishi Inspekta Haruni ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava ambao wanastahili na wana haki kabisa ya kujiweka katika lile kundi la “wakongwe katika fani”.Pia Inspekta anadumu katika lile kundi la “wataalamu wa vina(mashairi) na tunzi ambazo baada ya kutoka hewani hugeuka zikawa misemo ya mitaani.

Kama hukubaliani name,basi jaribu kuusikiliza kwanza wimbo mpya kutoka kwa Inspekta unaokwenda kwa jina la Haina Ngwasu kwa kubonyeza player hapo chini.

Na kama jadi mpya ya wasanii wa bongo flava mashairi ya wimbo huu yanaelekea kuwa “ujumbe” kwenda kwa mtu fulani au watu fulani?Mawazo yangu.Sikiliza na wewe utuambie.Pata burudani.

Photo/Ahmad Michuzi


 

KAZI BADO INAENDELEA… January, 27, 2009

Filed under: Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 7:41 PM

amatus-bliyumba

Kazi bado inaendelea…Zaidi bonyeza hapa.

 

BARUA YA WAZI KUTOKA KWA RAIS OBAMA KWA MABINTI ZAKE January, 26, 2009

Filed under: Special Interest News — bongocelebrity @ 9:30 PM

barackbc

Sina uhakika kama ulipata nafasi ya kuisoma barua ya wazi kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama kwenda kwa wanae Malian a Sasha aliyowaandikia siku chache kabla ya kuapishwa kuliongoza taifa hilo lenye kila aina ya mikimikiki ikiwemo ya kivita na sasa ya kiuchumi.Kama hukuisoma basi pata nafasi ya kufanya hivyo sasa.Ina maneno ya busara ambayo kama wewe ni mzazi au unatarajia kuwa mzazi basi unaweza kuwamegea wanao.

Dear Malia and Sasha,

I know that you’ve both had a lot of fun these last two years on the campaign trail, going to picnics and parades and state fairs, eating all sorts of junk food your mother and I probably shouldn’t have let you have. But I also know that it hasn’t always been easy for you and Mom, and that as excited as you both are about that new puppy, it doesn’t make up for all the time we’ve been apart. I know how much I’ve missed these past two years, and today I want to tell you a little more about why I decided to take our family on this journey. (more…)

 

MH.SOFIA SIMBA;UNAMSHAURI NINI? January, 25, 2009

Filed under: Siasa,Tanzania/Zanzibar,Wanawake na Watoto — bongocelebrity @ 6:48 PM

simbabc

Pichani ni Mheshimiwa Sofia Simba,ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM nchini Tanzania.

Mheshimiwa Simba alichaguliwa katika uchaguzi ambao unasemekana ulikuwa wenye upinzani mkali katika historia ya jumuiya hiyo.Alishindana vikali na Mh.Janeti Kahama.

Kama zilivyo chaguzi nyingi kinachofuata baada ya vuta nikuvute huwa ni kazi.Je unadhani ni matatizo gani ya msingi yanayowakabili wanawake wa Tanzania?Ungependa kumpa ushauri gani Mh.Sofia Simba kuhusiana na Jumuiya anayoiongoza?


 

NJOO-PROF.JAY ft KLEPTOMANIACS January, 21, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Single/Mpya — bongocelebrity @ 8:05 PM

prof-jay-bc1

Wakubwa wanapopiga kelele kuhusiana na sera za Jumuiya ya Afrika Mashariki,vijana wao wanafanya kazi.Wanashirikiana bila kusita katika kazi zao,hususani za kisanii.Sio kwamba nafananisha siasa na sanaa..hapana…nasema tu!Pengine kuna lolote wakubwa wanaweza kujifunza kutoka kwa vijana?Sina uhakika.

Ushirikiano ninaouongelea hapa ni ule wa Prof.Jay(a.k.a Red Carpert) katika single mpya iitwayo Njoo.Katika wimbo huu ambao umo katika albamu yake ya Aluta Kontinua(kama hujanunua kopi yako halali,fanya hivyo)Prof.Jay amewashirikisha wasanii kutoka Nairobi, Kenya wanaokwenda kwa jina la Depicto/D.E.P(jina kamili Collins Majale) na Nyashinski(jina kamili Nyamari Ongegu) na Munkiri(jina kamili Robert Manyasa) kutoka kundi linalojiita Kleptomaniacs.Wimbo huu umerekodiwa jijini Nairobi chini ya Producer Msyoka.

Hebu sikiliza jinsi hali inavyokuwa Kiswahili cha Dar kinapokutana na kile cha Nairobi.Patamu.Pata burudani.

Picha kwa hisani ya DJ Choka.


 

MSIACHE KUONGEA-MwanaFA ft LADY JAY DEE

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Single/Mpya — bongocelebrity @ 8:00 PM

mwanafabc10Ukishakuwa na umaarufu fulani ni wazi kwamba unakuwa kipenzi cha vyombo vya habari.Yaweza kuwa kwa mazuri au kwa mabaya.Watu hupenda kusikia mtu maarufu fulani kafanya nini,anapanga kufanya nini nk.

Mbali na vyombo vya habari,mitaani pia(labda kupitia walichokisoma gazetini au kukisikia redioni) maneno huwa hayaishi.Huko nako ni mwendo mdundo.Aidha kupewa “ushauri wa bure” au maneno yaliyojaa chuki binafsi na yenye nia ya kumuangamiza mtu.Ndio maisha yalivyo.

jide-komandobcLakini maneno yakizidi huwa yanaweza kuwa kero.Na hali ikifikia hapo,basi sio vibaya kukumbushana kwamba hapo sipo na mambo kama hayo.Maisha lazima yawe na uwiano.Kukumbushana tunapoteleza,kusifia inapobidi na siku zote kuwezeshana.

Sikiliza wimbo huu mpya kutoka kwa MwanaFA akiwa ameshirikiana na Lady Jay Dee.Wimbo unaitwa Msiache Kuongea. Katika chorus sikiliza kwa makini kwanini Jide na FA wanasema Msiache Kuongea.Kisha sikiliza kwa makini mashairi yaliyomo.Kazi nzuri FA na Jide.



 

“KARIBUNI RAINBOW CLUB”-BONNY LUV January, 19, 2009

Filed under: Burudani,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:37 PM

bonnybc1Endapo kila ifikapo mwisho wa wiki umekuwa miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakijiuliza waende wapi wawapo jijini Dar-es-salaam,BC leo inakuletea habari nzuri.Sasa una mahali pa kwenda. Sehemu hiyo inaitwa Rainbow na ipo maeneo ya Mbezi Beach ukiwa unatokea Michocheni(Kwa Nyerere).

Yapo mambo mawili ya msingi ambayo yanaifanya Rainbow kuwa kimbilio la wapenda burudani jijini Dar-es-salaam.Kwanza klabu hii ndio itakuwa “kijiwe” maalumu kwa wale wenzangu na mie ambao wanapendelea miziki ya “Old School”.

Pili burudani nzima itakuwa ikiporomoshwa na kusimamiwa na DJ mzoefu na ambaye katika watu kumi,tisa wanakubaliana kwamba ni moto wa kuotea mbali na anajua anachokifanya linapokuja suala zima la kukata kiu ya burudani. Huyu si mwingine bali ni DJ Bonny Luv(pichani)

bluvbc

Tulipopata habari kuhusu ufunguzi rasmi wa klabu hii,tulimtafuta Bonny Luv ili tujue machache kuhusiana na klabu hiyo maalumu kwa Old School na burudani zingine.Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi;

BC: Kwanza hongera sana kwa kuanzisha joint mpya na karibu tena ndani ya BC.Mambo yanakwendaje?

BONNY LUV: Shukrani sana kaka.Namshukuru Mungu

BC: Tumekutafuta ili tuongelee kidogo kuhusu hii sehemu mpya ya maraha uliyoianzisha.Kwanza ilikuwaje ukaamua kuanzisha disco hili.Uliona mapungufu yoyote kwenye medani ya burudani hususani upande wa disco? (more…)

 

ANSBERT NGURUMO ANAPOJADILI BLOGS January, 18, 2009

Filed under: Blogging,Blogs,Mtandao,Uandishi — bongocelebrity @ 1:50 PM

ansbert-ngurumobcJina la Ansbert Ngurumo sio geni hata kidogo miongoni mwa wapenda habari na mawasiliano na hususani wapenzi wa habari za magazetini. Ansbert ni miongoni mwa waandishi wa habari mahiri nchini Tanzania ambao wamejijengea sifa na heshima kutokana na kazi zao za uandishi wa habari.

Safu yake ya Maswali Magumu,inayochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima kila jumapili inabakia kuwa safu yenye wasomaji lukuki huku kila mara ikizua mijadala ya aina yake jambo ambalo ni uthibitisho kwamba sio tu inapendwa bali pia hujibu na pia kuuliza Maswali Magumu.

Ansbert ni blogger mzoefu pia.Blog yake ambayo inaongozwa na kichwa cha habari, Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua, ni sehemu mojawapo nzuri ambapo unaweza kukuta kazi zake za uandishi,mitizamo na pia mikingamo.

Hivi karibuni,jamaa wa mtandao wa Rap21,walifanya naye mahojiano ambayo kwa kila hali ni “must read” kwa mtu yeyote ambaye yupo kwenye fani ya ku-blog au ni mfuatiliaji wa maendeleo ya tekinolojia hii ambayo mimi naiita mapinduzi ya karne katika ulimwengu wa habari na mawasiliano.

Katika mahojiano hayo,Ansbert ameongelea kwa mapana jinsi ambavyo blogs,ikiwemo ya kwake, zinazidi kuboresha mapinduzi hayo na pia jinsi gani blogs zinaweza kutumika katika kuboresha maisha ya wanajamii,kutunza historia zetu,kufichua maovu nk.Bonyeza hapa ili kusoma mahojiano hayo.

 

KWANINI-NURU January, 17, 2009

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 1:15 PM
Tags:

nurumohdbc

Baada ya Walimwengu na Msela, mwanadada Nuru Magram (pichani) hapo jana amefyatua video ya wimbo Kwanini ambao ni miongoni mwa nyimbo 10 zinazotarajiwa kuwemo katika albamu yake aliyoipa jina Walimwengu. Albamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mnano mwezi wa Machi mwaka huu.

Sikiliza mashairi yaliyomo katika wimbo huu,tazama jinsi hadithi iliyomo kwenye mashairi inavyosimuliwa katika video hiyo.Ukiiangalia kwa makini utagundua kwamba lipo jambo moja ambalo sio la kawaida linatokea katika mlolongo wa simulizi hilo.Sio la kawaida kwani katika simulizi hilo kuna mtu ambaye hafanyi kile ambacho wengi wetu tungetarajia afanye.Itazame kisha uniambie kama unaweza kuona nilichokiona mimi.Pata burudani.Kazi nzuri Nuru.