BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SALAMU ZA FA KUTOKA COVENTRY February, 16, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Elimu na Maendeleo,Muziki — bongocelebrity @ 2:33 PM

fabc1

Hakuna ubishi kwamba kijana Hamis Mwinjuma au maarufu kama MwanaFalsafa(MwanaFA) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao wamefanikiwa.MwanaFA amefanikiwa sio tu kufikisha ujumbe alioukusudia kwa jamii bali pia kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yake kupitia muziki.Miziki yake imekuwa ikiimbwa na watu wa rika mbalimbali.Hayo nayo ni mafanikio.

Pamoja na mafanikio ya kimuziki au kisanii aliyonayo MwanaFA,anabakia kuwa mfano wa kuigwa linapokuja suala zima la elimu,muziki na maisha.Hivi karibuni alithibitisha hilo pale alipoamua kurejea tena shule.Safari hii ameelekea nchini Uingereza.

Nini kinamsukuma kijana huyu katika nyanja ya elimu? Na je hivi karibuni alipoachia wimbo unaokwenda kwa jina “Msiache Kuongea” alikuwa anamjibu Inspekta Haruni?Anazungumziaje maisha ya nchini Uingereza?Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi na MwanaFA

BC: Pamoja na mafanikio mazuri katika muziki kule Bongo bado umeamua kurudi tena shule.Nini kinakusukuma?Hapo UK umeenda kusomea nini na katika chuo gani?

FA: Kuna mengi yanafanya nifanye nnachofanya.Lakini kubwa na la msingi zaidi ni kuwa na nguzo nyingine kwa ajili ya maisha ninayoishi(Plan B).Kama unavyojua muziki pamoja na kuwa unakwenda vizuri lakini hautabiriki sana.Ni ngumu kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kwa angalau miaka 10 ijayo.

Na zaidi ni kuwa naona kama kuna muda mwingi kama msanii wa kibongo nakuwa naupoteza kwa kutofanya chochote baada ya kurekodi(ambayo sio kila siku),kufanya shows(mara nyingi huwa weekends),matangazo(mara chache kama una bahati) na interviews ambazo nazo sio kila siku.Kwa hiyo kwenye wiki kunakuwa na muda mwingi unaenda bure ambao nimeona ni vyema nikautumia kufanya kitu kitakachozalisha.
Hapa UK nasoma Msc Finance na nipo Coventry University.

BC: Una mpango gani na muziki kwa hivi sasa?Kama utaendeleza muziki na shule vilevile,lini labda wapenzi watarajie albamu yako mpya? (more…)

Advertisements
 

MAUNDA ZORRO February, 10, 2009

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 11:06 PM

maundabc

Anaitwa Maunda Zorro.Anatokea kwenye ile ile familia ya kina Zorro ambayo tunaweza kabisa kuiita “Music Family”.Tangu alipoingia rasmi kwenye fani ameshaachia nyimbo kadhaa ambazo sio tu zimeshika chati bali zimethibitisha kipaji alichonacho.Pamoja na uthibitisho wa kipaji,lipo swali ambalo bado sijalipatia majibu pamoja na kujaribu kulifanyia utafiti mara kadhaa;Hivi uimbaji(naongelea uimbaji mahiri ambao wengi tunaweza kukubaliana kwamba hapo sawa) ni kipaji mtu anazaliwa nacho au ni kitu ambacho yeyote anaweza kujifunza?Na mazingira anayokulia mtu yana mchango wa kiasi gani katika kipaji?

Miongoni mwa nyimbo hizo ni huu hapa unaokwenda kwa jina Nataka Niwe Wako


Photo/A.Mrisho.

 

CONGRATULATIONS NAKAAYA!! January, 29, 2009

Filed under: Burudani,Muziki,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 8:28 PM

nakaayabc112

Nilipomuuliza kwamba nini mipango yake ya baadaye kisanii au katika sanaa bila kusita Nakaaya alinijibu kama ifuatavyo; To be better and better and the best there ever was in Tanzania and in Africa. Hiyo ilikuwa takribani mwaka mmoja uliopita katika mahojiano yetu na Nakaaya ambayo unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

Leo hii,Nakaaya anakuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kupata mkataba na kampuni ya SONY MUSIC yenye makao yake makuu jijini New York nchini Marekani.

Kwa habari zaidi soma ujumbe huo mahsusi kutoka kampuni ya SONY MUSIC kama ulivyosambazwa leo kwenye vyombo vya habari.Hongera sana sana Nakaaya.Keep doing ya thing!

Nakaaya’s Photo/Stephen Freiheit

TANZANIAN SONGBIRD NAKAAYA SIGNED TO SONY MUSIC ENTERTAINMENT

An icon of contemporary Tanzanian music, Nakaaya, has been signed to Sony Music

Entertainment. Among the record label’s well-known subsidiaries are Columbia

Records, RCA Records and Epic records, just to mention a few. Nakaaya, who has

acquired a large following and growing fan base across the region, now makes

history by being the first East African artist ever to be signed to the second largest

record company in the world. The company’s roster includes internationallyacclaimed

artists such as Alicia Keys, Beyonce, Britney Spears, Celine Dion, Chris

Brown, Sean Kingston and many more.

The signing took place when Nakaaya was attending the “Music’s Relevance in Third

World Countries” Conference, in Copenhagen, Denmark, in late 2008. (more…)

 

HAINA NGWASU-INSPEKTA HARUNI

Filed under: Bongo Flava,Bongo Fleva,Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 7:43 PM

inspektabc1

Bila ubishi Inspekta Haruni ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava ambao wanastahili na wana haki kabisa ya kujiweka katika lile kundi la “wakongwe katika fani”.Pia Inspekta anadumu katika lile kundi la “wataalamu wa vina(mashairi) na tunzi ambazo baada ya kutoka hewani hugeuka zikawa misemo ya mitaani.

Kama hukubaliani name,basi jaribu kuusikiliza kwanza wimbo mpya kutoka kwa Inspekta unaokwenda kwa jina la Haina Ngwasu kwa kubonyeza player hapo chini.

Na kama jadi mpya ya wasanii wa bongo flava mashairi ya wimbo huu yanaelekea kuwa “ujumbe” kwenda kwa mtu fulani au watu fulani?Mawazo yangu.Sikiliza na wewe utuambie.Pata burudani.

Photo/Ahmad Michuzi


 

“KARIBUNI RAINBOW CLUB”-BONNY LUV January, 19, 2009

Filed under: Burudani,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:37 PM

bonnybc1Endapo kila ifikapo mwisho wa wiki umekuwa miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakijiuliza waende wapi wawapo jijini Dar-es-salaam,BC leo inakuletea habari nzuri.Sasa una mahali pa kwenda. Sehemu hiyo inaitwa Rainbow na ipo maeneo ya Mbezi Beach ukiwa unatokea Michocheni(Kwa Nyerere).

Yapo mambo mawili ya msingi ambayo yanaifanya Rainbow kuwa kimbilio la wapenda burudani jijini Dar-es-salaam.Kwanza klabu hii ndio itakuwa “kijiwe” maalumu kwa wale wenzangu na mie ambao wanapendelea miziki ya “Old School”.

Pili burudani nzima itakuwa ikiporomoshwa na kusimamiwa na DJ mzoefu na ambaye katika watu kumi,tisa wanakubaliana kwamba ni moto wa kuotea mbali na anajua anachokifanya linapokuja suala zima la kukata kiu ya burudani. Huyu si mwingine bali ni DJ Bonny Luv(pichani)

bluvbc

Tulipopata habari kuhusu ufunguzi rasmi wa klabu hii,tulimtafuta Bonny Luv ili tujue machache kuhusiana na klabu hiyo maalumu kwa Old School na burudani zingine.Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi;

BC: Kwanza hongera sana kwa kuanzisha joint mpya na karibu tena ndani ya BC.Mambo yanakwendaje?

BONNY LUV: Shukrani sana kaka.Namshukuru Mungu

BC: Tumekutafuta ili tuongelee kidogo kuhusu hii sehemu mpya ya maraha uliyoianzisha.Kwanza ilikuwaje ukaamua kuanzisha disco hili.Uliona mapungufu yoyote kwenye medani ya burudani hususani upande wa disco? (more…)

 

KWANINI-NURU January, 17, 2009

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 1:15 PM
Tags:

nurumohdbc

Baada ya Walimwengu na Msela, mwanadada Nuru Magram (pichani) hapo jana amefyatua video ya wimbo Kwanini ambao ni miongoni mwa nyimbo 10 zinazotarajiwa kuwemo katika albamu yake aliyoipa jina Walimwengu. Albamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni mnano mwezi wa Machi mwaka huu.

Sikiliza mashairi yaliyomo katika wimbo huu,tazama jinsi hadithi iliyomo kwenye mashairi inavyosimuliwa katika video hiyo.Ukiiangalia kwa makini utagundua kwamba lipo jambo moja ambalo sio la kawaida linatokea katika mlolongo wa simulizi hilo.Sio la kawaida kwani katika simulizi hilo kuna mtu ambaye hafanyi kile ambacho wengi wetu tungetarajia afanye.Itazame kisha uniambie kama unaweza kuona nilichokiona mimi.Pata burudani.Kazi nzuri Nuru.


 

DAWA YA MAPENZI-MBARAKA MWINSHEHE January, 15, 2009

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:02 PM

mbaraka3bc12Kwanza tukuombe radhi kwamba wikiendi iliyopita hatukuweza kukuletea burudani ya wikiendi kama ilivyo kawaida yetu.Maji yalizidi unga au unga ulizidi maji.Vyovyote vile haikuwezakana!

Bila shaka umeshawahi kusikia sana habari za watu kuhangaika huku na kule kutafuta “Dawa ya Mapenzi”.Ushasikia jinsi ambavyo wakati mwingine hufikia mtu akalala kwa karumanzira kisa eti,dawa ya mapenzi.Miaka nenda miaka rudi,imani kwamba dawa ya mapenzi inaweza kupatikana kwenye kibuyu kidogo kilichowekewa ugoro,unyoya wa bata mzinga na takataka nyingine imeendelea kutawala akili za baadhi zetu.

Je kuna dawa ya mapenzi?Ipo wapi?Hayati Mbaraka Mwinshehe anatusaidia kupata jibu la swali hilo hapo juu katika wimbo wake Dawa Ya Mapenzi. Tungependa pia kusikia kutoka kwako msomaji.Je kuna uwezekano wa kupatiwa kidonge cha mapenzi kushinda kile cha upendo,heshima,ushirikiano na maelewano baina ya wawili wanaoamua kupendana?Bonyeza player hapo chini upate burudani.Raha ya wimbo huu,pandisha sauti kisha nyanyuka uucheze.Kama unaweza nenda kabatini tafuta bugaloo kama unayo na kisha achia afro.Mkononi shikilia glass bila kusahau zile san gogo machoni.Wikiendi Njema.