BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ZUWENA-MARIJANI RAJABU NA DAR INTERNATIONAL November, 30, 2007

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Ni ijumaa tena,ijumaa ya mwisho ya mwezi Novemba 2007.Mwaka unayoyoma,umri nao unazidi kupaa.Siku hazigandi kama alivyoimba Jide.Ni wakati mwingine wa burudani.Wiki inapoelekea ukingoni sharti uburudike kidogo.Maisha yenyewe mafupi haya.

Leo tunaye “Jabali la Muziki”,Marijani Rajabu na bendi aliyotamba nayo sana ya Orchestra Dar International.Wimbo unaitwa Zuwena. Hii ni mojawapo ya zile classic maarufu za Marijani na Dar International.Pata burudani.

Pichani ni “Jabali la Muziki” alipokuwa mdogo kabla hajaanza shughuli za muziki.Picha hii ni kwa hisani ya Issa Michuzi.

Wakati unaburudika na muziki,hebu soma kibwagizo kifuatacho ambacho msomaji wetu mmoja ametutumia.Endelea hapa ili ukisome kibwagizo chenyewe.Samahani kwa wale wasiotumia kiingereza.Ijumaa Njema. (more…)

 

KILA LA KHERI RICHA November, 29, 2007

Filed under: Miss Tanzania,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 2:32 PM

 

Hivi sasa yamebakia masaa machache tu kabla ya fainali za shindano la kumtafuta mrembo wa dunia (Miss World) zifanyike huko Sanya nchini China.Tanzania inawakilishwa na Richa Adhia.Shindano la mwaka huu ni la 57 tangu kuanzishwa kwa mashindano haya. Nchi 106 zikiwakilishwa na warembo wao 106 wanashiriki shindano la mwaka huu.

Kuna mambo 100 kuhusu Miss World 2007 ambayo tunadhani wapenzi wa masuala ya urembo wa dunia wangependa kuyajua.Bonyeza hapa ili uyasome.BC inamtakia kila la kheri Richa Adhia.

Picha kupitia kwa Issa Michuzi.

 

FIRST PRIME MINISTER.

Filed under: Historia,Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Jina la “Simba wa Vita” ndio jina ambalo watu wengi wamekuwa wakilitumia kumtambulisha mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa (pichani). Huyu ni miongoni mwa viongozi wa mwanzo kabisa wa Tanzania ambao mpaka hivi leo bado,siku moja moja,huwa wanajumuika nasi katika matukio mbalimbali ya kitaifa.

Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza nchini Tanzania na baadaye kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.Alizaliwa mwaka 1926 katika kijiji cha Matepwende Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Tanzania. Alianza elimu ya Msingi huko LiwaleLindi mnamo 19411942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Dar es Salaam Secondary School.

Simba huyu wa vita,katika kipindi chake cha uwajibikaji,alishika nafasi mbalimbali za ki-uongozi.Ukitaka kuzijua nafasi mbalimbali alizowahi kushika tafadhali bonyeza hapa kwa CV yake kamili.

Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.

 

KWA PAMOJA WANAITWA NYUKI DJz. November, 28, 2007

Filed under: Burudani,DJs,Muziki,Watangazaji — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Tumewahi kusema siku za nyuma kwamba tofauti moja kubwa baina ya watangazaji wa radioni na wale wa kwenye luninga ni kwamba hawa wa kundi la pili huwa tunapata nafasi ya kuziona sura zao mara kwa mara.Wakati mwingine hata kila siku ikiwezekana kutegemea na kile anachokifanya mtangazaji huyo wa televisheni.

Hali hiyo ndiyo inayosababisha muendelezo fulani wa uhusiano (mtangazaji na msikilizaji) pindi ikitokea ukakutana nao mitaani au katika shughuli fulani au japo kuwaona katika picha kama unavyoweza leo kuwaona kundi hili la Djs wa Clouds FM ambao kwa pamoja wanajulikana kama Nyuki DJz.

Kutoka kushoto waliochuchumaa/kaa ni Steve B,Dj Too Shot,Dj Fetty,Mully B,na waliosimama toka kulia ni Pitter Moo,DJ Venture pamoja na Dj Nelly.

Picha kwa hisani ya MichuziJR.

 

MTANZANIA ATWAA UBINGWA WA DUNIA. November, 27, 2007

Filed under: Michezo,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:20 PM
Tags: , ,

 

Bondia wa Tanzania,Japhet Kaseba (kulia) ambaye ni bingwa wa mabara, jumamosi iliyopita aliibuka bingwa wa dunia (WKL) katika mchezo wa kickboxing baada ya kumtwanga bondia kutoka India,Abhijeet Pektar (kushoto) katika raundi ya kwanza,ambapo pambano hilo lilikuwa la raundi tano lililofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-es-salaam.BC inaungana na watanzania wote katika kumpa pongezi Japhet Kaseba.

Picha na habari hii kwa hisani ya MichuziJR.Picha ilipigwa ukumbi wa Maelezo jijini Dar siku moja kabla ya pambano wakati wakitambulishwa kwa waandishi wa habari huku kila mmoja akijinadi kumshinda mwenzie.

 

TULIPOONGEA NA RITA PAULSEN.

 

 

Ukizungumzia wanawake wajasiriamali(entrepreneurs) nchini Tanzania,huwezi kukosa kumtaja Rita Paulsen (pichani),Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni maarufu ya Benchmark Productions yenye makao yake makuu jijini Dar-es-salaam.

Rita ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 12 kwenye masuala ya utengenezaji matangazo na masoko,sio tu ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo yenye mafanikio nchini Tanzania na kimataifa, bali pia ni mmojawapo wa majaji katika show maarufu ijulikanayo kama Bongo Star Search. Show hiyo ambayo hivi karibuni imezidi kujipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania,ni ubunifu mwingine mahiri wa Rita na kampuni yake ya Benchmark Productions.

Show hiyo ambayo hurushwa kila jumapili mara tu baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku kupitia kituo cha televisheni cha ITV,inasemekana ndio show ambayo ni “very interactive” nchini Tanzania kwa maana ya kwamba inampa mtazamaji nafasi ya kutoa maoni yake au dukuduku lake wakati huo huo inapoonyeshwa. Hilo linawezekana kwa kutumia tekinolojia za kisasa za simu,sms nk.

Hivi majuzi BC ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na show hiyo. Katika mahojiano haya Rita anaweka wazi mustakabali mzima wa show hiyo na pia kutoa ushauri makini kwa vijana wa muziki wa kizazi kipya kuhusiana na kazi zao za kisanii na maisha kwa ujumla.Pia anajibu swali ambalo limekuwa likiulizwa na wengi;kwanini wakati mwingine majaji wa Bongo Star Search huwa “wakali” namna hiyo??!Fuatana nasi katika mahojiano hayo. (more…)

 

USHAIRI WA MRISHO MPOTO. November, 26, 2007

Filed under: Burudani,Sanaa/Maonyesho,Uandishi — bongocelebrity @ 12:05 AM
Tags: ,

Jina Kamili: Mrisho Mpoto.

Jina la Utani/Lakabu: Mjomba.

Mahali na Tarehe ya kuzaliwa: Songea, tarehe 27-10-1978.

Shule nilizosomea: Shule ya Msingi-Ilala Boma.Sekondari-MESAC

Jiji/Mji nilipendalo: Warsaw,Poland.

Chakula Nikipendacho:Wali na Maharage.

Wimbo Niupendao: Salamu Mjomba.

Filamu ambayo sitokaa niisahau: South Central.

Michezo/Mchezo niipendayo: Kuogelea.

Wasanii niwapendao: Wote wanaotumia fikra katika kuishi na zaidi Poets wote.

Siku niliyokuwa na furaha zaidi maishani mwangu: Nilipopata VISA ya kwenda Marekani wakati sikujua kuongea kiingereza.

Siku iliyokuwa ya huzuni maishani mwangu: Nilipopata mafanikio makubwa katika maisha yangu ya sanaa.Nilipofanya onyesho langu watu wakajaa mpaka wengine wakakosa nafasi ya kukaa na tiketi zote zikawa zimeisha. Kumbe ilikuwa ni ndoto tu.Hiyo siku naikumbuka sana maishani mwangu.

Msemo uniongozao(Life Motto): “Huwezi kwenda kwa jirani kama hukutokea kwako”.Ngugi

Huyo ni Mrisho Mpoto,mshairi mahiri,kijana wa kitanzania.Ukipata nafasi ya kumsikiliza akighani mashairi yake, utakubali kwamba “Mjomba” ni gwiji katika sanaa.Tulimuomba Mrisho atupe japo kipande kidogo cha ushairi wake,alitupa kitu kifuatacho (more…)

 

WELCOME HOME PARTY FOR RICHARD. November, 25, 2007

Filed under: Television,Weekend Special — bongocelebrity @ 10:10 AM

 

 

Richard(kushoto) akiwa ndani ya party ya kumkaribisha nyumbani ijumaa iliyopita.Wengine katika picha ni Kinje Ngombale Mwiru(katikati) na Edward(kulia) kaka yake Richard.

Ijumaa iliyopita kampuni ya Multi Choice Tanzania ilimuandalia party ya kumpongeza mshindi wa Big Brother Africa II,Richard Bezuidenhout. Party hiyo ambayo ilihudhuriwa na bongo celebrities wengi ilifanyikia ndani ya Millenium Hotel iliyopo Kijitonyama jijini Dar-es-salaam. Kampuni ya Multi Choice Tanzania ndio wahusika wakuu wa shindano la Big Brother Africa kwa upande wa Tanzania. Kwa picha zaidi za party hiyo mtembelee michuzijr.blogspot.com.

 

PICHA YA WIKI # 11

Filed under: Blogging,Blogs,Photography/Picha — bongocelebrity @ 12:03 AM

 

 

Upigaji picha ni sanaa.Ni sanaa ambayo inaongea.Wenyewe wanasema picha moja ni sawa sawa na maneno elfu moja.Wiki hii picha ambayo imetuvutia na hivyo kuwa picha yetu ya wiki ni hiyo hapo juu ambayo imepigwa na mwanablogu anayekuja juu,Bob Sankofa maarufu kama mwenye macho(MM)

Pichani ni sehemu ya Ziwa Victoria kwa upande wa Uganda (kutokea Jinja) ambako MM alizuru hivi karibuni. Tizama kijani kibichi hicho,tizama mawingu,tizama wavuvi.Tizama…Hii ndio picha yetu ya wiki hii.

 

WATU NA VIATU-NYOTA NDOGO November, 24, 2007

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 11:15 AM

 

 

Msanii kutoka Mombasa-kenya Mwanaisha Abdallah Mohamed a.k.a Nyota Ndogo alipowarusha wabongo na kibao chake kilichotokea kupendwa na kutamba sana kiitwacho Watu na Viatu (bonyeza hapo kuangalia video ya wimbo huo) ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza,jijini Dar hivi karibuni. Nyota ndogo katika wimbo wake huo anasema duniani kuna watu na viatu,kuna watu wana roho mbaya sana,waepuke.Ni kweli?Ukiitazama vizuri picha hii unaweza kuona sura za baadhi ya bongo celebrities.Unaweza kuwatambua?