BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NADYA MOHAMED March, 25, 2008

Filed under: Dini,Fashion,Swali kwa Jamii,Urembo — bongocelebrity @ 12:27 PM

 

Pichani ni Nadya Mohamed,Miss Kinondoni mwaka 2006.Pamoja na kushinda taji la mwaka huo la kitongoji cha Kinondoni,Nadya hakuweza kushiriki mashindano ya Miss Tanzania mwaka huo kutokana na kuzuiliwa na wazazi wake kufanya hivyo kutokana na sababu za kidini.Je unadhani huo ulikuwa uamuzi sahihi kutoka kwa wazazi?

 

57 Responses to “NADYA MOHAMED”

  1. Bablii Says:

    Bc huyu bint ni mzuri wa sura, lakini simfano wa kuigwa katika jamii, Jina lake halisi ni NIMO, lakini kwa kuwa ameliona jina hilo alilopewa wazazi wake ni baya akaamuwa kujiita NADYA, shame on her…! Ni bint na maadali yake lakini akaamuwa kwenda kuvua nguo mbele za watu..akaamuwa kuonesha watu mifupa alopewa na mungu, aliona vazi la stara kwake ni kama moto akaona kutembea na vichupi kwenye jukwaaa ndo ustaarab..

    I always call “a spade a spade , not a big spoon..”

    Bablii

  2. ifi Says:

    hongera wazazi kwa uamuzi mzuri

  3. maria Says:

    mimi nadhani ni sahihi maana hakuwashirikisha toka mwanzo ktk maamuzi yake mbaya zaidi alitumia jina la uwongo ambalo halikuwa lake ili awadanganye wazazi wake na wasijue. watu wengi watachukulia kuwa ni hatua yenye kumdhalilisha binti ila what did she expect akienda kufanya mambo ambayo yanamfanya kuwa public figure? She got a public punishment so what comes around goes around.
    sababu ya kidini sioni kama ni sababu tosha, wazazi wangekuwa wa kweli na kusema hawakufurahishwa na maamuzi ya binti yao ndio maana wameamua kum-punish hapo ingeeleweka zaidi maana wapo wasichana wa kila aina ya imani wanaoshiriki mashindano kama hayo, beauty pageants transcends religion borders.

  4. Gervas Says:

    Nafikiri wazazi saa nyingine tusiwalaumu sana, maana wazazi wengi wanajua u-miss sio profession saingine sio kosa lao ila ni ile picha inayokuwa inaachwa kwa jamii na wale dada zetu wachache ambao wanautumia u-miss kufanya mambo ya aibu kwa jamii. Maana hata mimi ningesita, maana nimewaona wa-miss wengi wanakuwa wazuri kitabia mwanzoni afu wakishavaa tu taji wanaharibiwa na wakwere wenye uchu kwa kuwachezea, maana u-miss wenyewe wanakupa gari ambayo hata pesa ya mafuta huna, kazi hamna nk. ningeshauri kabla ya kushiriki u-miss wawe wamegonga shule walau wawe na professional nyingine.

  5. Saidi Situ Says:

    Hawa warembo wanaweza wakafanya kazi nzuri sana kwenye jamii badala ya kuonyesha private parts zao hadharani. Wazazi wake walikuwa sahihi kwa 100%. Nimefurahi kuona kuwa aliwatii na hakushiriki.

  6. usinijue Says:

    sioni haja ya kuhoji uhalali wa mzazi kumkanya mwanae kufanya jambo ambalo sote tunaliona haliina maana ila ni kuiga tamaduni za weupe tu mmbogo na kutembea nakichupi mbele zawatu wapi na wapi,wala halina udini hilo

  7. Subby Says:

    Sababu za kidini walizotumia wazazi wa Nimo au Nadya kama anavyojiita ni sababu tosha kulingana na maadili ya dini ya kiislam. Kwa sababu umeuliza sababu za kidini nami nitajibu kwa misingi ya kidini. Dini ya kiislam hairuhusu binti aliyebaleghe kuonyesha maumbile yake kwa watu ambao si harim zake, (ambao wanaweza kumuoa). Sasa mashindano ya umiss yanaendana na kuonyesha maumbile ya mtoto wa kike kwa kuvaa bikini wenyewe mnaita beachwear au watoto wa mjini wanaita vichupi.

    Pili katika dini ya kiislamu wazazi ndio walezi na masu-uli. Yaani siku ya hukumu au kiama (Waislam tunaamini kuna siku ya kiama na hukumu) mzazi au wazazi wataulizwa kuhusu malezi ya watoto wao kwani wana jukumu la kuwalea na kuwaongoza watoto wao katika misingi ya dini. Hilo ndilo jukumu ambalo nadhani lilimfanya baba yake Nimo (Nadia) kufunga safari kutoka Arusha kwenda Dar na kufanya kile ambacho aliona kinaendana na misingi ya dini, hasa ukizigatia mzee huyo ni kiongozi wa dini.

    Mwisho naomba kuuliza hivi katika karne hii ambayo wanawake wanadai usawa na kuheshimiwa na kudhaminiwa, nini hasa faida ya haya mashindano ya Umiss? Nataka nijibiwe hili swali na watu wenye mtazamo na uelewa wa feminism na gender rights! Kwanini wanawake waparade nusu uchi? Au wa dance nusu uchi? Huko ndiko kuelekea kwenye usawa wa kijinsia au kuendelea kutumiwa katika matangazo na mashoo kwa manufaa ya watu wachache?

  8. Michelle Says:

    weeee sister weee, kama dini yako hairuhusu kuvaa vichupi mbele za watu acha wazazi wako wasije kukulaani bure, maana hao wenzako wengine hawana dini washakiuka siku nyingi.

  9. Michelle Says:

    Ohhhhhhhh, nilisahau wenzio kina Nakaaya na mdogo wake Nancy kabila yao inawaruhusu kutembea uchi na vichupi.

  10. Kamanzi Says:

    Ninachojiuliza hadi leo ni kwamba hivi hawa mamiss wengine wanaoshiriki hadi mwisho mashindano ya kihuni ya Hasheem Lundenga hawana wazazi pia? Wanasubiri nini hawa wazazi badala ya kuwakataza watoto wao kujitembeza uchi kama wazazi wa huyu mwarabu walivyofanya? Kama swala si kudhalilisha kama wanavyosema miaka yote kwanini wasifanye mashindano wakipita mbele na nguo za heshima? Kwanzan mashindano yalishapigwa marufuku nani huyo kayarudisha tena? Shame on him/her.

  11. Hans Says:

    Hivi ingekuwa ni ni mwanao wa kumzaa anaekuhusu kabisa anatembea na chupi mbele za tv wewe ungejisikia vipi kaka?

  12. queen Says:

    Ninawasifu wazazi wa Nadya kwa kuonyesha malezi bora. pili napenda kutoa kitu kama wazo kuhusu mashindano ya mwanadada bora.kwa nini yasifanyike kitaifa tuu au kiafrika na wakavaa mavazi ya heshima kama vile utamaduni wa mwafrika ulivyo? Kwani ni lazima tushindane na dunia nzima? tunaweza kufanya tuache mkumbo. kuna nchi nyingi pia hazina utamaduni wa kuvaa vichupi mbele ya kadamnasi.tushindane na hizo nchi tusiwadhulumu akina dada vipaji vyao.

  13. kyekue Says:

    Jamni, sasa hivyo alivyovaa kwenye hiyo picha….ushungi wa nini sasa, si uvue tu uwe kama mimi kafiri jamani, hapo ndipo unapojishusha kwa sababu unataka kuwa kwenye dunia mbili kwa wakati mmoja…. amua kuwa moto au baridi unahadaaaa..labda wenzetu umeshaungama nisikuhukumu mwaya labda ishi uwezavyo ndio sera yako

  14. Longolongo Says:

    Haka ka binti kazuri, kanafaa kuwa mke wangu wa kumi na moja.

  15. Harry Says:

    Nadya nilikuwa nakutafuta. Nicheki hgkahama@yahoo.com.
    Mdau- Washington DC

  16. nyarubamba Says:

    Wazazi walichemka jamani lazima tukubali.Ebu mtazame binti mwenyewe mpaka ana tatooes hapo ni sehemu ndogo tu alioonyesha huko kwingine sijui!Sasa kuna udini hapo?Huyu mzazi anajitahidi kumrekebisha mwanae baada ya kuvuka mpaka hatofaulu kabisa pamoja na kwamba hakushiriki lakini bado anashiriki katika mambo mengine.

  17. Ali Says:

    Atakoma kufuata mila sizizokuwa za kiislam, hakubaliki huku wala huku. Hukumu za Muumba zinaanza kumnasa hapahapa duniani. M/Mungu Muongoe., na utuongozee vizazi vyetu

  18. Zyb Says:

    Ndio, huo ulikuwa uamuzi sahihi kabisa. Dini yetu ya kiislam hairuhusu watu kutembea uchi!!! Walifanya busara sana. Mimi kama msichana huwa nachukia sana kwenye hadhara yoyote iwe muziki au mitindo ETI WASICHANA WAKO UCHI IL HALI WANAUME WAMEVAA SUTI HATA KAMA KUNA JOTO LA NAMNA GANI!!!! Huyu dada hakupata washauri wazuri tangu mwanzo. Kwa kujua msimamo wa dini wa wazazi wake asingethubutu jambo hilo bila ridhaa yao.

  19. mtoto wa mkulima Says:

    Hizi dini hizi..sijui zinatupeleka wapi. Ndo maana waafrika tunazidi kuwa maskini. Dini kaleta mzungu na mwaraabu leo ndo tunaoda ndo kipimo cha maadili yetu!

    I believe in indivvidual leberty and freedom. Kila mtu ana haki ya kufanya maamuzi as long as ana miaka kumi na nane..hii ya kutumia dini kuweka maamuzi yako juu ya mwingine si haki.

    Nadya ana haki ya kufanya apendavyo as long as ana umri na akili inayomruhusu. Harafu swala la kubadili jina nadhani ni utashi wa mtu. Hata kama angeamua kujiita chungwa au limao..who cares?

    Tuache hizi mentality za kujifanya kwamba tunajua what is good for others! why impose your values on somebody else?

    Wazungu siwazimii sana, lakini napenda namna wanavyoheshimu liberty ya mtu as long as havunji sheria za nchi. Huyu Nadya wazazi wake wangekuwa justified kumkataza kama angekuwa under 18….eti vichiupi..mbona serikali imeruhusu..na kumbuka mkataba ni kati yetu sisi watawaliwa na watawala. Kwa hiyo kama kitu tumekubaliana nacho..ni uamuzi wa mtu kufanya au kutofanya.

    Lets stop hypocricy kabisa! Huyu dada had all the rights kufanya apendavyo as long as hakumuingilia mtu kwenye anga zake. Hii ya kujifanya kwamba you know morals kuliko wengine naita ni cheap reasoning!

  20. Reg Miserere Says:

    Jamani sisi kama jamii tunapaswa kushirikiana kwa dhati kupinga kudhalilishwa na hasa hasa kujidhalilisha mwenyewe maana hakuna dini inayoruhusu binti au mama kuonyesha maungo yake.

    Ni uasi tu kuona mtu yuko kwenye imani na wakati huo huo anajidhalilisha.

    Heko kwa wazazi, hamna sababu ya kuwalaumu na kufikiri hawajui walilokuwa wakilifanya.

    Jambo la kushukuru naona wachangiaji wengi hawakubaliani na hii tabia.

    Thanks to all and big up………………

  21. Amina Says:

    mi mwenyewe nashindwa kuelewa alikua na maana gani kujibadili jina…..bravo wazazi wa huyu binti nahaya mashindano yapigwe marufuku kabsa

  22. solange Says:

    mhhh mwenyewe nilishangaa kweli nilipomuaona akijiita nadya….heee NIMO….ma dia sijui ulifikwa na nini…..huko kwenu hakuna kideo ukadhani hao wazazi hawatakuona kideoni au bla bla za mahoyoo wenzenu zishindwe kuwafikia wazee wako?mhhh kazi …mtumie na akili kidogo

  23. Panchanga Says:

    Nawapongeza sana wazazi wa Nadya laiti kama wazazi wote wangekuwa hivyo basi naamini hata majanga ambayo yanaendelea kutukumba yasingekuwepo.

  24. sikubaliani Says:

    Huo ni ushungifashion nini? au kujisitiri kwenyewe? ushungi na mabega wazi wapi na wapi jamani ?wazazi mmechukua uamuzi mzuri ila tokea mwanzo alipoanza kujiingiza na kugombea umiss kinondoni hamkujua itakuwaje? je mlitegemea nini ? au vichupi ndio vimewasitua?

  25. msdon Says:

    majina ya kina Nimo ni wasomali,huyu atakuwa msomali hata sura inaonyesha.sasa usomali na umiss wapi na wapi tumezoea kuwaona wasomali wakijifunika gubi gubi

  26. Chris Says:

    Tamaduni hubadilika lakini sio misingi ya dini nafikiri. Wazazi wakikua sahihi lakini nahisi kama hawaku-play their parenthood role tokea mwanzo ninavyoona. It seems walishtuka kuona ameshinda kitongoji cha mwanzo… Na wao wakawa more reactive than proactive as they had to be.

    It’s a challenge kwa wazazi kuwa karibu na makuzi ya watoto. Maana kama aibu alishaifanya,kama kuchojoa alishachojoa Kinondoni kitongoji.

    Ila ni mrembooooooooo…

  27. changa la macho Says:

    Sidhani kama Nadya alitendewa haki.Kesha kuwa mtu mzima na mwenye akili timamu aliyekuwa akiitazama dunia nzima wenzake wa rika lake wanafanya nini katifa mataifa mengine.Alikuwa na malengo ya mbali sana zaidi ya ufinyu wa akili za watu kufikiria utupu na vichupi taswira ya uzinzi ikiwa imegubika nafsi zao!Hivi ni wapi Mwenyezi Mungu aliyemuumba binadamu akiwa mtupu aliko agiza kwamba ni kumtukana Mungu binadamu akivaa chupi awapo katika fukwe za bahari au awapo katika sherehe za kibinadamu ambazo hazihusiani kabisa na ufuska isipokuwa kwa utashi wa binadamu mwenyewe akisukumwa na Ibilisi?Mimi nafikiri wakati sasa umefika kwa Watanzania kutanabaisha Utamaduni wao wa asili kuanzia mavazi katika sherehe na matukio mbalimbali na kuacha kushabikia tamaduni zilizotoka Uarabuni au Uzunguni na kuzifanya ni zetu za asili.Kwa bahati mbaya sana Dini na Tamaduni zimetenganishwa na ‘MSTARI MWEMBAMBA SANA’,na wengi hujikuta wakiuvuka mstari huo bila kujitambua na kujikuta wakichanganya imani za kidini na mila na destruri za watu katika mazingira yao ya asili.TOBA kama nimeziudhi hisia za baadhi ya wale walovuka huo mstari.

  28. Hassan Adam Says:

    HAU

    Aslan hakuna mila wala desturi ya kitanzania niijuayo mimi inayoruhusu msichana kusimamishwa hadharani nusu uchi ili akodolewe macho na halaiki ya watu kana kwamba ni bidhaa inayouzwa, huku akiambiwa mara ageuke huku mara ageuke kule na kutembea “kipaka” na kutingisha nyuma!

    Mitaarafu huyo binti ninayedhani ni Mwislamu, dini yake, kama ilivyokwisha elezwa humu, hairuhusu aslan msichana afuataye maadili ya dini yake kujinadi nusu uchi hadharani huku amevaa kichupi na kijisidiria!

    Tatizo letu sisi Waafrika ni UIGAJI na UTHAMINI wa ya kigeni na kudharau ya kiafrika! Swali ni: Je, tuwaigao (wazungu) huiga tamaduni zetu za Kiafrika na kuziheshimu?

    Wengi wetu tulioko ughaibuni tunaporudi nyumbani, tunashangaa kuona jinsi uzungu ulivyozagaa nchini: toka bungeni (suti na tai shingoni!), muziki (rap!), mavazi n.k.; na jinsi mila na desturi za kikwetu zilivyotoweka na kuyoyoma!

    Niliporudi nyumbani, baada ya kuishi ughaibuni kwa muda wa miaka mingi, nilishangaa kuona jinsi idadi ya “mashombe wa kike” walivyoongezeka nchini! Nikaambiwa kuwa hao si mashombe bali ni dada zetu waliojikwatua kwa kile wanachoita “mikorogo” ili wawe “weupe” na kuvaa nywele bandia za singa (hatujui zilikotoka na zilikuwa za nani!).

    Hiyo ni dhahiri kuwa tunakana uafrika na maumbile yetu ya asili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu, na tunathamini zaidi ya kigeni! Wahenga walisema: “Mdharau asili, si jasiri!”

    Kuhusu haya mashindano ya “uzuri”, utaona kuwa wapendwao zaidi (wanaochaguliwa) ni wale wenye umbo la “kizungu” (wembamba!) ilhali uzuri wa mwanamke wa kiafrika ni ule wa kujaa mwili! Sasa mashindano haya tunawafanyia nani?

    Wasichana “vijiti” wanaonadi mitindo ya nguo ughaibuni, huwa wanajinyima raha ya kula vyakula vizuri ili wajikondeshe. Kumbe wateja wengi wanunuao nguo na mavazi ya kisiku hizi ya wanawake/wasichana ni wale waliojaza mwili walao vizuri!
    Hivi sasa kuna wanaofikiria kuwaajiri wanamitindo wa kike wenye kujazajaza mwili kuliko “fito” tuzionazo zikinadi mavazi!

    Jamani, wakati umewadia wa kuthamini zaidi Uafrika wetu kuliko kuiga tamaduni za kigeni na kujivunia nazo. Tukifanya hivyo, tutaheshimiwa zaidi na wale tuwaigao kuliko kuwaiga watudharauo!

  29. Matty Says:

    Bora huyu kuliko Richa kubadili jina ni maamuzi ya mtu na alikochokosea ni kutowashirikisha wazazi wake tu…ila mrembo sana.

  30. mimi Says:

    dini my fooooooot, hiyo tatoo inakubalika kidini? dini yenyewe ya kiislam???

  31. Subby Says:

    Hapo alipoweka tatoo ni recently na si wakati ule wakati anasoma, nadhani pia hiyo ni mchoro wa hina au piko wanavyoita, nadhani hayuko chini ya wazazi wake kwa sasa, lakini kipindi alichoshiriki mashindano ya urembo alikuwa chini ya mamlaka ya wazazi wake ingawa alikuwa amemaliza form six.

    Swali tulilotakiwa kujibu ni kuwa je ilikuwa sahihi kwa wazazi wake kumkataza kushiriki mashindano ya urembo kwa sababu za kidini, na nafikiri wengi wamelijibu kiufasaha. Sijui anafanya shughuli gani kwa sasa maana hiyo picha nafikiri ni ya mwaka jana kama sikosei.

    Kwa wanaosema kuwa tuangalie tamaduni zetu na si dini zetun kwa kuwa zimeletwa na wageni, basi atuambie ni utamaduni wa kabila gani wenye mashindano ya umiss ili tuufuate na kujua kuwa hii ni sehemu ya utamaduni wa kiafrika.

    Suala zima hapa ni kuwatumia wasichana kama viburudisho kwani watu huingia kuangalia wasichana wanavyoparade na kupimwa uzuri wao, huu ni mfumo dume, kwanini wanawake tu ndio waparade nusu uchi na kupimwa uzuri na kupatikana mwanamke mmoja mzuri kuliko wote duniani? Hizi ni haki za kijinsia kweli, kuna haja ya kuona mapaja, miguu, matiti ya mwanamke ili kupima uzuri wake? Ili iweje hasa? Kwa mtazamo wangu Mungu aliumba wanawake wote wazuri na wanaume wana uzuri wao wa aina yake. Hakuna haja ya kushindana kwa uzuri kwa sababu kila mtu ana mtizamo wake kuhusu uzuri. Uzuri wa kwa mzungu is uzuri kwa mwafrika na ndio maana waafrika wanabidi waende extra mile ili kufikia vigezo vya kizungu sasa kama haya mashindano ya urembo sio mental slavery ni nini?

  32. mimi Says:

    huyo mschichana ni mnafiki,huo ushungi alioufunga ni ushungi wa kinafki,yani kafunga ushungi,nywele zinaonekana,makwapa nje,hlf bado anapita hadharani na vichupi,then watu wanataka wazazi wake wakubali,tena msomali comon guys,lets not mix religion and fashion,uislam una fashion zake lakini zinamtaka mwanamke ajistiri kuanzai juu mpk chini,wazazi wake wako asilimia 2000 correct,its against islam,na huyo msichana alikua anajua kua wazazi wake wasingekubali ndio maana akabadili jina,lakini ulimwengu umemuumbua,asiefunzwa na mama yake hafungwi na ulimwengu,anachopswa na kuomba radhi kwa mungu,na kwa wazazi wake,then aishi maisha anayaopaswa kuishi kwa mujibu wa dini ya kiislam,mwenyezi mungu nimwingi wa msamaha.

  33. sweetoh Says:

    hiyo si tatoo ni piko inayopakwa pamoja na hina, kiislam
    inaruhusiwa mradi anapotia udhu, wakati wa kwenda kusali
    ngozi yake inagusa maji.
    kwa mawazo yangu alichokosea ni
    kuvaa HIJAB nywele na kikwapa nje. Dini ya kiislam hairuhusu hivyo, tunafanya tu.

  34. Anna Says:

    yah you are rigth mimi
    Dini my foooooooot?
    Mnamaaninsha kuwa dini zingine ndio wanaruhusu kuvaa vichupi, mimi sioni kama kwenye umisi kuna kuvaa vichupi, simply ni sports kama sprots zingine,

  35. Queen Says:

    MWACHENI BINTI WA WATU, WENGINE WALOANDIKA MAONI HAPO JUU, HUENDA NDIO MAFUSKA ZAIDI YAKE….

    KABADILI JINA, KATEMBEA UCHI, YOTE MAAMUZI YAKE, NA HAIWAHUSU NYINYI TO JUDGE HER IN ANYWAY NA WAZAZI WAKE….

    GROUP UP… AND LEAVE HER ALONE

    PEACE!

  36. changalamacho Says:

    Usilolijua litakusumbua!Nasikia Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam alimshushia kina Eva wapatao Saba hivi ili aishi nao pamoja.Leo hii nawashangaa sana waliong’ang’ania kuwa na mke mmoja tu kwa wakati mmoja au katika maisha yao yote!Tatizo hivi vitabu vimekuwa vikifutwa futwa mistari kila alipo kuja Mfalme au Mtawala mwingine!Mwenyezi Mungu alikuwa na Siri Kubwa alipompa kila binadamu UTASHI WAKE. utashi huo ungekuwa unafanana kwa binadamu wote dunia hii isingekalika! Wapo miongoni mwetu watakao shabikia na kutetea kwa nguvu zao zote watakapo mkuta Mzee mmoja kijijini akiwa na wake ishirini lakini haohao watakao piga kelele kupita kiasi wakimuona mtoto wa kike akipita mbele yao na nguo fupi sana na iliyobana mauongoni eti kakufuru! VIOJA VYA WALIMWENGU HIVYO? Sishangai, mwanamume jasiri sana kama Julius Ceaser lakini mbele ya mwanamke si lolote si chochote, jeuri hana! WANGEKUWA NA UWEZO WANGEAMURU KILA BINTI AZALIWAE ATOBOLEWE MACHO ILI ASIWAONE WANAUME WENGINE, akichukuliwa na mmoja basi abakie na huyo huyo mmoja. Selfishness, Lust and Greed ‘the most horrible sins’ and the cause of all evils. God Forgive My Pen!

  37. Dignified H. Says:

    Sasa wewe Matty, Richa ameingia vp hapa? Hivi nyie watu mtaacha lini roho dhaifu mlizonazo??, anahusika vipi richa wa watu hapa? Huo ni udhaifu wa kimawazo na kifikra ulionao vilevile

  38. zee la kitaulo Says:

    mimi hiyo sio tatoo ni hina kitu ambacho baada ya muda kinafutika na hina kwa wanawake wa kiislaamu (au wa pwani) ni jambo la kawaida

  39. MTOTO MZURI KINOMA UYO, SIJALI KAMA JINA NI NADYA, NIMO ATA AKIWA ANAITWA TABU. WAZAZI WA KIBONGO WANAZIBA, UMISS SIO UMALAYA. KAMA DEM NI MALAYA NI MALAYA TU ATA AKIWA HOUSE GIRL NDO KWANZA ATADAKWA NA MZEE MWENYE NYUMBA. BONGO AKUNA OPPORTUNITY. KINA NANCY NA FLAVIANA WAMETOKA KTK UKATA WA MAISHA, INAMAANA NAO TUNGESEMA IVYO TZ ANGEIWAKILISHA VIZURI NANI LEO. TUACHENI KUWAZIBIA MABINTI ZETU, NDO TAIFA LETU LA KESHO. UKILETA MAMBO YA DINI MBONA HAO HAO MASHEHE NA MA PADRI WANABAKA WATOTO. WHICH IS WORST. ELIMIKENI NYIE MNAO LETA COMMENT ZENU ZA KUZIBA TU.

  40. Longolongo Says:

    Ki-asili, kila mwanamke mzuri anapendwa na mwanamume.

    Mie sitaki mtu kukashifu au kukosoa imani ya mwingine hapa, Chonde chonde wadau wenzangu; Imani ya mtu ni jambo la ajabu sana ambalo linagusa maisha ya baadaye.

  41. lily Says:

    MIMI NASEMA HIVI HUYU NI MBUZI AMEKATA KAMBA SIKU NYINGI WAZAZI WALISHASHINDWA KUMLEA WASITAKE SIFA KWANI HIYO TATOO HAWAIONI?WASHINDWE

  42. xxxxxx Says:

    huyu binti hata kama amefikisha miaka 18 na ana maamuzi yake lakini anatakiwa aheshimu misingi y a dini aliyokulia na wazazi wake wanasema nini,siyo moyo wake unataka nini,dini hairudishi mtu nyuma hata siku moja,kuna mmoja kasema huko ni kurudishana nyuma kivipi?kwani mtu anafanikiwa kwa kutembea uchi tu?na tusilete hapa habari za mashehe na mapadri,kwani wao ni watu kama watu wengine kwahiyo tushindane nao sbbu wanafanya uchafu na sisi tufanye uchafu..hebu fatilieni kwanza maisha ya kwao yakoje,na mtu huwezi kufanikiwa kama hukupata baraka za wazazi,angeendelea basi kiubishiubishi halafu angeona..mnaotetea ni ujinga..heshimuni dini za wengine hata angekua mlokole angemkatalia mwanae siyo tu waislamu

  43. chikku Says:

    naona uamuzi wa wazazi ni wa busara ukuizingatia na dini ya wazazi wake. azingatie maamuzi ya wazazi kwa ndio mungu wa pili kwake hapa duniani.

    ni binti mzuri kwa kweli

  44. rclicafe kisutu sayz Says:

    sisi tunawaomba wazazi wake wamwache huru ila tu wamshauri kwani jambo hilo la kutembea na vichupi mbele za watu ni kukiuka mila na desturi za dini ya kiislam maana karibu kila mtu anaangalia mashindano hayo sasa wazazi nao wanaona aibu kumuona binti yao anapita na vazi la aibu mbele za watu huku wazazi ni watu wa dini na ni swala tano.

  45. rachel Says:

    hello!
    me naomba niwapinge hao wadau wa rclicafe kwa kweli wabongo mmezidi gele mtu akifanya vibaya mnasema akifanya vizuri pia mnaongea . jamni acheni hizo atuwezi kuendelea wajameni! kila mtu ana uhuru wa kuamua maamuzi yake tanzania ia free country.

    nawatakia siku njema wadau

  46. Juma Rioba Says:

    Zamani(inawezekana hata sasa) katika kabila langu wanawake walikuwa wakiacha matiti wazi na sehemu kadhaa za viungo vyao ambazo kwa sasa tunaviona kama”haramu” kuonekana hadharani!
    Wakati huo, matiti hayo na sehemu zingine “binafsia” hazikutusumbua sana kwani tulijua ni kitu cha kawaida. Kwani tulijua kwamba matamanio na kufanya matendo ya ngono kabla ya kuoa na kuolewa ni zaidi ya kitu kisichowezekana. Hivyo basi hakuna aliyefikiria wala kuwa na wazo kichwani mwake la hata kumsimamisha binti aliyekifua wazi na “nusu uchu” ili kumwambia kwamba kaenda kinyume na maadili ama “kamtega”.Tulichojua ni kimoja-kwamba mambo ya ngono/mapenzi na matamanio hayapo kwani yanahusu rika fulani na kipindi chake kinaeleweka vizuri tu-baada ya kuolewa.
    Hata hivyo baada ya kujua “mema na mabaya”, baada ya maadili kuporomoka, kila mtu anafikiria mambo ya ngono kutokana na sababu nyingi ikiwemo kutokuwa na kazi ya kukukeep busy na kufanya shughuli za msingi,kuchukulia maisha ya magharibi kimakosa kwa kuangalia TV na internet, n.k. Jamii yetu kila kitu siku hizi inakifikiria kimtizamo wa mambo ya ngono!Hata mtu akijitanda mavazi kede kede, bado watu wana uwezo wa kuridhisha nafsi zao yaani ubongo ambao ulishahifadhi picha ya mwanamke/mwanaume “akiwa kama alivyozaliwa” iwe ni sokoni, shuleni, barabarani n.k. Issue sio uvaaji wa wanawake ukoje, issue ni mawazo yako muda wote umeyaelekeza wapi?
    Kila kitu ni mazoea. Ukishaizoeaza akili yako kufikiria mwanamke/mwanaume akiwa kama alivyozaliwa, hata aingie kichakani utachora picha na kuiridhisha nafsi yako kwa kuipa picha ya mwanamke/mwanammne alivyo -akiwa kama alivozaliwa. Wenzetu wa magharibi(simaanishi tuwaige kwa kila kitu kwani nao wana matatizo na tabu zao),wanavaa nguo kutokana na hali ya hewa na sio vinginevyo. Wakati wa baridi utaona watu wamevaa makoti na masweta na makofia. Kipindi hiki kama unaoa kwa kuangalia miguu ya pepsi ama ya bia basi hutaoa kwani wengi wamevaa masuruali na pengine makoti mareefu ya baridi. Wakati wa majira ya joto watu huvaa nguo nyepesi mno na fupi sana. Kwa hapa nyumbani tutasema wanavaa vichupi. Hata hivyo hakuna mwenye muda wa “kuthaminisha” watu wala kufanya matamanio wala kuona “kategwa”” kwani ni kitu cha kawaida. Pia tamaa za kumwona kila mtu na unamtaka si za binadamu aliyeumbwa na kupendelewa kwa utashi tofauti na mnyama(japo hata wanyama wana majira ya kufanya ngono). Kama una shuguli nyingi na za maana, na utamaduni hauruhusu “kuangaliana angaliana” na watu, hutakuwa na muda wa kuwashangaa watu na kusema “wamekutega” ama hawana “adabu” kwa kuvaa walivyovaa.Asiye na maadili ni wewe unayetumia muda wako kumshangaa na hatimaye kumtamani na si yeye aliyevaa ndo mwenye makosa.
    Tuliache hilo. labda niulize hivi: Hivi tunatumia vigezo gani kusema msichana ni “mrembo” ama anafaa kuwa mzuri machoni pa Watu(watanzania)?
    1/je tunatumia vigezo vya wenzetu wa magharibi ama?
    Siku wakisema miss anatakiwa kuwa mzungu tutafika?Wakisema awe na pua nyembamba sana, hivi watanzania wangapi wanayo hiyo?je atamwakilisha nani huko? Je wakisema awe na lips ndogo kama wao tutafanya surgery?
    Kwa nini tusiwe na vigezo vyetu vya uzuri ni nini na tukavifanyia kampeni?Kwani uzuri ni kitu mtu anaambiwa ama kinakuja tu?Hivi wewe unahitaji kuambiwa ni mwafrika na sio mzungu ama unalijua tu kwa “instincts”? Vitu kama tekinolojia na sayansi twaweza kutizama kwao kuongezea na ujuzi wetu kupata sayansi yetu endelevu lakini sio kuambiwa mzuri ni nani na anatakiwa kuwaje. Naamini kwamba kutokana na historia yetu, maisha yetu na jinsi tulivyoumbwa tunajua “uzuri” ni nini na uko wapi. Hatuhitaji kuambiwa, umefika wakati “ku-decenter” vigezo vyao na kutumia vyetu na kusema- basi.Ni bora tuwe tunapeleka miss “bantu” na tunashindwa kila mwaka lakini tunawapa ujumbe kwamba sisi tunauona uzuri ama “umiss” vinginevyo. Baada ya muda watachoka na watafanya kila mbinu kufanya mjumuisho wa uzuri kutegemeana na wapi mabinti wametoka.Mambo mengine kama uwezo wa kufikiri, uchangamfu n.k yaweza kubaki yalivyo japo pia yanahitaji msasa kwani uchangamfu unavyochukuliwa kwa wachina ni tofauti na uchangamfu wa watanzania ama wa watu wa magharibi.Kuna wengine ukitabasamu wanatafasiri tofauti.Kujiamini kunavyochukuliwa kwa wamagharibi ni tofauti na kujiamini kwetu sisi.Kama hawataelewa haya basi tujitoe tufanye u-miss humuhumu kwetu hadi watapotambua baadae kwamba kuna “uzuru” wa aina mbalimbali.
    Najua safari ni ndefu lakini najua urefu wake unasababishwa na Umagharibi kuonekana kipimo cha kila kitu kutokana na uchumi walionao.(center and periphery).Sasa cha kufanya ni nini? Tuache ubinafsi, tufate sheria tunazojiwekea wenyewe, tuwatumie watu wenye vipaji na akili nchini kutuzidi na sio kuwazima. Kumbuka waliovumbua tekinolojia ya kurusha ndege ni wachache mno lakini wanaozipanda leo ni mimi na wewe na wengine wengi.Tatizo letu wenye akili na uwezo tuna wa-“zima” na na kuweka wabovu. Tukubali kwamba binadamu wanatofautina.Tuache wizi na mambo ya “kizamani” ya vikundi vikundi kama vya ukabila na udini. havina mpango na havijawahi kuwa na mpango katika historia ya dunia. Heshima yako inategemea na heshma ya Taifa lako.Ukiwa tajiri na unatoka taifa maskini utadharaulika daima. Utaheshimika daima hata ukiwa maskini lakini unatoka taifa tajiri.Kaaaazi kweli kweli!

  47. mordi Says:

    Binti anataka kustiriwa huyu..sio kulaumiwa ama kupongeza wazazi….sasa? nani yuko tayari? by Mordi from Mombasa, Kenya

  48. mange Says:

    namjibu mdau wa hapo juu aliesema Nimo alijibadilisha jina kwa vile hakupenda jina lake…well, ni kwa vile hamumjua nimo….nimo is proud of her name, anapenda dini yake, anawaogpa na kuwaheshimu wazazi wake na mungu wake…

    mimi ndio nilimbadilisha Nimo jina kwa vile alikataa kata kata kushiriki umiss, nikampromise akibadilisha jina wazazi wake hawatokaa kujua kuwa ni yeye…it worked for a while baadae ikafumka ofcourse.

    nimo hakushiriki ili aonyeshe mwili wake mbili za wake. alishiriki kwa vile she is educated, beautiful, intelligent and she wanted to encourage other women from oppresed cultures that they could stand up for themselves if they wanted to and mainly she participated cos she has a big heart she wanted to reach out to the less unfortunate people and as miss tz or miss world that would have been easy.

    so before judging people know the facts..au sio…

    if theres anybody to blame ni mimi na kamati yangu tulimshawishi mtoto wa watu kushiriki… mwacheni binti wa watu….

  49. mange Says:

    na hiyo tatoo sio real wewe mbea hapo juu…its just a sticker…tafuteni facts jamani..mnaboa

  50. Shuu Says:

    we recho unaongea nini

  51. victor Says:

    Nadia ni mzuri sana,super beautiful!! ange proceed ungekuta yeye ni miss world sasa hivi..ila wazazi wana uamuzi wa mwisho, hatuna choice but ku respect & kukubaliana na uamuzi wao..

  52. ahmed Says:

    this chick! she is fine on her face, blessed with bad manners, habits and all that. she is not good example to community therefore can not qualified to encourage anybody to be like her although she is smart with various talent ” ya kuchuna ma pedegiee” na hapo pichani she is after market only. she is not worth to disscuss at all.

  53. mipigo Says:

    She is just !! Ah ! me can’t finish this.

  54. Ikiwa ni kwa uzuri wake ni bora amuonyeshe Mume wake wa ndoa na sio kuuonyesha mwili wake kwa watu hadharani, mwili wa mwanamke ni kama fitna, sio vizuri kufanya jambo kama hili hasa akiwa ni muislam ni bora amuogope Allah swt na uamuzi wa wazee ni sawa, ikiwa mtu haogopi duniani basi ataogopeshwa kesho siku ya qiyama.

  55. dastala Says:

    Wabongo waache ushamba nipoa kama wazazi hawakufill confotable lakini wabongo walioweka commwnt wasimsakame mtoto wa watu pamoja na warembo wengine, Eti kuvaa chupi first of all ni swimming cloth nyie ham-swim nini au mnaswim na nguo acheni ushamba ndio maana wabongo hatuendelei

  56. Naima Says:

    jamani bfore mcomment mjue ukweli.. Alowaambia hiyo ni tattoo ni nani? Hiyo ni piko na hinna.. Mnapenda kuongea vitu visivokuwa na msingi.. Kubadili jina ni uamuzi wa mtu, ndo maana katika sheria kuna deed poll on change of name… Kuendelea kushiriki. Miss Tz au kuacha ulikuwa ni uamuzi wa nadya.. Akaamua kuwasikilza wazazi wake well and good.. But Kama angendelea ilikuwa between her and her parents..but nyinyi kukoment inawahusu nini?
    I know nadya very well.. Si mhuni Kama mnavyodai.na hui ushungi ni part ya vazi alovaa katika function moja.. I has nothing to do with dini.

  57. watubwana Says:

    ishi maisha yako upendavyo na si wapendavyo,usafi wa mtu si kwa kumwangalia machoni bali moyoni,siri ya mtungi aijuaye ngata.ukipenda boga sharti upende na majani yake.watanzania mmeamua kurudisha mashindano ya miss,basi mkubali na yote yanayofanyika huko,kama kuvaa vichupi,kutembea nusu uchi,ndo mashindano.kama mnaona ni kinyume na maadili ya kitanzania?acheni kushiriki,hamlazimishwi.hizo pesa za kuandaa mashindano saidieni yatima na mtoe misaada kwa wasio jiweza.


Leave a reply to mtoto wa mkulima Cancel reply