BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“USIOGOPE KUCHELEWA,MUHIMU NI KUANZA”-KP February, 14, 2008

Filed under: African Pride,Fashion,Fashion Designer,Mfanyabiashara,Ujasiriamali — bongocelebrity @ 12:10 AM

Kwa wengine bado anaendelea kuwa mchora katuni aliye maarufu zaidi nchini Tanzania.Kwa wengine ni mtangazaji maarufu wa redioni ambaye kila asubuhi huwapa wasikilizaji habari mbalimbali na pia burudani. Lakini kwa wengine,yeye ni mbunifu wa mitindo(fashion designer) ambaye anakuja juu kwa kasi ya aina yake.Huyu si mwingine bali Ali Masoud,(pichani) maarufu kama Masoud Kipanya au ukipenda KP.

Leo hii yawezekana kabisa kusema kwamba Masoud ni kijana mjasiriamali ambaye anajaribu kutizama mbali kushinda maelezo. Ni kijana anayependa kujishughulisha kwa bidii na maarifa bila kuchoka wala kukata tamaa.Mwaka jana alitimiza mojawapo ya ndoto zake za muda mrefu kwa kuzindua lebo/nembo ya KP iliyokwenda sambamba na KP Wear.Hivi leo sio ajabu kukutana na watu mitaani waliovalia nguo zenye nembo na ubunifu kutoka kwa KP!

Kwa mara ya pili,hivi karibuni BC ilifanikiwa kupata fursa ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na sio uchoraji katuni wala utangazaji bali ubunifu wa mitindo. Nini kilimsukuma kuingia kwenye fani ya ubunifu wa mitindo?Unataka kuijua falsafa inayomuongoza katika fani hii?Je anahofia kitu gani zaidi linapokuja suala zima la ubunifu wa mitindo?Nini mipango yake ya sasa na baadaye kidogo?Kwa hayo na mengineyo mengi zikiwemo picha za baadhi tu ya viwalo vilivyosheheni ubunifu wake,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Masoud Kipanya,karibu kwa mara ya pili ndani ya BC.Tofauti na tulipofanya mahojiano nawe kwa mara ya kwanza,safari hii tunataka kuongea nawe kuhusu na kazi zako za ubunifu wa mitindo.Kwanza hongera sana kwa kuanzisha lebo ya KP.Mambo yanakwendaje mpaka hivi sasa? Watu wameipokea vipi KP?

KP: Namshukuru sana mola, watu wameipokea vizuri sana sana sana KP ingawa bado kuna wachache ambao wangali wamepigwa na butwaa wakiamini kwamba ninachofanya ni kununua nguo na kuweka lebo. Naomba nitumie nafasi hii kuwaambia kuwa sisi sote, hasa watu weusi, tumepewa uwezo wa hali ya juu kifikra, kinachotukwamisha ni kutojiamini na kujidharau.

BC: Unaweza kutuambia nini kilikusukuma kuanzisha lebo ya KP?Ulifikiaje uamuzi wa kuiita KP?

KP: Ni muda mrefu sana nimekuwa nikitamani kuona mtu ama watu wakiwa wamevaa kitu nilichotengeneza mimi.Na hili lilipata msukumo zaidi katika miaka hii ambayo nimekuwa nikichora. Mara zote tunapochora watu lazima uchore na nguo, hili lilipelekea kutamani kuona mtu wa kweli akiwa amevaa nguo niliyoibuni.

KP imetokana na KIPANYA, na huwezi amini, Marehemu Amina Chifupa ndiye aliyekuwa akinikatisha kwa kuniita KP tulipokuwa katika vipindi vya watoto miaka ya nyuma, hivyo nikaamua kulisajili na kulitumia kama lebo ikiwa na kichwa cha Kipanya mwenyewe.

BC: Kumekuwepo na maswali mengi sana kuhusiana na mchango au involvement nzima ya mbunifu wa mitindo(fashion designer) kama wewe katika zoezi zima la kutengeneza nguo,yaani kuanzia mwanzo mpaka inapofika dukani.Unaweza kutuambia kwa kifupi jinsi wewe mwenyewe, kama Masoud Kipanya, unavyoshiriki katika zoezi zima.

KP: Asante kwa swali zuri ambalo litazidi kuweka wazi mchakato mzima.Ninachofanya ni hivi; kichwani nakuwa na aidia ya dizaini ya kitu husika, iwe ni shati au tshirt au jeans au chochote, kisha nachora katika karatasi na ku-save kwenye cd, kwa kuwa huwa natengenezea nje. Nikifika kule huwa naenda katika masoko makubwa ya material, kisha nachagua huku nikijua kuwa kila material ninayonunua itakwenda kutumika katika mchoro fulani.

Baada ya hapo nakwenda katika factory zinazotengeneza lebo, kuanzia vigozi vya jeans mpaka vifungo vikubwa vya jeans vikiwa na logo ya KP. Then nakwenda viwandani nikiwa na lebo na dizaini ninazotaka.Within a week wananitolea sampo, nikiipitisha wana-produce kwa idadi ninayotaka.Ni zoezi gumu linalohitaji commitment ya hali ya juu.

Mtaka cha uvunguni sharti ainame.KP akiwa kazini.

BC: Kila mbunifu wa mitindo huwa na falsafa au mwongozo wake kuhusiana na sanaa ya mitindo.Unaweza kutuambia yako ni ipi?

KP: Falsafa inayoniongoza au ninayoitumia katika sanaa ya ubunifu wa mavazi ni ukweli usiofichika kwamba fashion design has no rule, one can branch out to where no one has ever thought of reaching.

BC: Ni wabunifu gani wa mitindo,ndani na nje ya Tanzania,ambao unadhani kwa njia moja au nyingine wamechangia kuikuza sanaa yako ya ubunifu wa mitindo?Kivipi?

KP: Wabunifu wa ndani walionitangulia wamenisaidia sana kwa ku-pave the way.Hawa, akiwemo khadija Mwanamboka na Mustafa Hassanali, wamewafanya watanzania wengi japo kwa taratibu kuanza kutuamini. Wa nje wengi wao wamekuwa wakinipa usongo wa kutamani kufanya wanayoyafanya, (sio kutamani kuwa shoga ohooooo!!!)

BC: Nini unakipenda zaidi na nini usichokipenda kuhusiana na kazi yako ya ubunifu wa mitindo?

KP: Kwa kweli nafurahia kila hatua ya kazi ya ubunifu, kinachonikera ni ile hali ya kwenda kuhangaika nchi za watu kutengeneza nguo wakati viwanda tunavyo ingawa vyote vimebinafsishwa na matokeo yake sasa ukiwa na oda ndogo ya $ 20,000 au $40,000 hawakubali kwa vile tu nguo zote wanazotengeneza wana-export kutokana na oda za mamilioni ya dola wanazopata kutoka makampuni makubwa duniani.

BC: Kila binadamu hutokea akawa na rangi(zinaweza kuwa nyingi) anayoipenda zaidi.Kwa upande wako,je kuna rangi fulani ambayo unaipenda zaidi?Kama jibu ni ndio,kwanini?

KP: Brown ni rangi ninayoipenda sana hasa ninapokuwa nafanya painting, naweza nisiwe na sababu za msingi lakini namna ambavyo nikiwa natumia tubes wakati wa kupaint, huwa inanipa raha kuiua kwa mchanganyiko wa rangi za giza ama kuipa nuru kwa mchanganyiko wa rangi zinazowaka.Matokeo ya mchezo wote huu hunipa raha na kunifanya hata kuithamini zaidi rangi ya miili yetu waafrika bila kujutia kwa nini mimi si mweupe.

BC: Hivi karibuni tulipoweka kiunganishi(link) ya tovuti yako ya kpwear.com,kumetokea maoni mbalimbali yakionyesha kwamba watu wengi wanalalamika kwamba bei zako kidogo ni kubwa.Baadaye tulipowasiliana ukaweka mambo sawa kwamba bei zilizokuwa kwenye website zilikuwa zimekosewa au kubandikwa tu kwani tovuti bado ipo matengenezoni.Unaweza kuchukua fursa hii kuwaambia wananchi juu ya bei halisi za nguo zako na ni katika mazingira gani bei zingine zinaweza kuwa katika fedha za kigeni?

KP: Kwanza kabisa naomba niwaombe radhi kwa usumbufu uliojitokeza, kwa wale ambao wameshafika dukani kwangu pale Millennium Towers watakubaliana nami kwamba bei zangu ni za kawaida. Naomba nisisitize, jeans ni wastani wa shilingi 30,000 mpaka 36,000 tu, kwa kifupi hakuna nguo ya shilingi 40,000,zote ni chini ya hapo.

Kilichotokea katika website ni kwamba iko katika matengenezo ili tuwawezeshe walioko mbali waweze kununua online.Bahati mbaya webmaster wangu akaweka bei zile kama mifano, na sikujua kama zingeweza kuwapotosha watu.

Gharama za nguo zitaongezeka nadhani kidogo kwa wale watakaokuwa wanaagiza kutokea mbali kama America, Ulaya na Asia. Hii itatokana na gharama za shipping ambazo nina hakika wote tunazifahamu, hata hivyo haitofikia bei za kutisha.


BC: Unaweza kutuambia matumizi ya mtandao wa internet yanakusaidiaje au yamekusaidiaje kufikia hapo ulipo kama mbunifu wa mitindo?Unaitumia vipi internet kwa kazi zako za ubunifu wa mitindo?

KP: Internet imenisaidia sana kuzitangaza nguo zangu, blogs na websites kama hii ya Bongo Celebrity zinasomwa na watanzania wengi ndani na nje ya nchi.Na ni kwa kupitia mitandao hii ndipo nitakapoweza kuuza nje ya nchi, kwa hilo nawashukuru wajanja waliotutangulia katika teknolojia na ninyi wenye mitandao hii, Mungu awabariki sana.

BC: Wabunifu wengi wa mitindo wamekuwa wakisikia fahari pindi mtu au watu fulani maarufu wanapoonekana wakiwa wamevaa nguo walizozibuni wao.Kwa upande wako,unajisikiaje unapoona celebrity fulani amevaa nguo zako na ungependa siku moja kumuona celebrity gani ambaye bado hajavaa nguo zako akifanya hivyo?

KP: Kwangu iko tofauti kidogo.Celebrity mmoja si sawa na watu kumi wa kawaida.Hivyo basi kiu yangu ni kuona watu wengi wa kawaida wakivaa nguo zangu.Sina tatizo celebrity akivaa nguo zangu, ila kwangu mtu wa kawaida akiikubali nguo yangu nasikia raha kupita kiasi.

BC: Ni kitu gani unachokihofia zaidi kuhusiana na sanaa au kazi yako nzima ya ubunifu wa mitindo?

KP: Nawahofia zaidi mabingwa wa kufoji!! Ingawa kila kitu kitu kimekuwa registered, bado kuna maeneo ambayo watu wanaweza kufoji kwa quality ya chini na kupelekea kuharibu jina la KP.

BC: Katika muda mfupi tu KP imeanza kutanuka na hivi sasa viwalo vinapatikana mikoani.Wakati huo huo umetudokeza kwamba una mipango ya kuhakikisha kwamba KP inakuwa ya kimataifa zaidi na hivyo kupatikana sehemu nyingi duniani.Unaweza kutueleza kidogo kuhusu mipango hiyo?

KP: Yes, kwa kuanzia ukiachilia mbali mikoani ambako nimekuwa nikisogea kama Dodoma, Mwanza na Mbeya huku mipango ikiwa ukingoni kwa Arusha na Tanga.Nategemea kutumia marafiki zangu walioko sehemu mbalimbali duniani kuwa kama mawakala kwa ajili ya kuwafikishia nguo za KP ndugu zangu watanzania na marafiki zao popote pale ulimwenguni. Pia nawakaribisha watanzania mbalimbali walio na maduka ya nguo nk popote walipo ulimwenguni kuwa wakala wa KP.Wawasiliane nami tuzungumze zaidi.

BC: Unatoa ushauri gani kwa vijana au wabunifu wa mitindo wanaochipukia hivi sasa?

KP: Wasiogope, na wala wasikubali kukatishwa tamaa, na hili haliishii kwa wabunifu tu, kwa fani yoyote ile.Ndoto yoyote uliyokuwa nayo inawezekana kuwa kweli. Usiogope kuchelewa, muhimu ni kuanza.Usiishie kuwa na wazo tu bila ya kulitekeleza.

Katika walet yangu natembea na kipande cha karatasi nilichokikata miaka mitatu nyuma, kimeandikwa…You can not get anywhere unless you start.Anza na utashangaa milango ya kupita itakavyokuwa inafunguka kadri unavyoikaribia. Yaani hamjui ni kiasi gani nayapenda haya maisha.

BC: Asante kwa muda wako KP.Tunakutakia kila la kheri katika kazi zako.

Original from KP
Just from KP.
Like what you see?Mtembelee KP dukani kwake pale Millenium Tower jijini Dar-es-salaam ujipatie viwalo vyako.

 

81 Responses to ““USIOGOPE KUCHELEWA,MUHIMU NI KUANZA”-KP”

  1. Mwana wa mkulima Says:

    Big up mkuu!

    Vijana kama nyinyi ndo mnaliendeleza gurudumu la uhai wa taifa letu. Iam so proud of you my man! Iam sure nikija hapo dukani kwako nitatafuta hata chansi ya kununua shati! Youa re an inspirational man. Wengi hatujui, maisha ya siku hizi ni kufight and you have to BELIEVE AND WORK FOR YOUR DREAMS! Wengi tunakata tamaa mapemaaaaa!

    All the best KP and I really wish you the very best.

  2. mamanye Says:

    sina la kusema nimekuwa nikifuatilia maisha yake tangu enzi za kipindi cha chuchu yeye na Bonda na Marehemu Amina. Nilikuwa mtu mzima lakini nilipenda kipindi cha watoto kama mwalimu na sasa napenda kipindi chao cha Power Breakfast 88.4 kama mtaalam wa masuala mengine. Ninaimani atakuwa na lebo hiyo kwenye manunuzi ya suti kwani haitawezekana kuvaa jeans na T-shirt ofisini na Bungeni!!
    Tuangalie na sisi wa kundi hilo.

  3. Mama wa Kichagga Says:

    KP,

    Nakukubalia 100%. Kaza mwendo utafika, omba uzima hakuna lisilowezekana.

    “Make your business sustainable”

    Nitakutembelea dukani.

  4. Leila Says:

    Aminia KP you have DONE IT Inshallah kila la kheri naamini Mola atajaalia tu. Kukubalika kwako na jamii ni Faraja na FAHARI kubwa kwa Watanzania nje na ndani ya Bongo Keep it Up Mchizi wangu.

  5. Sura si Mali Says:

    Ukiwa kama kioo cha Jamii, hupaswi kutoa comments kama uliyotoa hivi karibuni juu ya Beaty and Beast. Hii imekushusha sana sifa sana Bwana Kipanya.

    Mfano usingekuwa vizuri mimi nianze kusema chapati ukunji!!!!!!!

    Jirekebishe, Nilikuwa nakufagilia sana sana yaani nilikuwa shabiki wako lakini si sasa.

  6. zawad haji Says:

    Hongera Kp uko juu brother,ungefanya matangazo na hata kwenye television ili hata wale wasiotembelea bc waone kazi zako.

  7. nas Says:

    Big up mzee,,really appreciate ur work,,keep it up.B blessed.

  8. Impokochole Says:

    Mimi naongelea kazi yake ya kukaragosi matukio na watu.

    Jamani, ni vema mtu kujua kuwa Wasanii tuko kibao utofauti unaonekana katika jinsi tunavyoutumia usanii wetu kwa ajili ya kujibomoa au kujijenga.

    Kwa kweli kitendo cha juzi cha kumtumelaizi- kidenishi PM wetu kimempandisha graph KP Masoud kutoka 90% hadi 5%

    Na alinichecheta kufuatilia kuinyaka resepsheni yake iliyo katika rekodi za buku la ginesi.

    Nilichokikuta, nilimnyanyulia kofia maana kweli ni mzuri usipime! Amepambwa kwa lips zake za pinki kama naniino ya pink pink!
    Aidha alinivutia sana pia kwa macho yake kama vile yametanakishiwa kwa kazi ya wanyama wadogo wa Mathare wanaopaa, ok kumbe wanaitwa Nairobi flaiz lakini nilipewa tipu toka ndani ya FM kuwa ni kwa ajili ya misosi yake ya nguvu anayoikandamiza mara kwa mara kwa jina Delta-9-Tetrahydrocannabinol aka THC!

    BC hii inatoka hivi hivi bila kuiminya maana anapostahili sifa mtu husifiwa.

  9. Wema Says:

    Yap its good kaka,But mm naweza kununua nguo zko ila mtu wakaida bado fanya ata shs 20000 plz kama itawezekana ili utue mzigo ulete mzingo,Napenda sana kazi yako.Ni hayo tu.

  10. owner Says:

    Of all days jana/juzi sijui ulichemsha nimekushusha graph kabisa. Kitendo cha kumchora vile Mhe. Waziri Mkuu Mizengo sikukipenda kabisa sijui wadau wengine walioona katuni ile kwa kweli. Kitendo cha kumuita Beast huo ni ukosefu wa adabu kwa kweli mbele ya jamii inayokuzunguka. Hata kama ni uhuru wa vyombo vya habari huwezi dhihaki uumbaji wa Mungu kwa kiasi hicho. Imagine angekuwa ni babako mzazi ungejisiakiaje kuitwa beast? Au mwenzetu wazazi wako unawachukuliaje? Kwa kweli huo ni utovu wa nidhamu na umevuka mipaka. Hata kama ni umaarufu si kwa stahili hiyo.

  11. noah gondwe Says:

    BIG UP MY BRO UR SO CREATIVE, EVEN OUR ALLMIGHT GOD SAY IN THE BIBLE “WHEN U DISCOVER UR TALENT U WILL NOT BE POOL” I CAN SAY UR MY ROLE MODE. SALUTE SANA MY BRO

  12. amina Says:

    jamani mi msinichekeshe juzi mi mwenyewe nilikoma na ile katuni ya byuti and the bist huyu mkaka anajiamini sana..sijui alifikiria nini utani umezidi..unamdhihaki prime minister wetu mkuu?we haya

  13. Matty Says:

    Hongera kwa kipaji ulichopewa na mola wetu na ubunifu wako kaza buti!!!!lakini mimi pia huwa sizipendi baadhi ya katuni hasa ya juzi (ni mtizamo wangu tu) haziko sawia hasa kwenye kumkosoa Mola wetu hilo silifagilii kabisa!
    Vinginevyo Kazi nzuri kaka!nitafika hapo dukani kwako japo nifanye windowshopping!

  14. Mwana wa mkulima Says:

    watu mnaolalamika humu, what was wrong with the catoon?

    Kama nyinyi ni watoto wa mafisadi mmetumwa humu, mtajijua..KP is great..Anachorwa Bush na Putin..sembuse Pinda..anayelipwa klodi zetu?? Viongozi siyo miungu watu…and they are public figures as such they are susceptible to public scrutiny! Mpo?? hivi nyinyi mnaishi dunia ya wapi?

  15. Dinah Says:

    Naomba kuuliza hivi huyu ni mbunifu wa mitindo ya mavazi au mmiliki wa lebo ya mavazi?

  16. Angelina Says:

    go bro go….sky is the limit

  17. Swaiba Says:

    Hongera Masudi, keep it up na ubarikiwe. Nitatembelea dukani kwako nione hivyo viwalo. Many thanks

  18. eMbunye Says:

    Ehh kijana wa kichaga chapa kazi. Kweli Wchaga ni watafutaji ni wenye akili haswa. Vijana wengine igeni mfano huo wa ujasiria mali.

  19. Obwatasyo Says:

    Wacha we ukulima wako nani kamwambia Bush & Putin ndiwo kipimo cha kutukanwa au kuheshimiwa

    Ebu usitulinganishie PM wetu na Kichaka aangamizaye dunia kwa mwavuli wa mihimili ya maovu (axis of evils).

    kuhusu huyo MKGB ,
    Bofya hapo chini,
    http://video.google.com/videoplay?docid=-3781931043335299865

    au search kwenye You tube,

    “Litvinenko accuses Putin of Politkovskaya’s murder ”

    Unashuleshwa kwamba, katika majukumu aliyopewa Pinda hakuna kitu kama kuuza ulimbwende au ulembo.
    Hiyo aina ya mdudu wako wa Public Scrutiny peleka huko kwa waandalizi wa Miss Tanzania & Miss Utalii, Mr. Tanzania au kafufue na kushiriki lile shindano la Dr. Ongala na wewe mwenyewe ndio unaondoka kidedea!

  20. kalili Says:

    Dinna ni mmbnifu mwenye lebo yake mavazi.

  21. Dinah Says:

    Asante Kalili. Alafu wewe dogo (KP) kumuita waziri wetu mkuu mbaya sio vema kwani hayuko pale kuonyesha uzuri bali kulitumikia Taifa.

    Yule baba/mzee sio mbaya ni umri au aiana ya maisha aliyokuwa akiendesha ndio yamechangia kuwa na makunyanzi mengi usoni lakini he’s fine ukilinganisha na Yule Ex Spika wa bunge, Arap Moi wa kenya au Obasanjo wa Nigeria…..there are so many things u can chora about na kufikisha ujumbe kwa jamii sio muonekano wa mtu…..subiri na wewe ufikishe miaka 60 tuone utakavyotisha.

    Kale kakatuni Umechemsha na kama ni uhuru basi umepitiliza….sio safi dogo, unakuwa kama hujaenda shule bwana.

    Kuhusu ubunifu wa mavazi, kila la kheri!

  22. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

    Mie sikupi maksi nyingi, maana unawaita wenzako “Beast” hivi ukijaliwa kumpata mtoto wa aina hiyo (beast) utamtupa?
    Mambo yako kwa asilimia zaidi ya hamsini ni mazuri.

  23. TWIN Says:

    Amchore babake mzazi au mkwewe tumuone. Shame on u. Maadili sifuri tupu. Hivi wee Kipanya unaijua SYSTEAM vizuri kweli? we endelea mpaka siku utakayofanywa vibaya ndiyo utajua. Si vizuri kumuita kiumbe wa Mungu Beast, sikutegemea kutoka kwako kabisa. Shame on u.

  24. Lucious Says:

    Big up saaaana mchizi waaaaangu KP..

  25. tonny Says:

    Nilimpongeza mwenzako Finna na wewe lazima nikupongeze.Keep it up Big Boy!Mto ulianza na kiji chemchem.Unayo yafanya sasa utayaona madogo lakini nakuhakikishia inshallah iwapo hutorudi nyuma mafanikio yake utayaona.Ila nikushauri kitu kimoja tu.Hapa nchini bado hatujapata Creative Designer ambaye amefanikiwa kuwasoma watanzania vilivyo na kuibuka na Indegineous Costumes, Mitindo ya Mavazi ya Kiasili yenye Mvuto wa Kisasa.West Africa wenzetu utawatambua kwa mavazi yao.Afrika ya Kusini utawatambua kwa mavazi yao vilevile hususan wanapokuwa ugenini kama majuu.Hapa kwetu bado.Ubishi uliokithiri umetokana na kukosekana kwa Ubunifu.Mitindo ya mavazi kamwe hailazimishwi kwa watu.Acheni watu wavae wapendavyo,wao ndio waamuzi wa mwisho.UBUNIFU UKIKUBALI bila ya kusukumwa na yoyote watu wenyewe kwa hiari yao watajikuta wakifurika kununua mavazi ya mitindo fulani.Nafikiri ujumbe umefika KP. Pili,jitahidi sana kuendeleza FABRICS za hapahapa nyumbani ingawa hilo litategemea zaidi na kukubali kwa soko.Tatu,bila shaka hilo pengine umeshalifanya, jitahidi uwe mwanachama wa klabu za ma designers mashuhuri duniani,uwe na ratiba za maonesho ya mitindo ya mavazi ulimwenguni, uwe na selected sample ya models-mabinti wazuri watakaofaa kwa kazi hiyo na mara kwa mara ujitokeze katika maonesho ya latest designs.Usijisahau na Usibweteke kwa mafanikio hayo finyu.Kazi bado kubwa mbele yako.Nina imani vijana wengi wataiga mfano wako.Usisahau Corporate sponsorship.Keep it going Jack,by giving them people what them people want!Uko creative Bro, no doubt about that,just a bit of polishing!

  26. Matty Says:

    Safi sana Obwatasyo na Dinah kwa kumuelimisha huyo mwana wa mkulima.

    KWAKO MWANA WA MKULIMA,
    HAKUNA ALIYE NA LEBO HAPA INAYOONESHA MTOTO WA FISADI AU LA! MIMI NIMETETEA KUHUSU KUMKOSOA MOLA WETU, HATA KAMA NI UHURU WA HABARI SI KWA DIZAINI HIYO PLS!UUMBAJI WA MUNGU UNAPASWA KUHESHIMIKA NA SI KUDHARAURIKA KAMA UNAVYODHANI WEWE, YEYE SI MJINGA NA NDO MAANA AKAMUUMBA NA SURA ILE UPO?????
    POLE WEWE UNAYEMPAPATIKIA BUSH NA PUTIN WAKE MIE NAWAONA NI WATU KAMA PM WETU TU THOUGH WANATOFAUTIANA SURA NA VYEO VYAO!
    TUNATAKA MTENDAJI BORA, MUADILIFU ASIYE FISADI NA MTETEZI WA MALI YA UMMA KWA MASLAHI YA TAIFA SIYO SURA!

  27. kijiwe Says:

    hivi nyie mnaolalamika wazazi wenu madikteta nini?
    mwacheni kila mtu aseme anachotaka it is freedom of expression and in this particlular case any cartoonist can sketch any pilitician or government leader as long hawamsketch mtu uchi au any other unrespectable manner.
    kwani huyo Pinda kama ni mzuri au mbaya how does that affect Pinda mwenyewe,serikali au wananchi?
    Jamaa anaexplore talent yake so let it be as long as haingilii imani za watu for example kama angemchora Yesu au Mtume Mohammed au sijui Hare Krishna au mganga wako unayemuamini (au whatever faith you have) in any offensive way then hapo mnaweza kumaind.
    Mmezidi kuwafanya viongozi miungu watu ndiyo nyie nyie mkiwekwa chini yao mtashindwa kubisha akisema changia katika ufisadi huu na ule mtakalia kusema bwana mkubwa kasema.
    Jengeni constructive arguments kuhusu huyu KP instead ya kumshusha graph kwani mmesikia hizi graph zenu zitampunguzia kitu?Infact mnampandisha chati indirectly by just discussing about him LOL.
    mnapenda kumaind vitu vidogo sana halafu mnapenda kukosoa watu sana ndiyo maana michanga inawaingia kilaini LOL.

  28. Chris Says:

    Kwanza namkubali jamaa mno… The hunk is objective, think akiendelea hivi atafika mbali sana. Wish him the best in his endearvours.

    Nashangaa mnaosema kuhusu na The Beauty n’ beast cartoon. Kwanza nafikiri u’ve to know the msg behind the cartoon. Yeye alifikisha ujumbe na ninamini wote mnaompinga mmeupata ujumbe na ninafikiri that was his intention. So, amefanikiwa.

    Personally sioni tatizo la ile cartoon,kile ni kikaragosi lazima kifikishe ujumbe ukiwa unacheka….lkn pia ukweli ukiwemo.

    Sasa mliktaka ampake mafuta kwa mgongo wa chupa Premier kwamba ni handsome? Watanzania hatutaendelea kwa kutaka vitu vya kupinda pinda na kutotaka ukweli…msg mlitaka hadi ipinde pinde….

    Hivyo hivyo KP its better to call a spade spade in msgs.. Hakuna ubaya ktk hilo..

    Once again wish u the best…

  29. justin Says:

    Tatizo la huyu mtoto ni kukosa malezi bora ya wazazi.Kipaji anacho lakini PR yake ni ndogo na vilevile naamini shule yake ni ndogo. Huwezi kumchora mtu ambaye kikawaida hajakukosea chochote na kumwita beast. Chora katuni yako na waache watu wa jaji kama ni beast au beauty. Mtoto umekosa adabu na nakutahadharisha kwamba HII INAWEZA KUKU COST KATIKA MAISHA YAKO,au career yako. Mwombe msamaha Waziri Mkuu wetu.

  30. Q Says:

    Poa Mr. KP kaza buti bwana mzee maisha si unayaona yamevaa bukta.

    BIG UP

  31. pamba Says:

    Masoud kazi zako ni nzuri, ila kuna siku uliboa kama ulivyodai we ni mzuri ktk kipindi fulani kny mahojiano na Redio fulani si kweli kaka unajidanganya kwanza mdomo huo balaa na aliyekudanga kufunga nywele kakudanganya nyoa utakua smart kidogo.ok keep it up.

  32. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

    KP mimi nakukubali sana na kazi zako ni za muhimu sana katika kuwaelimisha watu wote Tanzania na hata nje ya nchi. Tunakupa pia hongera kwa kazi yako ya ubunifu wa mavazi.

    Hata hivyo niruhusu niseme yafuatayo:

    Ndg. Kijiwe wewe ndiye dictator wa wazi.
    Hii si mara ya kwanza KP anatoa kazi yake hadharani.

    Siku zote zimesifiwa na wengi kama si wote maana ni kazi nzuri inayofurahisha na kufundisha pia.

    Sasa alipokosea mara moja ameambiwa wazi na hii haina haja ya kuwa mtaalamu wa ukaragosi au uandishi kuona kuwa kakosea. Toka aje na upuuzi wa kumdhalilisha PM kwa kigezo cha sura watu wenye akili zao na taaluma mbalimbali hapa BC, kwa Michuzi, Jiachie, Darhotwire, ktk magazeti mbalimbali n.k wamepinga vikali na kumsahihisha. Hebu wewe kijiwe na KP ingieni mitandaoni muhesabu comments za watu mbalimbali walivyoandika kupinga kazi yake ya siku hiyo.

    Usitegemee tuje na constructive criticisms kama hata baada ya kukueleza kwa lugha nzuri na upole bado wewe mwenyewe au washikaji zako wanakuja hapa kwa kukutetea unconstructively kwa kutoa rejea za anayofanyiwa Bush na Putin na kupindisha maana ya freedom of press isiyo na mipaka wala kiasi!

    KP sikiliza, binadamu si Mungu. Sote tunafanya makosa. Ukigundua makosa yako ni kuomba msamaha na kufanya marekebisho kwa siku zijazo, huna haja ya kung’ang’ana na kujitetea au kutufanya sisi washabiki zako na wengine humu na mitandao yote niliyokutajia na kwingineko kuwa ni wajinga au kuwa tulikurupuka kutafsiri kikaragosi chako visivyo.

    Kwanza unapaswa kujua kuwa hata kama nia ya KP ilikuwa nzuri lakini kwa sababu ya nyenzo au maneno au alama alizotumia, ujumbe haukueleweka au umetafsiriwa vibaya bado, yeye mhabarishaji ana jukumu la kuomba msamaha maana nia yake ni ujumbe kueleweka na sio kutoeleweka kwa kutafsiriwa visivyo!

    Aidha mimi sioni haja ya kumtisha Masoud, eti sijui ATASHUGHULIKIWA na vijana wa Usalama wa Taifa n.k maana idara hiyo haikuanzishwa kwa sababu hiyo!

    Badala yake, Kwa kutotaka kukubali kosa lake na kwa kutotaka kuomba msamaha ATAJISHUGHULISHA YEYE MWENYEWE hapa duniani!

    Mfano mwingine ni huu ambao watu wengi wamekuwa wanaadika na kumchora kwa namna mbalimbali EX-PM kuhusiana na sakata la Richmond hadi kujiuzulu kwake.

    Wengi tumekuwa tunakubaliana na jumbe hizo maana hakika zilitakiwa kutolewa kuonyesha Serikali na hata wananchi wengine makosa au mapungufu makubwa aliyokuwa nayo EX-PM, ambayo hayajawahi kuwekwa hadharani.
    Lakini sasa leo baadhi ya watu wameendeleea mpaka wanajaribu sasa kuwasilisha jumbe zao kwa kutumia photoshop, corel n.k ‘kumtundika’ EX-PM na wenzake eti msalabani na kunukulisha maneno kama aliyotoa Yesu Kristo pale gholgota!

    Binafsi na wengine hatufurahishwi na hilo kwani katika tamathali zote za semi na maandiko hatuoni haja ya kumuhusisha EX-PM na Yesu Kristo maana sasa hata inaweza kupoteza maana ikawa kama yeye EX- PM alionewa tu, kwamba yeye ilibidi atolewe au ajitoe kafara kwa ajili ya dhambi au makosa ya wengine. Au mbaya zaidi ni pale Yesu kristo anaweza kusomeka kuwa naye alisulubiwa kwa sababu makosa yake kama aliyoyafanya LOWASA; inaleta kichefuchefu ndani dini yangu (yetu)!

    Mimi kama Mkristo na mdau wa blogu na vyombo vinevyo vya habari sikubaliani kamwe na matumizi ya MSALABA KUFIKISHA UJUMBE WA KUANGUKA KWA KIONGOZI KAMA LOWASA!

    NAWASHAURI WACHORAJI WATAFUTE PICHA ZA HERODE AGRIPA ALIYEJIKWEZA NA KUJINYANYUA, AKAKAA JUU YA KITI CHA UKUU NA PALE PALE MUNGU AKAMWADHIBU KIFO HADI KUOZA KWA KULIWA NA MINYOO.

    Wasilisheni jumbe zenu kwa mifano iliyohai na inayoshabihiana.

  33. kijiwe Says:

    Chris upo deep sana ,big up!

    JUSTIN naku quote
    “Mtoto umekosa adabu na nakutahadharisha kwamba HII INAWEZA KUKU COST KATIKA MAISHA YAKO,au career yako. Mwombe msamaha Waziri Mkuu wetu”

    wewe umekuwa MUngu jamani?Mbona unaleta hukumu za alfajiri?wakati wote hatuijui siku wala saa.
    Au unatania eeh LOL!sasa mtoto nani hapa wewe au KP?tihi tihi tehe

  34. Vanessa Says:

    HUYU JAMAA (KP) ANANITIAGA NYE… SANA HUYU.
    MIMI NINAONA YUKO SEXY SANA…….
    AMEOA KWANI?

  35. Oliv' Says:

    Haki yanani, ama kweli “you can not get anywhere unless you start” asante kwa kunifumbua macho, usemi huu umenigusa sana, naufanyia kazi na mimi katika nyanja zangu ili na mimi nitoke.
    Asante kwa kunifumbua mawazo, kumbe I have to start now and not someother time

  36. any Says:

    He is handsome, ana midomo mizuri, hawezi kufananishwana Beast, give him a break

  37. Mama wa Kichagga Says:

    Nyakatakule Asante sana. Umewasilisha ujumbe kwa undani na kwa ufasaha pia.

    Kukosea ni ubinadamu na kwamba hakuna asiye kosa! KP achague mwenyewe namna ya kujirekebisha na asonge mbele mambo mengine ni historia sasa.

    Maadamu wadau wawili wa mwanzo walikwishamkosoa kazi yake ya kikaragosi, ilitosha kabisa kufikisha ujumbe na wadau waliofuatia wangejichimbia zaidi katika kuchangia hoja tajwa sio kuendelea kukosoa weee hadi hoja tundikwa ina kosa maana!

    KILA MTU ANA MAZURI YAKE NA MABAYA YAKE! Kwanini tusiwe na mazoea ya kujikita katika kuzungumzia mazuri ya mtu zaidi kwani ndiyo yatakayotujenga kuliko kujikita katika mabaya yake ambayo yanazidi kuturudisha nyuma?

    Hivyo hivyo pia kwa watuhumiwa wengine hasa wa ufisadi! Kuendelea kuwakosoa na kuwatukana hakutatusaidia, badala yake mimi naona tungejichimbia zaidi kujua nini chimbuko la huu ufisadi hapa Tanzania, nani wanahusika? Je, mtandao wao umejengeka katika misingi ipi? Wenzetu hao usifikiri hawafuatilii hapa, wanatusoma uelewa wetu na wanarudi kuimarisha ngome yao ya kuuendeleza ufisadi.

    Nitafurahi sana BC kama siku moja utaweka mada bila picha ya kujadili chimbuko la ufisadi Tanzania, ukuaji wake na mtandao mzima ulivyojengeka ili wadau watoe maoni yao. Kwani bila kujua hili ukomeshaji wa ufisadi utakuwa ni ndoto! Ni kama kulima shamba la SANGARI AU KOLE (aina fulani ya majani yenye mizizi ambapo ukipalilia shamba leo na kuacha kipande cha mzizi kesho yake unakuta shamba limeota majani upya kama vile jana hukulipalilia kabisa).

    Tuuchambue huu ufisadi kwa undani: yaani kikabila, kidini, Ki-eneo (mkoa unaoongoza zaidi), Makampuni/Mataifa (yanayo fanya biashara na hawa mafisadi), sekta, wizara, umri na hata jinsia za wadau wake. Baada ya hapo ndipo sheria kali ziwekwe ili kukomesha hili janga la maangamizi ya vizazi hadi vizazi. Vinginevyo tutakuwa tunampigia mbuzi gitaa kila siku.

    Kwa mtizamo wangu kung’ang’ania kuwafikisha WATUHUMIWA 5 mahakamani kwa kosa la ufisadi na kuuacha mtandao mzima ukiendelea na ufisadi ni kukurupuka na kwamba tutayakosa mambo mengi sana. Hawa jamaa wangefilisiwa kwanza halafu watumike kama chambo cha kutoa taarifa zote muhimu kuhusiana na ufisadi.

    TUKOMAE KIAKILI ZAIDI KULIKO KIHISIA!

  38. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

    Unayejiita Vanessa,
    acha matusi kwenye hii blog. Kama huwezi kujiheshimu basi sio lazima uchangie.
    (Asilimia mia wewe sio mwanamke bali ni mwanamme.) Umetumia hili jina la kike ili kufikisha ujumbe wako wa kijinga.

  39. amina Says:

    nyakatule nakuunga mkono…..hao wanaomtetea wataelewa sasa

  40. mmy Says:

    All in all, me i have nothing to say .

    But may be wadau wamesikia vibaya kama binadamu thats why they complain. Basi kaka jirekebishe tu mambo yaishe si ndio jamani!! tumalize basi tusilumbane sana coz ujumbe ameupata

    ok all the best 4 him

  41. kijiwe Says:

    Tafadhali Ndg. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO naomba usome comment yangu ya mwisho then utaelewa motive yangu.

  42. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

    Kijiwe comments za mwisho ziko wazi kabisa. Nadhani nilishtuka tu na kiingilio cha comments zako za mwanzo. samahani sana.

    Dinah, Metty, Upendo Furaha Amani, Amina na wengine wote, nami nawapa shavu kwa michango yenu. Nadhani hili limeeleweka kama alivyosema MMY.
    Mama wa kichaga hoja uloshuka nayo naiunga mkono. BC ni kweli kama inawezekana tuanzishieni mjadala ili yumkini tutoe mapendekezo ya si tu nini kifanyike kwa Mafisadi wa sasa bali zaidi kuchunguza vyanzo vya ufisadi na namna ya kukata mizizi ya hiyo miti ya ufisadi hata kwa vizazi vijavyo nchini kwetu TZ.

  43. any Says:

    Sasa mlitaka awadanganye aseme uongo kuwa P is more handsome than Kikwete! ila cha muhimu afanye kazi kwani Pinda hakushinda Miss TanzaniA! so tumvumilie tufumbe macho tusubiri utendaji, msiangalie sura, jali kazi!

  44. nice kz Says:

    Keep it up kp i really admire you, your very creative and you involve your self for many things just for better life.

    I wish the youth to follow your plan they don’t have time to use for drugs (madawa ya kulevia), cause they will be busy.

    To have your on lebo is not a jokes you must be very aggressive.

    i will visit your shop at millenium tower very soon.

  45. TWIN Says:

    Tatizo ni kukosa shule na upeo finyu wa mawazo basi! Hana adabu.

  46. kijiwe Says:

    NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO
    its ok tupo pamoja

  47. any Says:

    KP keep on doing ur thing, huwezi kuridhisha population nzima, kila mtu na mtazamo wake, kama mnamwona Pinda mzuri basi ni macho yenu, ila yeye kamuona vile alivomwona, and above all it was just a joke to make our day! lakini watu wameichukulia serious kuliko issue ya Richomonduli. Go babe KP we are behind u, ila we wont touch it, so dont worry. heheheheheh.

  48. Jennas Says:

    Hiyo katuni iko wapi na mimi niione jamani siwezi kuchangia kitu bila yakuiona
    Msaasa kwenye tuta jamani!
    Dinnah mdogo wangu embu nitumie ama mtu yoyote anielekeze ilipo

  49. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

    Jennas safu kwenye blog ya Michuzi utaona hiyo katuni.

  50. mwalimuzawadi Says:

    Mimi Masoud namfahamu angalao kidogo, sio sana. Nadhani kuna watu wamesema kuwa upeo au elimu nayo inachangaia sana katika utendaji wa kazi ya sanaa. Ni kweli. Anatumia zaidi utoto wa mjini bila kujua kuwa kuna wengine wako makini katika kuchambua kazi zake bila kujua CV yake.

    Kwa mujibu wa kitabu changu cha tafsiri ‘beauty’ ni uzuri, urembo au haiba na ‘beast’ ni mnyama pori au hayawani. Pia ‘beastliness’ ni uchafu, upujufu, ukatili au unyama.

    Kama alilinganisha viongozi wa taifa hili kwa maana hizi kweli alipotoka. Ila kama alitumia maana ya juu juu kuwa filamu/kikundi cha BoyzIIMen kilivurunda, na anategemea filamu ya the Beauty and the Beast italipa, sidhani kama ulinganishi wake umefaa. Nadhani hii imeumiza sana watu kutokana na ukweli kuwa ‘ubeast’ si kitu kizuri na waziri mkuu wetu hatuwezi kumwita ‘beast’ wakati hata ofisini hajakaa hata EL na uharamia wake hakuitwa ‘beast’

    Mdau Jennas, hako kakikaragosi kalitundikwa kwenye blog za Michuzi, Chemi, Mjengwa na hata kwenye gazeti la Mwananchi karibu wiki sasa imepita

  51. Jacob N Says:

    Vijana wabunifu nawapa hongera sana na nikija Africa tena ningependa kukutana nanyi ili niweze kuongea nanyi.

    Tafadhali soma link hii http://jacobkashimba.blogspot.com/

    Asanteni

  52. saada Says:

    Big up men , kp hakuna tena. ila umeniboa sana kumuita pm wetu beast. angalia utapoteza umaarufu.

  53. GMOPAO Says:

    BIG UP MZEE UKO JUU SANA HONGERA SANA NI WACHACHE SANA AMBAO WANAKUA NA JITIHADA KALI ZA KIMAISHA KAMA WEWE MKUU..HONGERA USIKATE TAMAA UTAPATA KESHO..

  54. Elizabeth Says:

    Mi nawashangaa hao walioamua kulalamika khs cartoon ya PM, kwani hapa hoja ilikuwa khs cartoon au his designing carrier (mavazi). Hayo ya beast yanakujaje? Au Hamkuchangia siku cartoon ilipotoka….

  55. mimi Says:

    Yeye mwenyewe mbayaaaaa, pua kaa kaptula ya mdoli, domo utafikiri kolezeo la moto, eti beast!!! Kumbe elimu ni muhimu eee!!! Nilikuwa namuona wa mana kumbe hana tofauti na yule zero!! mtu na akili zako timamu huwezi kusema namna ile na unajua kabisa haya magazeti yanasomwa na watu wengi!! ebu nipishe niende zangu mie kwenye shughuli zangu!!!

  56. Diana Says:

    Nampongeza sana Masoud kwa vipaji vyake! kuchora ambacho huwa kinanichekesha sana, lazma niangalie ni jambo gani la jamii lililochorwa siku hiyo….
    Pili…..Nguo….nimenunua jeanz pale dukani, i must admit….i am more than satisfied with the quality….the cuts are good too……ilikuwa low wait…….t really hangs on the low-low, withought showin the butt crack, which is very good!!
    Top sikukuta sana, naisi zimeisha, tunaomba utukumbuke wenye maumbo 8, vitop vifupi vinapanda juu, so longer tops zahitajika…(haimaanishi ziwe pana kama t-shirt)
    all in all…..big up!!!!……

  57. Lui Says:

    jamani kweli nyani haoni kundule yaani KP yeye ameshajiangalia vizuri?? maana km siyo kukaa mjini angekuwa kituko zaidi, kuwa makini KP

  58. Jane Says:

    AISEE NYIE WOTE MLIOANDIKA KUWA KP SIJUI HANA ADABU, SIJUI MBAYA, MAMBO MEEENGI NAHISI NA NYIE SURA ZENU ZIMEPINDA NDO MANA MNA HASIRA, MANA KWENYE KATUNI HAKUSEMA MP NI MBAYA, UJUE AKILI ZENU ZIMEDUMAA, MNA MAWAZO FLANI YA KIZUSHI..SURA ZENU MBAYA NDO MANA MNAJISHUKU NA MNAHASIRA!!!! HA HA HA HA AH AHA HA AHAAAAAAAAAAAAA

  59. Chakoma Says:

    KUSEMA KWELI HUWA NAJIULIZA KILA SIKU HUYU JAMAA ANATUNGA AU ANATUNGIWA KWA KUWA KILA NINAPOSOMA MAMBO YAKE LAZIMA NICHEKE TENA CHEKO LA LEO LITASHINDA LA JANA BIG UP KP NAKUAHIDI NIKIRUDI HOME LAZIMA NIJE KUONA NA UBUNIFU WAKO

  60. Aina Says:

    Naweza nisiwe mtu muhimu kwako lakini kama Mtanzania mwenye heshima na upendo. Najisikia vizuri kukuambia kuwa Katuni yako ya The Beauty and the Beast imenikwaza sana na kweli nimetokea kuchukia katuni zako. Kwa kifupi kwangu umaarufu wako umepotea. Najua sitakupunguzia chochote ila lazima nikwambie. Angalia kwa makini kazi zako.

  61. Jennas Says:

    Asanteni mwalimuzawadi na Upendo furaha na amani kwakunifumbua majicho yangu.

    Mpaka hapo sichangii lolote nimeshaiona 5%
    Mbarikiwe sana.

  62. RHYEEM Says:

    kabla ya kulaumu ama kutoa maamuzi juu ya jambo fulni ni lazima sisi tukiwa kama binadamu tuliopewa uwezo wa kufikiri,tujiulize kwa nini,kwa sababu gani tunchukua maamuzi ya kufanya mambo fulani.ni vibaya sana kukurupuka kutenda ama kutoa maamuzi.sasa basi kwa suala hili la huyu jamaa lazimatumpe nafasi ya kutueleza kuwa kwa nini yeye anaiona sura ya pm wetu katika huo mtazamo.yawezekana macho,fikra,ama mazingira ya uelewa wake viko hivyo.kwa hiyo kumsema tu kwamba anafanya vibaya kumwelelezea pm hivyo ni kuingilia mtazamo wake ambao hatujui kuwa unasababishwa na nini.kwa hiyo bwana masoud tunaomba uueleze umma kwa nini mtazamo wako ulieleza hivyo.binadamu tulimbwa kila mmoja na mtazamo na fikra zake ambazo zaweza kusababishwa nakitu kimoja ama kingine.KUKOSOANA NI KUFUNDISHANA.

  63. Sura Says:

    Ndugu zangu, Nilichogundua kwa KP ni “kasumba” jamaa yetu huyu Mtanzania mwenzetu, akiona ngozi nyeupe basi anaona kila kitu kwake sawa. Kumuona mwezie anasura ya kupewa jina Beast ni kwa ajili ya rangi yake tu! angepewa rangi nyeupe kama ya mkewe haya yote yasingetokea. ” Tujifunze kuwaambie watu wasirubuniwe na sura, waomba hekima ya kuona ndani ya mioyo ya watu.

  64. mroki Says:

    kp nakubali mambo yako babake yaaniubunifu wako sio mchezo ukweli ndio huo kama kuna anaye pinga huo utakuwa wivu kaza buti babake mm nakuombea MUNGU uwafunike paka wakina timberland (J.M) nihayo tu mtu wetu lol
    from washika dau opensanit enterprises god bless u man

  65. Tutahany Says:

    Hi bro KP! Bro yo creative, I really appreciate yo work. keep it up bro and b blessed.

  66. Adam Magege Says:

    Big up KP kwa kwa kujali watu wa hali ya chini kwani baadhi ya watu wa status yako wangekuwa wanawajali Macelebrity tu. kwako issue ni tofauti BIG UP Mtuwangu.
    Nakuombea na we mwenyewe endelea kujiombea coz ninaimani umepata mafanikio haya kutokana na kumuomba keep it up, ili akujalie uweze kuitanua biashara yako mpaka huko Nje unako kusudia kuifikisha. GOD BLESS YOU ma Brother.

    Adams.
    MPANGO WA DAMU SALAMA TANZANIA.

  67. lufingo Kosssam Says:

    Kipanya ni miongoni mwa wanazuoni wachache mnaoijua Dunia.Keep it up.Sikuwahi kuishi karibu na baba na mama yangu lakini ninaposikiliza kipindi chenu cha asubuhi nahisi niko na familia yangu.

  68. bcdef Says:

    mwacheni KP, sababu hata huyo MP hajali huo upuuzi. Nyie ndio mnajua kuchonga. Ebu ongeeni mambo ya maana.

  69. Mama wa Kichagga Says:

    KP,

    Asante sana nilikutembelea pale mahala na watoto wametoka MCHICHA ILE MBAYA. Ongeza size za 4×4 kaka maana hapa haachwi mtu nyuma labda awe mzembe mwenyewe!

    Nice quality and designs!

    NB: Wewe mind kazi zako anayelonga mwache aendelee maana wakati mwingine watu husumbuliwa na wivu na ufinyu wa fikra.

    HAKUNA MTU ALIYEUMBWA KUWA HAKIMU WA MWENZIE HAPA DUNIANI!

  70. kaundime Says:

    jamani we mutoto ya mama mwenzangu umugumu kwa kweli mugumu sana Mungu akuzidishie ukomae hivohivo Umepewa bwana na kama usingalizaliwa bimkubwa saa hizi mgonjwa sana sasa siunaona aaaaaaaaaaa

  71. KIDISA,Kidifresh Says:

    Kaka umepiga hatua kubwa sana.Wewe ni mjasiamali kamili,kaza buti.
    Kidifresh.

  72. eugenia Says:

    ki ukweli hapo alikosea na mnajua kwamba kosa mara ya kwanza si kosa ila kurudia ndio kosa atakuwa amewasikia na i hope atajirekebisha. pia congratulation sana its good to hear that u r a designer nakupa sapoti sasa watanzania tuwe pamoja na tuwasaport watu kama hawa unajua watanzania wana kosa moja tu wanapenda kuwavunja wenzao moyo alaf hawajui kwamba no body is perfect lazima binadamu akosee na pia sasa hakuna suala la nani mzuri na nani mbaya we all know wote tumeumbwa kwa udongo na tunafukiwa na huo huo udongo ubaya wa mtu na uzuri haujalishi as long as wote tuko njia mmoja.

  73. gaty Says:

    go go go go go go go go go kp!!!!!!!!!!u really work hard, success is all what you deserve!!!!!!!!

  74. cent74 Says:

    na wa salimu tena

  75. zaina seif Says:

    kp kazi nzuri sana, kaza buti kaka yangu safari bado ni ndefe! usiace mtu yoyote akuangushe ushauri 2takupa ila nikazi kwako kuucekeca ,au sio? big up bro

  76. maryciana Says:

    hii comment naweza kubaniwa,ila hamna lolote na huyu KP

  77. lufingo Kosssam Says:

    Masoud Kipanya let the sky be your limit!keep it up

  78. mkuu big up sana!!!!
    mi nakukubali hasw ktika disign,nakumbuka toka kp iko kwenye karatasi as scatch,hadi imekuwa kitu chenyewe duuh!!!

  79. bella Says:

    hellow kp
    hongera sana n keep it up guy
    nice talent n nakupa big up sana kazi nzuri kp

  80. Tamu Says:

    asingechora katuni msingepata ya kusema.

    sio siri katuni zake zinabamba hata kama umenuna ukisoma lazima utabasamu.

    kuhusu mavazi ya lebo ya kp usipime jeans zina quality nzuri kwa kweli.

    amechorwa bush kavaa kimini na sidiria sembusse nanilii teh teh teh

  81. Mary Mkwaya Malamo Says:

    duh! ebwana wewe ni noma.
    yeah man!.


Leave a reply to Angelina Cancel reply