BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 3 September, 30, 2007

 

Dada huyu ni mshairi wa kiswahili, anachanganya mashairi na kucheza ngoma za Kiafrika ili kupeleka ujumbe kwa hadhira. Hapa alikuwa akighani shairi aliloandika na kuliita Mama Afrika. Hii ilikuwa pale British Council jijini Dar-es-salaam siku za hivi karibuni wakati wa matamasha ya WAPI( words and Pictures).

Picha imepigwa na Bob Sankofa, mwanablog,mwanaharakati na pia mtengeneza filamu. Hivi tunavyoandika Bob anaomba kura zenu ili aweze kushinda katika tuzo za sinema ziitwazo ZAFAA. Documentary aliyoitengeneza hivi karibuni yenye jina PLAY YOUR PART imechaguliwa kuwania tuzo katika kipengele cha Best Documentary Feature. Mpigie kura kwa kutembelea tovuti ya ZAFAA kwa kubonyeza hapa. Ukifika pale nenda upande wa kushoto utaona palipoandikwa Nominate Here. Bonyeza pale kisha tafuta kipengele cha Best Documentary Feature.Unaweza pia kwenda moja kwa moja kwenye ukurasa wa kupigia kura kwa kubonyeza hapa.Mpe kura Bob Sankofa ili atutoe kimasomaso! Kila la kheri Bob.

Advertisements
 

DR.ASHA-ROSE MTENGETI MIGIRO. September, 29, 2007

Filed under: Bunge,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 5:43 PM

Tarehe 1 Februari mwaka 2007 ni tarehe ambayo Dr.Asha-Rose Mtengeti Migiro hawezi kuisahau kirahisi. Hii ndiyo siku alipokabidhiwa rasmi ofisi na majukumu ya unaibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa cheo ambacho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 kilikuwa hakijawahi kushikiliwa na sio tu na mwanamke yeyote mweusi bali pia mwafrika yeyote. Kwa maana hiyo Dr.Asha-Rose Migiro ndiye mwanamke wa kwanza mweusi kushikilia wadhifa huo na pia mwafrika wa kwanza. Mwanamke mwingine ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kushikilia cheo hicho alikuwa ni mzungu raia wa Canada Louise Frechette ambaye alianza kukitumikia cheo hicho mapema mwaka 1998.

 

Dr.Migiro anayo historia nyingine ya kujivunia. Yeye ndio alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania tangu nchi yetu ilipopata uhuru mwaka 1961. Aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 2006.

Hivi leo Dr.Asha Rose Migiro ambaye ni mke wa Professa Cleophas Migiro na pia mama wa watoto wawili wote wakiwa wakike, ni fahari ya Tanzania. (more…)

 

WANAUME TMK September, 28, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki — bongocelebrity @ 10:29 PM

 

Kwa pamoja wanajulikana kama Wanaume TMK. Makazi yao ya kudumu ni Temeke jijini Dar-es-salaaam. Wao na lile kundi lingine lijulikanalo kama Wanaume Halisi inasemekana hivi sasa ni “watani wa jadi” kama sio washindani wa kudumu.

 

KIFO September, 27, 2007

Filed under: Sanaa/Maonyesho,Sinema,Tanzania/Zanzibar,Utamaduni — bongocelebrity @ 11:43 PM

Leo ni Ijumaa. Utaratibu wetu mpya ni kwamba kila Ijumaa ni wakati wa kupata midundo kidogo,zilizopendwa na zinazopendwa. Kwa kuzingatia kwamba bado tunaomboleza msiba wa mwanasanaa mkongwe,Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma, wimbo wa leo unaendana na maombolezo. Msikilize Remmy Ongala katika wimbo “Kifo”.Ijumaa Njema!

 

 

MZEE GODWIN KADUMA HATUNAYE TENA.

Filed under: Breaking News,Developing News,Filamu/Movie,Sanaa/Maonyesho,Utamaduni — bongocelebrity @ 10:49 AM

 

Habari za kusikitisha zilizotufikia ni kwamba gwiji la sanaa za maonyesho nchini Tanzania Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma hatunaye tena duniani.Habari hizo zinazidi kupasha kwamba mauti imemfika Mzee Kaduma katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa ajili ya matibabu zaidi.Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza(stroke).

Msiba upo nyumbani kwake Bagamoyo jirani na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo. Heshima za mwisho kwa walio Dar-es-salaam zitatolewa kesho (Ijumaa) saa nne asubuhi habari zaidi zinasema heshima za mwisho kwa marehemu mzee Kaduma kwa walio Dar es salaam zitatolewa kesho saa nne asubuhi hospitali ya Muhimbili kabla mwili wake kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Bagamoyo na kisha baada ya kuagwa saa nane mchana utapelekwa kijijini kwake Itamba, Iringa, kwa mazishi. (more…)

 

“UREMBO SIO UZURI”-HASHIM LUNDENGA September, 26, 2007

Filed under: Fashion,Miss Tanzania,Tanzania/Zanzibar,Urembo,Utamaduni — bongocelebrity @ 11:18 AM

Ni vigumu sana kuzungumzia mashindano ya urembo nchini Tanzania hususani yale ya Miss Tanzania bila kumtaja Hashim Lundenga au Uncle Hashim kama ambavyo wengi hupenda kumuita. Sio tu kwamba Hashim Lundenga ndio aliyafufua tena mashindano ya urembo mwaka 1994 bali kampuni yake ya Lino International Agency Limited ndio haswa mratibu wa mashindano hayo ambayo kila mwaka yanazidi kuwa maarufu na hivyo kuwa tukio linalosubiriwa kila mwaka kwa hamu.

Kwa mwaka huu wa 2007,mashindano ya Miss Tanzania huenda yakawa yameandika historia mpya kabisa nchini Tanzania. Mshindi wa mwaka huu,Richa Adhia, ni mtanzania wa kwanza mwenye asili ya Asia (India) kutwaa taji hilo.Isitoshe ushindi wake umepokelewa kwa hisia tofauti miongoni mwa watanzania jambo ambalo limebakia kuwa gumzo mpaka hivi leo.

 

Sasa ili kujua kwa undani kuhusu mashindano haya ya urembo huna budi kumuuliza Hashim Lundenga.Hivyo ndivyo tulivyofanya hivi karibuni katika mahojiano naye ambapo aliweka wazi nini kilimsukuma kufufua mashindano haya, anasemaje kuhusu ushindi wa Richa Adhia na nini watanzania tutegemee kutoka katika mashindano ya dunia (Miss World) mwaka huu? Pia Hashim anajibu swali ambalo limekuwa likiulizwa sana na wananchi;Je mashindano ya urembo ni kwa watoto wa “vizito’ peke yao?Haya hapa mahojiano kamili; (more…)

 

LADY JAYDEE & BANANA ZORRO September, 25, 2007

Filed under: Bongo Flava,Muziki,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 11:42 PM
Tags: , ,

Pichani ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Banana Zorro na Lady Jaydee. Wasanii hawa ni miongoni mwa wasanii wachache wa muziki wa kizazi kipya ambao wanamiliki bendi zao na hivyo kutoa burudani “live” katika maonyesho yao. Banana Zorro anamiliki B Band wakati Lady Jaydee anamiliki Machozi Band. (more…)