BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TUMEHAMA/WE HAVE MOVED February, 24, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 9:00 PM

movedbc

Tumehamia katika makazi mapya.Kututembelea Bonyeza Hapa

We have moved to our brand new house.To visit us,please Click Here.

 

LIYUMBA AINGIA MITINI! February, 19, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 8:55 PM

Zimetanda habari za kushtua kidogo.Habari zinapasha kwamba mtuhumiwa Amatus Liyumba(pichani) ametoweka,hajulikani aliko na heka heka za kumsaka kwa udi na uvumba ndio zimeshaanza? Waliomdhamini wameshaanza kukiona cha moto.Ilikuwaje?Kaenda wapi?Ni kweli?Bonyeza hapa kujua zaidi.

 

MSIBA BOSTON,USA February, 12, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 1:27 PM
Tags:

Ndugu,Jamaa na Marafiki,

Tunapenda kuwajulisha ya kuwa Mzee Leonard NJ Merere ambaye pia ni baba mzazi wa ndugu zetu Naomi na Jacob[JJ] Merere wa Boston-Masachusetts amefariki dunia siku ya Jumanne [Feb 10th 2009] asubuhi hapa Boston,USA.

Marehemu alikuwa  na umri wa miaka 73, ameacha mjane,watoto watatu na wajukuu wanne.

Taratibu na mipango ya  kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es salaam kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa watoto wake huko Boston-Masachusetts.

Kila mmoja wetu anaombwa kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi.

Gharama za kuhifadhi mwili,kusafirisha mwili,Jeneza pamoja na ticket ya atakaye kwenda pamoja na mwili ni dola elfu ishirini[$.20,000].

Ni mzigo mkubwa sana ambao kila mmoja wetu anombwa kusadia ili kukamilisha shughuli hii hasa ukizingatia ya kuwa kwa kadri mwili unavyokaa funeral-home ndio gharama zinavyozidi kuongezeka.

Mwili utasafirishwa punde zitakapopatikana fedha za kulipia gharama.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account ya wafiwa kama ifuatavyo:

NAOMI  MERERE

BANK OF AMERICA,

ROUTE NUMBER :011000138

ACCOUNT NUMBER:009441233628

Au kwa adress hii:

Jacob & Anna Merere

510 Skylinedrive suite # 11

Dracut,MA 01826.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Jacob & Anna Merere [JJ]-978-726-2227 au 978-957-2153.

Naomi Merere-978-413-3722 au 978-632-9823.

Juma Malika-781-244-7353

Saimon Twalipo-978-423-1192

Pastor Abisalom Nasua-214-554-7381

Email-Adress:- RambiRambi@Yahoo.com

Tafadhali chukua muda kuwafariji wafiwa na kuwaombea

Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa kuwasaidia familia Merere !

Mbarikiwe,

Mch.Abisalum Nasua,

Jackson Mollel

Michango-Kwa Niaba ya Marafiki wa Familia ya Merere.


 

ETI HUYU NI NANI? February, 9, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 8:27 PM

pres-kbc

 

X-MAS EVE BASH December, 15, 2008

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 3:37 PM

flyer1bc1

 

Niko fiti-Eve E December, 8, 2008

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 11:06 AM

bc4

Pichani kulia ni Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Eve E akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo jioni kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempisk kuhusiana na onesho lao linalofanyika usiku huu ndani ya gymkana club, na shoto ni mmoja wa waratibu wa onesho hilo kutoka Prime Time Promotions/Clouds Fm Gerald Hando.Eve E amesema kuwa yuko fiti kwenye makamuzi ya leo na ameahidi kuwa wengi waliobahatika kufika uwanjani hapo hawatajutia kiwango cha pesa walichoto kulishuhudia onesho hilo

 

Fat Joe,Eve E kukamua leo usiku gymkana club

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 10:43 AM

bc2 Mwanamuziki wa miondoko ya hip hop kutoka nchini Marekani pichani Fat Joe ametua jana usiku kwa ajili ya onesho lake moja tu linalofanyika usiku huu ndani ya viwanja vya Gymkana club,pichani Fat Joe akielekea hoteli ya kilimanjaro Kempisk  huku akihojiwa na watangazaji wa redio ya Clouds Fm jana usiku.Fat Joe atakamua jukwaa moja na mwanadada Eve E sambamba na kundi la P-Square kutoka nchini Nigeria,katika onesho hilo kiingilio kimepangwa kuwa 10,000/= na 15,000/= kwa kila kichwa

 

BINADAMU HANA WEMA/SHUKRANI KWA MJOMBA-OSS December, 5, 2008

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 12:05 AM

binadamubcTunapozungumzia wasanii kama kioo cha jamii, huwa tunazungumzia jinsi ambavyo msanii anaweza kuyaweka matatizo ambayo yanamkumba yeye binafsi au jamii inayomzunguka katika mfumo wa kisanii (muziki,maigizo,ngonjera,ushairi nk),huku akitanabaisha mambo kadha wa kadha kwa minajili ya kuonya, kukanya na hata kuelimisha juu ya hali halisi iikumbayo jamii bila kusahau kuburudisha.Hivyo ndivyo sanaa ilivyo na inavyotakiwa kuwa.

Tunapofunga wiki,kama kawaida ni wakati wa burudani,wakati wa zilipendwa.Kwa wengine ni wakati wa mapumziko huku wengine ukiwa ni wakati wa moja moto,moja baridi mbele ya kaunta huku wakiagiza nyama choma kwa mbwembwe.Mwezi bado mchanga huu kwa hiyo wenye nazo bado wanazo.Hakuna anayelia ukata bado.

Leo turejee kwa wana Orchestra Safari Sound enzi hizo wakiwa na kina Maalim Gurumo, Hassan Rehani Bitchuka na wengineo wengi ambapo walitokea kuwa moja ya bendi zenye mpangilio mzuri wa vyombo na ubora wa muziki kuanzia mashairi mpaka ala.

Wasikilize hapa katika vibao vyao Binadamu Hana Wema na Shukrani kwa Mjomba. Wikiendi njema.


Burudani na ujumbe wa leo vimeletwa kwenu na Mubelwa Bandio Laurel wa http://changamotoyetu.blogspot.com. Mtembelee.

 

Miss Tazania 2008 Nasreen karim aagwa rasmi leo November, 14, 2008

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 12:12 PM

bcPichani ni Waziri wa mambo ya ndani Mh Laurence Masha ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi miss tanzania 2008 Nasreen Karim bendera ya uwakilishi katika hafla fupi ya kumuaga rasmi  mlimbwende huyo wakiwemo na wadau mbalimbali wa urembo na kutakiwa kuwa balozi mzuri katika mashindano ya Dunia yatakayofanyika Afrika Kusini baadaye mwezi ujao.Wengine pichani shoto ni mkuu wa mfuko wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba,nyuma ya tukio ni Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) Bw Emanuel Ole Naiko ambaye pia ni mlezi wa  kamati ya miss tanzania,Bw, Hashim Lundega akishuhudia kwa mbaali hivi pamoja na Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Bw Ephraim Mafuru.Hafla hiyo fupi imefanyika leo asubuhi nje ya kituo hicho5Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim akitabasamu baada ya kukabidhiwa bendera ya ubalozi wa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya urembo ya Dunia yatakayofanyika nchini Afrika Kusini baadaye mwezi ujao.

Bongocelebrity inamtakia mlimbwende huyu kila la kheri katika mashindano hayo 

 

WHERE LIFE CAN TAKE US… November, 10, 2008

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 5:46 PM
Tags: , ,

XX ScannedImage016.jpg

Obama na bibi yake.Hii ilikuwa Obama alipotembelea “nyumbani kwao” kwa mara ya kwanza.