BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

KISA CHA KWELI? May, 23, 2007

Filed under: Bongo Flava — bongocelebrity @ 12:40 PM

Mojawapo ya videos ambazo sisi wahariri wa BongoCelebrity tumezikubali ni hii ya Mandojo na Domokaya katika wimbo uitwao Dingi. Je hiki ni kisa cha kweli? Mahojiano rasmi yatakujieni hivi karibuni.

Advertisements
 

MJUE FLAVIANA MATATA May, 21, 2007

Filed under: Urembo — bongocelebrity @ 10:32 PM

flaviana.jpg

Kwenye sanaa ya urembo hivi sasa jina linalotajwa zaidi ni Flaviana Matata. Huyu ni mrembo wa kitanzania anayeshiriki mashindano ya Miss Universe ambayo yanatarajiwa kufikia kilele chake Jumatatu tarehe 28 Mei 2007 pale jijini Mexico City nchini Mexico.Yanatarajiwa kurushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha NBC kuanzia saa tatu kamili usiku saa za mashariki (ET). Kwa Tanzania hiyo itakuwa ni saa kumi na moja asubuhi alfajiri.

Lakini Flaviana Matata ni nani? Ni mzaliwa wa Shinyanga-Tanzania.Utotoni alikuwa na ndoto za kuwa daktari ndoto ambazo ziliyeyuka alipojikuta amekuwa fundi-umeme.Anatarajia kuendelea na masomo baadaye ili awe mhandisi umeme (Electrical Engineer). Anasema anamhusudu sana mlimbwende maarufu wa kimarekani anayeitwa Tyra Banks

Kwa habari zaidi tembelea tovuti ya Miss Universe. Picha kwa hisani ya Michuzi.

 

Hasheem Thabeet ndani ya Dar!

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 8:47 PM

Hasheem Thabeet, kijana anayetarajiwa kujiunga na ligi maarufu ya NBA hapo mwakani amerejea nyumbani Tanzania kwa mapumziko ya majira ya joto (summer). Hasheem ambaye anasomea masomo ya Saikolojia katika chuo kikuu cha Connecticut pia anachezea timu ya kikapu ya chuo hicho maarufu kama UConn Huskies.Alizaliwa jijini Dar-es-salaam tarehe 16 Februari mwaka 1987. Nini matarijio yake, anasemaje kuhusu maisha ya Marekani na anajisikiaje kuondoka nchini kama mtu wa kawaida tu na kurejea na umaarufu alionao? Tarajia mahojiano yetu na Thabeet Hasheem hivi karibuni.

Pichani juu ni Hasheem Thabeet akiwa na mama yake mzazi (Rukia Manka) mara baada ya kuongea na waandishi wa habari jijini Dar hivi karibuni.Picha kwa hisani ya Michuzi.