BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MAJOR NYIRENDA HATUNAYE TENA! December, 21, 2008

Filed under: African Pride,Breaking News,Msiba — bongocelebrity @ 1:47 PM

nyirendabc1

Kwa huzuni na masikitiko makubwa tumezipokea habari za msiba wa Major Alex Gwebe Nyirenda.Huyu ndiye shujaa aliyepandisha bendera ya Tanganyika huru na Mwenge wa Uhuru kileleni Mlima Kilimanjaro usiku ule wa mkesha wa Uhuru miaka 47 iliyopita.

Marehemu Nyirenda ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa kwa muda sasa, amefariki jana majira ya saa moja jioni(saa za Afrika Mashariki) katika hospitali ya taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.Mapema mwaka huu Major Nyirenda alipelekwa nchini India kwa matibabu zaidi kufuatia kudhoofika kwa afya yake.

Marehemu Nyirenda anatarajiwa kuzikwa siku ya jumatano ijayo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar-es-salaam.Msiba upo nyumbani kwake huko Mbezi Beach,Flats za National Milling karibu na njia panda ya kwenda Africana.

Ni siku chache tu zilizopita ambapo tuliweka mahojiano tuliyofanya na Major Nyirenda kuhusiana na harakati za uhuru,zoezi zima la sherehe za uhuru nk.Unaweza kuyasoma mahojiano hayo kwa kubonyeza hapa.

Katika mahojiano yale,Major Nyirenda aliongelea mambo mengi.Lakini katika mengi hayo pengine ushauri au usia aliotuachia wa kujitolea,uvumilivu na uaminifu ndio ambao hatuna budi kuufanyia kazi ipasavyo kwa minajili ya kumuenzi Major Nyirenda na pia kwa maendeleo yetu binafsi na jamii zetu.

nyirenda-3

Katika picha hii iliyopigwa mwezi wa pili (February) mwaka huu,inamuonyesha Major Nyirenda akiwa hospitali jijini Dar-es-salaam akihudumiwa na mkewe.Hii ilikuwa ni kabla serikali haijaingilia kati na kumpeleka nchini India kwa matibabu zaidi.Picha na Mpoki Bukuku.

Tunapenda kuungana na ndugu,jamaa,marafiki na watanzania wote kwa ujumla katika wakati huu mgumu wa kuondokewa na shujaa wetu,Major Alex Gwebe Nyirenda.Mungu ailaze pema roho yake milele na milele.Rest in Peace Major Nyirenda.


 

20 Responses to “MAJOR NYIRENDA HATUNAYE TENA!”

  1. Dunda Golden Says:

    POLENI NDUGU WAFIWA NAMI PIA KWANI MSIBA WETU WOTE
    NDUGU JAMAA NA MARAFIKI

  2. Joseph Mbele Says:

    Nakumbuka wakati alipopandisha mwenge juu ya mlima Kilimanjaro. Nilikuwa nimemaliza darasa la tatu. Kitendo chake hicho kilisisimua kizazi chetu, na ile hotuba ya Nyerere kuhusu azma ya Watanganyika kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya mlima Kilimanjaro ilichochea hisia za utaifa nchi nzima. Ni hotuba fupi iliyosheheni hisia za kishairi na mvuto mkubwa. Mawaidha aliyotoa Meja Nyirenda kwenye mahojiano na Bongo Celebrity ni muhimu, kwa watoto wetu na kwa Taifa kwa ujumla. Nasikitika shujaa huyu ametutoka. Anastahili kuzikwa kwa heshima zote za kiTaifa. Natoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu. Mungu awape nguvu ya kustahimili shida hii, na amweke mahali pema Peponi shujaa wetu huyu. Amina.

  3. rasto Says:

    mwenyezi mungu ailaze roho yake pema peponi

  4. Ray Says:

    kweli jamani nilimuon wakati uke kabla hajapelewkwa mumewe muhimbili.tumuombee shujaa wetu

  5. binti-mzuri Says:

    poleni sana to wafiwa and tanzanians in general

  6. Majita Says:

    RIP Nyirenda.

    Mimi nitakukumbuka Sana HASA nikikumbuka picha hii ya BC iliyokuwa kwenye kitabu cha kiswahili darasa la sita (STD VI) enzi zetu na mwlwangu alivyokuwa anakusimulia ushujaa na ujasiri wako.
    AMEN

  7. Dinah Says:

    Aah! Mungu awape uvumilivu wafiwa kwenye kipindi hiki kigumu.

  8. Kama Mungu ameamua kuwa naye ni kwa kuwa amekamilisha aliyohitaji afanye. Nasi tunaendelea kumlilia kwa kuwa tunaendelea kumhitaji. Lakini ukweli ni kwamba alitekeleza yale aliyotakiwa kufanya kwa wakati na nafasi yake na kama alivyotuasa kwenye mahojiano yake na BC, ni kwamba ni wakati wetu sasa kuamka na kutenda yale aliyoamini yanastahili kutendwa sasa. Mungu amlaze mahala pema peponi nasi tumuenzi kwa kusikiliza na kutekeleza ushauri wake kulingana na uwezo wetu.
    Blessings

  9. Mattylda Says:

    ohhh jamani hata mwezi bado tangu tusome mahojiano yako hapa BC, poleni sana wafiwa.

    Kila nafsi itaonja mauti imeandikwa,ni mapito tu!

    PUMZIKA KWA AMANI NYIRENDA!

  10. Dumayai Says:

    RIP major
    Hivi major alipanda mlima peke yake au aliongoza wengine? tafadhali wakuu msaada for that swali ndugu?

  11. Tuliza Says:

    Hii ni kwa ajili ya swali la mdau hapo juu, Dumayai (22 Dec. at 5.55AM)

    Mzee Nyirenda ndiye aliyepewa jukumu la kupandisha Mwenge wa Uhuru na bendera ya Tanganyika juu ya mlima Kilimanjaro. Kulikuwa na farasi mmoja na watu aliofuatana nao. Farasi alifia njiani kabla ya kufika kileleni sababu hakuhimili baridi kali. Watu alioongozana nao walikuwa ni kama wabeba mizigo na wengine wasaidi wa mzee Nyirenda. Kumbuka kipindi hicho ndio alikuwa ofisa wa kwanza wa kijeshi mtanzania kumaliza masomo ya kijeshini katika chuo kikuu cha cha kijeshi nchini Uingereza, Sandhurst Royal Military Academy.

  12. hombiz Says:

    POLENI SANA WAFIWA NA WAZALENDO WOTE KWA UJUMLA.
    MWENYEZI MUNGU AMREHEMU, APUMZIKE KWA AMANI.
    UMETANGULIA NASI TUNAFUATA
    -VIJANA TUWE WATENDAJI, TUJITOLEE NA TUWE WAVUMILIVU NA WAAMINIFU KAMA ALIVYOSHAURI MZEE NYIRENDA KTK MAHOJIANO YAKE YA MWISHO NA UTAWALA WA BC.

  13. so upset Says:

    wewe tuliza,kuna usemekano jamaa hakuwa mtanzania bali mnyasa

  14. watubwana Says:

    siri ya mtungi aijuaye ngata,
    BWANA ALITOA,NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.AMEN

  15. BLACKMANNEN Says:

    Mwenyezi Mungu Hutoa! Mwenyezi Mungu Hutwaa! Ndivyo alivyofanya kwa kumtwaa Shujaa wetu “Major Nyirenda” (R.I.P.).

    Katika kuonyesha uwezo wake Mwenyezi Mungu kwa wanadamu. Kupitia miujiza yake ya Kimungu. Aliwatuma Viongozi wa Bongo Celebrity, kwenda kuonana na Major Nyirenda ili kufanya mahojiano ya mwisho naye, kabla hajamchukua, ili atuachie usia wake (Nyirenda) sisi Watanzania kupitia “Blog” hii, na hasa vijana ambao hawakuwa wanaielewa historia yake.

    Wanachama wa BC na wasomaji wake, wameshikwa na simanzi kubwa sana kuliko kawaida, walipopata habari za kifo cha Shujaa Nyirenda. Maneno yake ya kiadilifu, tulikuwa bado tunayazungumza na kuyatafakari katika kiwango cha hali ya juu.

    Binadamu hatuna uwezo wa kuzuia matakwa ya Mwenyezi Mungu. Tutaendelea kumkumbuka Shujaa wetu kwa kila kitu. Iliyobaki ni kumwomba Mwenyezi Mungu Aiweke Roho Ya Marehemu “Major Nyirenda” Pahali Pema Peponi – Amen!!!!

    Black=Blackmannen

  16. Chris Says:

    My condolences to his Wife and hommies. Life has never been easy especially when someone dearly loved by the family and with historical tentacles for the country dies. R.I.P Major Nyirenda.

  17. Gervas Says:

    RIP…interview uliyoitoa hapa, hatukujua kama ndo ulikuwa unatuaga Watanzania. Ingawa umeondoka, Jina na Heshima uliyoiweka kwenye historia ya Taifa letu haitaondoka.

  18. mzushi Says:

    mdau no 13 soma mahojiano ya Major Nyirenda na BC utajua kwanini kuna watu wanadhani ni mnyasa “sasa naamini kweli watz hatusomi” Binafsi namuombea kwa Mungu amlaze mahala pema peponi,Kwetu life lazima isonge na tuyafuate yale yote mazuri aliyotuasia!

  19. Tuliza Says:

    Anon wa 13 hapo juu.. yeye kuwa mnyasa sio tatizo. Amekulia na kulelewa Tanzania. Aliipenda Tanzania, aliitumikia Tanzania, hivyo bado ni mmoja wa mashujaa wetu.

    Haya mambo ya makabila sijui alikuwa wa Malawi tuyaache tu kama yalivyo kwani tukianza kufatilia sana siajabu tutajikuta wengi tuna damu ya Ki-Congo, Msumbiji, Zambia, Malawi, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ugiriki (wakoloni wa mikonga) etc..
    Hata babu yangu mzaa baba ajulikana ni mzaramo, lakini anakwambia baba yake alizaliwa Lubumbashi (Zaire) enzi za ufalme wa kibelgiji.

  20. jessica shayo Says:

    Vinara wetu mnaondoka na kutuwacha wapweke..everything has a reason you will alaways be in our minds and hearts becuase what you did is in unforgetable in the history of TANZANIA..ROHO YA MAREHEMU ILALE KWA AMANI…AMEN


Leave a comment