BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KIKWETE MWENYEKITI MPYA AU January, 31, 2008

Filed under: African Pride,Breaking News,Developing News,Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 12:17 PM

Habari ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kwamba Rais Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Afrika (AU).

Rais Kikwete amechaguliwa katika kikao cha 10 cha Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika kilichoanza leo huko Addis Ababa,Ethiopia na kinachotarajiwa kumalizika siku ya Jumamosi Februari 2,2008.Rais Kikwete anamrithi Rais wa Ghana,John Kofi Agyekum Kufuor ambaye amemaliza muda wake.

Kwa kawaida Mwenyekiti wa Umoja huo hupatikana kwa njia ya mzunguko wa kikanda (geographical rotation) ambapo kwa mujibu wa utaratibu huo, Mwenyekiti mpya alitakiwa kutoka miongoni mwa nchi wanachama zilizopo mashariki mwa Afrika eneo ambalo linazo nchi 14 ambazo ni Burundi, Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, Sudan, Tanzania na Uganda.

Raisi Kikwete anayaanza majukumu yake huku akikabiliwa na changamoto nzito kama hii ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Kenya.BC inaungana na watanzania wote kumpongeza Rais Kikwete na kumtakia kila la kheri katika kazi zake yakiwemo majukumu mapya ya Uenyekiti wa AU.Wakati huo huo unaweza kuisoma hotuba ya Rais Kikwete ya kila mwezi,kwa mwezi huu wa Januari hapa (more…)

Advertisements
 

MENGI APATA TUZO YA MARTIN LUTHER KING.

Filed under: African Pride,Mahusiano/Jamii,Tuzo,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 11:24 AM

 

Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi, amepokea rasmi tuzo inayoheshimika ya Martin Luther King. Mengi anakuwa Mtanzania wa nane kutwaa tuzo hiyo. Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.BC inampongeza Mengi kwa tuzo hiyo.

 

FORMERLY KNOWN AS THE EAST COAST TEAM

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Pichani ni baadhi ya wasanii wa kundi lililokuwa likijulikana kama The East Coast Team lililokuwa na makazi yake Upanga jijini Dar-es-salaam.Kundi hili limeshasambaratika.Unadhani kwanini makundi mahiri kama hili ambalo lilikuwa linaonekana kuwa lenye mafanikio huishia kusambaratika?Umoja sio nguvu tena?

Picha kwa hisani ya AY

 

KP DESIGNS January, 30, 2008

Filed under: Fashion Designer,Ujasiriamali — bongocelebrity @ 11:52 AM

 

Baadhi ya mitindo kutoka kwa Masoud Kipanya au KP.Kwa habari zaidi unaweza kutembelea www.kpwear.com.

 

TUNAWAENZI VIPI?

Filed under: Filamu/Movie,Swali kwa Jamii,Utamaduni,Wanawake na Watoto — bongocelebrity @ 12:12 AM

 

Mama Tecla Mjata(pichani)mmoja wa waigizaji wa filamu na michezo ya kuigiza wakongwe nchini Tanzania.Mama Tecla ni mmojawapo kati ya washiriki wa filamu ya Bongoland II kutoka Kibira Films International inayotarajiwa kutoka mwaka huu.Swali gumu ni kwamba,kama taifa,tunafanya nini kuwaenzi wasanii wetu wakongwe kama Mama Tecla Mjata?

 

OLIVER MTUKUDZI NDANI YA TZ HIVI KARIBUNI January, 29, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,News,Sanaa/Maonyesho,Tamasha,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 1:31 PM

Mmoja kati ya wanamuziki magwiji na maarufu barani Afrika,Oliver Mtukudzi “Tuku” kutoka nchini Zimbabwe anatarajiwa kufanya maonyesho “live” jijini Dar-es-salaam na Arusha hivi karibuni.Hii ni nafasi adimu kwa wapenzi wa muziki,hususani wenye mirindimo ya kiafrika kwenda kumuona “Tuku” kama ambavyo wapenzi wake hupenda kumuita,akifanya vitu. Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Bonyeza player hapo chini umsikilize Oliver “Tuku”Mtukudzi katika wimbo wake maarufu Todii.

 

ORIGINAL FIRST LADY

 

Original First Lady,Mama Maria Nyerere,mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Kabla ya kuolewa na Mwalimu Nyerere alijulikana kwa jina la Maria Gabriel Magige.Alifunga ndoa na Mwalimu tarehe 24,Januari mwaka 1953.