BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MAUNDA ZORRO February, 10, 2009

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 11:06 PM

maundabc

Anaitwa Maunda Zorro.Anatokea kwenye ile ile familia ya kina Zorro ambayo tunaweza kabisa kuiita “Music Family”.Tangu alipoingia rasmi kwenye fani ameshaachia nyimbo kadhaa ambazo sio tu zimeshika chati bali zimethibitisha kipaji alichonacho.Pamoja na uthibitisho wa kipaji,lipo swali ambalo bado sijalipatia majibu pamoja na kujaribu kulifanyia utafiti mara kadhaa;Hivi uimbaji(naongelea uimbaji mahiri ambao wengi tunaweza kukubaliana kwamba hapo sawa) ni kipaji mtu anazaliwa nacho au ni kitu ambacho yeyote anaweza kujifunza?Na mazingira anayokulia mtu yana mchango wa kiasi gani katika kipaji?

Miongoni mwa nyimbo hizo ni huu hapa unaokwenda kwa jina Nataka Niwe Wako


Photo/A.Mrisho.

Advertisements
 

17 Responses to “MAUNDA ZORRO”

 1. BLACKMANNEN Says:

  Aliyenacho, atabaki nacho tu, na ukipanda mahindi ni lazima uvune mahindi, vivyo hivyo, ukipanda bangi ni lazima uvune bangi. Familia ya Zorro ni ya wanamiziki, hakuna ubishi.

  “Maunda”, kwa kawaida huanza maoni yangu kwa wanamuziki wa kike kwa kuwasifia wajihi wao jinsi Mwenyezi Mungu alivyowajalia uzuri katika maumbo.

  Vivyo hivyo Dada Maumba, naanza kwa kusema……. Umeumbwa na umeumbika!!!. Sijui nianzie wapi kukusifia umbo lako…au sura yako kwa ujumla. Maana nikianzia kifuani na macho yako……. Nashindwa kuendelea kuandika. Maana nabaki nikikutazama tu.

  Lakini, ngoja kwanza niusikilize mziki wako bila ya kukutazama wewe, ili nitakapotoa maoni yangu kuhusu mziki wako, yawe ni maoni yahusuyo mziki tu, nisipate upofu wa kuuchambua mziki na uelewa wa kitu, kutokana na mvuto mkubwa wa sura yako. I’ll Be Back……!!!!!!

  It’s Great To Be Black=Blackmannen

 2. Mattylda Says:

  Maunda mrembo wimbo wako mzuri sana, sauti nyororo, wewe mwenyewe mashaallahhuu!!!!!!!safi sana kaza butiiiiiiiii!

  mimi naona uimbaji mahiri unatokana na kipaji mtu anazaliwa nacho,ila sasa ambacho sinaga jibu ni hivi,utakuta mimi nasema jamani natamani kuimba lakini sina sauti heee nashangaa naaambiwa sauti unayo ila inahitaji mazoezi mhh hapo sasa ndo pana utata kidogo maana kama ni zoezi ndo nitaweza kuimba kwa ufasaha basi hakuna haja ya kuwa na kipaji hapo!

  Mazingira anayokulia mtu pia yanaweza mfanya akapenda kitu mf.hii familia ya kina Zoro kwa kuimba imejaaliwa hata home unaweza kuta watoto wanaimba imba tu kwa kufatisha nyimbo za dingi na hapo sasa si ndo wanapata experience kabisa ya uimbaji!

 3. Jay Says:

  Si mchezo mtoto Maunda yuko sexy kinoma.

  Ray C akae chonjo… siku zake zinahesabika.

  By the way wadau wa Lalola mmejifunza nini kwenye tamthilia hii?

  Kaka Michuzi anauliza swali.

  BOFYA HAPA kutoa maoni

  Jay

 4. papuu Says:

  wewe jay namba 5 acha masikhara..huwezi hata siku moja kumfananisha na ray c. huyu maunda sauti haina kitu kipya,tushazisikia type hii.

 5. Edwin Ndaki Says:

  Inawezekana kuzaliwa familia ya vipaji NA USIWE na kipaji.

  kuishi karibu na mahakama mfano kisutu..hakufanyi uwe mwanasheria…

  Tutafika tu..hongera maunda unakipaji jiendeleze utafika mbali zaidi.

  kuwa makini tu na wakware usije changanya muziki na wizi..

 6. mdau UK Says:

  dah mtoto mkali sana, sio masihara yuko so sexy na hata nyimbo zake ni bomba, naomba kuuliza bwana BC vp ana mchumba au kaolewa..??

 7. @BLACKMANNEN: Blackmannen umenichekesha sana Mkuu!Umesahau zile kauli za nikioga nakuona kwenye beseni nini?:-) Labda kama ushamcheki ukimsikiliza tu sauti bado unaweza kukumbuka muonekano wake. AU?

 8. Sue Says:

  to me she is the next diva ana uwezo kuliko anavojijua love ya gal keep it up the spirit

 9. michelle Says:

  Mtoto wa snake is snake!!!!!!!!! haya dada Maunda hongera.

 10. dan Says:

  Kawaida sana! Hakuna jipya! Tumeshazisikia za type hiyo! Perhaps ndio uwezo wa wanamziki wetu na maproducer wetu! Katika chart za bongo wimbo huvuma kwa wk 2 kisha hutoweka na ukishaenda hautakumbukwa tena! Something unique lasts longer!!!!!!! album zinapakulwa kila siku! too flowery , papara nyingi matokeo yake hkuna umakini!
  Kizazi kipya kazi bado mnayo!

 11. salma Says:

  The girl is beautiful tena ukimuona live ni mzuri zaidi kuliko hata kwenye shooting nakwambieni..mimi niliona kipindi kinaitwa FRIDAYNITE LIVE AT CH5 EATV wakati msanii nuru alico-host the show na musa na maunda alikuwa mmoja wa wasanii wenzake na maunda aliulizwa kaolewa au,,,akajibu hajaolewa ila ana boyfriend….kazi nzuri

 12. Nautiakasi Says:

  Mhhh yangu macho tu…! Sasa ndo ni nini hii? Jamani kuimba sio “genetic trait” kama ulivyo uzeru zeru, kwamba kama babayo ajuwa kuimba basi na wewe uzaliwe na genes yakuimba…maaaaawe! Sijui anaimba sauti ya 1 au 2 naona zogo tu, haifai kuitwa nyimbo labda tuseme ni ngonjera..obs!pia haikidhi kuwa ngonjera, sababu ngonjera huwa na vina na mafunzo maalum. Hizi ni kelele tu, hazina tofauti na kelele za nzi waloona mzoga!

  1. Mashairi hayana ujumbe wowote!
  2. Sauti inakwaruza kama kanywa conc.sulphuric acid
  3. Haendi na beat kabisa, yeye yuko kwenye low notes beat ziko high notes
  4. Mashairi atunge kaka yake halafu aimbe yeye!!!!
  5.Hana haiba ya uwana muziki, i.e havuti hisia za wadau ambao wengi ni vijana,Kwa hiyo show zake hazilipi
  6. Hana wivu wakujifunza ndo maana haendi shule kujifunza muziki

  Ushauri: Angetafuta kazi nyengine ya kumuingizia kipato kama vile kuuza mkaa au kujiunga na jeshi la mgambo kuondoa hao machinga wanaochafua jiji. Sababu hafiti kwenye muziki.

 13. Aunt D Says:

  Tatizo ni mapoudaaaaa……………………

 14. John Says:

  Huo wivu au chuck binafsi! eti sauti inakwaruza, low note! Unaujua mziki wewe au ni ushamba wako! Kiazi kweli mijitu mongine inajisemeaga tu!

 15. jordan Says:

  she needs another job that voice is not cutting it for me.

 16. Lina Says:

  Hongera Maunda unajitahidi sana na Kipaji unacho. Waache waseme mwishowe watachoka wewe unasonga mbele. Nyimbo zako zinasisimua bwana si mchezo hata kama ametunga Banana hiyo sio sababu. Kaza buti kama ni makosa madogomadogo yanarekebishika. Kwa mimi sijaona tatizo liko wapi. Naweza kusema hizo ni chuki binafsi.

  All the best Dada Maunda.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s