BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

ALLY REHMTULLAH’S LONDON FASHION WEEK LAUNCH September, 23, 2008

Filed under: Fashion Designer,Photography/Picha,Sanaa/Maonyesho,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 9:57 PM

It is every designers dream to be part of the London Fashion Week, and this year Ally Rehmtullah, a 22 year old Tanzanian designer was given this honour. On the 19th of September Ally Rehmtullah launched his new African Couture at the Museum of London during the London Fashion Week. Ally was also part of fashion diversity whereby as an established designer he was an inspiration to the young and upcoming designers in London. Ally Rehmtullah’s couture was modelled by MAHOGANY MODELS from London.Here are some images.

(more…)

 

DINA NA ASIA NDANI YA KIMASOMASO June, 25, 2008

Filed under: Fashion,Fashion Designer,Watangazaji — bongocelebrity @ 11:54 AM

Mbunifu wa mavazi Mama Asia Idarous (kulia)akiwa amepozi na mtangazi wa Clouds Fm,Dina Marious,wakati wa fashion show iliyokwenda kwa jina Kimasomaso hivi karibuni jijini Dar-es-salaam.Vazi alilolivaa Dina ni mojawapo ya ubunifu wa Asia Idarous.Mavazi mengi yatumikayo kwenye harusi yalionyeshwa katika show hiyo.

Photo/Ahmad Michuzi

 

“SIJAACHA KAZI CLOUDS FM ILA…”-MASOUD KIPANYA June, 18, 2008

Filed under: Developing News,Fashion Designer,Special Interest News,Watangazaji — bongocelebrity @ 6:36 PM

Hakuna ubishi kwamba kipindi cha PowerBreakfast kinachorushwa na radio ya Clouds FM ni mojawapo ya vipindi vya radio vyenye wapenzi na wasikilizaji wengi nchini Tanzania.

Hivyo basi haishangazi kwamba hivi karibuni watangazaji wawili wa kipindi hicho waliokuwa wamezoeleka,Masoud Kipanya(KP) na Fina Mango, walipopotea hewani maswali mengi yaliibuka.Wako wapi KP na Fina?Maoni na e-mails zikarushwa kwetu tukiombwa kuwatafuta na kujua nini kimetokea na kama wapo likizo tu au inakuwaje?

Wakati tukifanya juhudi za kujua nini kimetokea,blog maarufu ya Michuzi ikaandika habari iliyokuwa na kichwa cha habari Fina Mango na Masudi Kipanya niaje?Mjadala ukazuka.Kwa bahati nzuri,nasi tukawa tumebahatika kumpata mhusika mmojawapo yaani Masoud Kipanya(KP) ambaye hakusita kutupa yake machache kuhusu nini kimetokea au kilitokea,yuko wapi,anafanya nini nk.Anasisitiza kwamba nia yake ni kutoa ufafanuzi(kwa upande wake) ili watu wasiendelee kujenga picha ambazo pengine hazitakiwi kujengwa wala hazipo.

Je PowerBreakfast ya Masoud na Fina ndio imefikia kikomo? Je ni kweli kwamba masuala ya mshahara ndio yamesababisha wapotee hewani?Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi;

BC: KP,kwa muda wa wiki kadhaa sasa kumekuwepo na tetesi,minong’ono,udaku nk kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwenu katika kipindi chenu maarufu cha PowerBreakfast kupitia CloudsFM.Hivi leo,blog ya Michuzi(bila shaka umesoma kilichoandikwa) iliweka kidogo kuhusiana na kilichokuwa kinazungumzwa mitaani. Je ukweli uko wapi? Upo au haupo tena katika PowerBreakfast?Nini kimetokea? (more…)

 

ZEZE NA MWANAMBOKA June, 10, 2008

Filed under: Blogs,Fashion Designer,Urembo,Wanawake na Watoto — bongocelebrity @ 1:52 PM

Mbunifu wa Mitindo maarufu,Khadija Mwanamboka, akiwa pamoja na Shamim Zeze,mmiliki na mwendeshaji wa blog ya 8020 Fashions,hivi karibuni jijini Dar. Khadija Mwanamboka ni miongoni mwa waanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Tanzania Mitindo House ambalo linajaribu kusaidia watoto yatima na wasiojiweza nchini Tanzania. Mwaka jana tuliwahi kuongea kidogo na Mwanamboka kuhusiana na TMH.

 

REHMTULLAH DURING TEMPTATIONS SHOW May, 29, 2008

Filed under: Fashion Designer,Sanaa/Maonyesho,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 3:58 PM

Mbunifu wa mitindo ya nguo anayekuja juu kwa kasi nchini Tanzania,Ally Rehmtullah,akipita jukwaani kuwasalimia na kuwashukuru watu mbalimbali waliohudhuria show yake iliyofanyikia katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski jijini Dar-es-salaam wiki iliyopita.Rehmtullah aliita show yake Temptations.Kwa habari zake zaidi unaweza kutembelea tovuti yake kwa kubonyeza hapa.

 

PRIDE OF TANZANIA March, 19, 2008

Filed under: Fashion,Fashion Designer,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:03 AM

 

Kama kuna mafanikio yoyote katika masuala ya urembo ambayo Tanzania inaweza kujivunia,basi vielelezo vya mafanikio hayo ni mabinti wawili wanaoonekana pichani.Kushoto ni Nancy Abraham Sumari ambaye mwaka 2005 aliibuka kuwa Miss World Africa na Flaviana Matata,Miss Universe Tanzania 2007 ambaye pia aliipeperusha vyema bendera ya Tanzania huko nchini Mexico katika mashindano hayo ya dunia na kushika nafasi ya sita huku akiacha gumzo duniani kote kwa kuwa mshiriki wa kwanza wa mashindano hayo ambaye aliingia na “kipara”.

Usiku wa leo,Flaviana Matata, anatarajiwa kuonyesha mitindo ya mavazi ya mbunifu wa mitindo,Angelo Elly Mlaki katika Ukumbi wa Kituo Cha Utamaduni Cha Ufaransa(Alliance Francaise Cultural Center) kilichopo jijini Dar-es-salaam.Maonyesho hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Compass Communications ambao ndio waratibu wa Miss Universe nchini Tanzania.

 

READY FOR FESTIVE COLLECTIONS March, 4, 2008

Filed under: Fashion,Fashion Designer,Sanaa/Maonyesho,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 1:24 PM

 

Pichani models(ukipenda waite modoz) ambao watashiriki katika onyesho la mavazi la mwanamitindo Fatma Amour ambalo limepewa jina la Festive Collections. Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 8 March,2008 ndani ya Movenpick Hotel na kiingilio kimepangwa kuwa Tshs 20,000 kwa kichwa.Burudani itakuwepo na itatolewa na wasanii Matonya,Unique Sisters,Ne-Shabaan Kassim aka Ne-Mo pamoja na wengineo.Picha hii imepigwa leo mchana maeneo ya Mikocheni jijini Dar-es-salaam.

 

“USIOGOPE KUCHELEWA,MUHIMU NI KUANZA”-KP February, 14, 2008

Filed under: African Pride,Fashion,Fashion Designer,Mfanyabiashara,Ujasiriamali — bongocelebrity @ 12:10 AM

Kwa wengine bado anaendelea kuwa mchora katuni aliye maarufu zaidi nchini Tanzania.Kwa wengine ni mtangazaji maarufu wa redioni ambaye kila asubuhi huwapa wasikilizaji habari mbalimbali na pia burudani. Lakini kwa wengine,yeye ni mbunifu wa mitindo(fashion designer) ambaye anakuja juu kwa kasi ya aina yake.Huyu si mwingine bali Ali Masoud,(pichani) maarufu kama Masoud Kipanya au ukipenda KP.

Leo hii yawezekana kabisa kusema kwamba Masoud ni kijana mjasiriamali ambaye anajaribu kutizama mbali kushinda maelezo. Ni kijana anayependa kujishughulisha kwa bidii na maarifa bila kuchoka wala kukata tamaa.Mwaka jana alitimiza mojawapo ya ndoto zake za muda mrefu kwa kuzindua lebo/nembo ya KP iliyokwenda sambamba na KP Wear.Hivi leo sio ajabu kukutana na watu mitaani waliovalia nguo zenye nembo na ubunifu kutoka kwa KP!

Kwa mara ya pili,hivi karibuni BC ilifanikiwa kupata fursa ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na sio uchoraji katuni wala utangazaji bali ubunifu wa mitindo. Nini kilimsukuma kuingia kwenye fani ya ubunifu wa mitindo?Unataka kuijua falsafa inayomuongoza katika fani hii?Je anahofia kitu gani zaidi linapokuja suala zima la ubunifu wa mitindo?Nini mipango yake ya sasa na baadaye kidogo?Kwa hayo na mengineyo mengi zikiwemo picha za baadhi tu ya viwalo vilivyosheheni ubunifu wake,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)

 

KUTOKA FABAK FASHION February, 9, 2008

Filed under: Fashion,Fashion Designer,Watu na Matukio,Weekend Special — bongocelebrity @ 9:10 AM
Pichani ni baadhi ya models wakionyesha vivazi jana usiku ndani ya Moevenpick Hotel (zamani Royal Palm Hotel) jijini Dar-es-salaam.Fashion show hiyo iliyokwenda kwa jina Lady in Red iliandaliwa na Asia Idarous wa Fabak Fashion.Ilifana.
Baadhi ya warembo maarufu nchini nao walihudhuria kama wanavyoonekana pichani.Pia kama unavyoweza kuona, shorter hair seems to be a new style/fashion in town!Wamependeza lakini,au?
Models waliokuwa kazini jana.Shorter hair rocks again!
 

KP DESIGNS January, 30, 2008

Filed under: Fashion Designer,Ujasiriamali — bongocelebrity @ 11:52 AM

 

Baadhi ya mitindo kutoka kwa Masoud Kipanya au KP.Kwa habari zaidi unaweza kutembelea www.kpwear.com.