BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MSIBA BOSTON,USA February, 12, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 1:27 PM
Tags:

Ndugu,Jamaa na Marafiki,

Tunapenda kuwajulisha ya kuwa Mzee Leonard NJ Merere ambaye pia ni baba mzazi wa ndugu zetu Naomi na Jacob[JJ] Merere wa Boston-Masachusetts amefariki dunia siku ya Jumanne [Feb 10th 2009] asubuhi hapa Boston,USA.

Marehemu alikuwa  na umri wa miaka 73, ameacha mjane,watoto watatu na wajukuu wanne.

Taratibu na mipango ya  kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es salaam kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa watoto wake huko Boston-Masachusetts.

Kila mmoja wetu anaombwa kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi.

Gharama za kuhifadhi mwili,kusafirisha mwili,Jeneza pamoja na ticket ya atakaye kwenda pamoja na mwili ni dola elfu ishirini[$.20,000].

Ni mzigo mkubwa sana ambao kila mmoja wetu anombwa kusadia ili kukamilisha shughuli hii hasa ukizingatia ya kuwa kwa kadri mwili unavyokaa funeral-home ndio gharama zinavyozidi kuongezeka.

Mwili utasafirishwa punde zitakapopatikana fedha za kulipia gharama.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account ya wafiwa kama ifuatavyo:

NAOMI  MERERE

BANK OF AMERICA,

ROUTE NUMBER :011000138

ACCOUNT NUMBER:009441233628

Au kwa adress hii:

Jacob & Anna Merere

510 Skylinedrive suite # 11

Dracut,MA 01826.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Jacob & Anna Merere [JJ]-978-726-2227 au 978-957-2153.

Naomi Merere-978-413-3722 au 978-632-9823.

Juma Malika-781-244-7353

Saimon Twalipo-978-423-1192

Pastor Abisalom Nasua-214-554-7381

Email-Adress:- RambiRambi@Yahoo.com

Tafadhali chukua muda kuwafariji wafiwa na kuwaombea

Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa kuwasaidia familia Merere !

Mbarikiwe,

Mch.Abisalum Nasua,

Jackson Mollel

Michango-Kwa Niaba ya Marafiki wa Familia ya Merere.


 

7 Responses to “MSIBA BOSTON,USA”

  1. Mwanamke wa shoka (UK) Says:

    Wapendwa poleni sana, na MUNGU awape subira na uvumilivu katika mapito hayo magumu.

    Mungu alitoa na MUNGU ametwaa. Jina lake lihimidiwe.

    May the departed soul rest in peace.

    Amen.

  2. anonymous Says:

    pole

  3. Mattylda Says:

    Rest in Peace Merere,poleni sana wafiwa Mungu awape uvumilivu!

  4. trii Says:

    poleni wa fiwa,

    ushauri mlio huko majuu muwe na chama cha kuzikana/shida,wakati wa shida inakuwa rahisi kusafirisha mwili,sio kujirusha tuu na tuweka mapicha ya magari ya kifahari kwenye web.

  5. Dinah Says:

    Mungu awape uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu cha kiuchumi wakati mnaomboleza. Roho ya marehemu ipumzishwe kwa amani.

  6. Tamu Says:

    $ 20,000 baada ya mazishi familia inaendelea kujirusha. Nawashauri wazike huko huko
    Maana itakuwa rahisi kwa watoto wake kwenda ku visit kaburi maana inaonekana yeye na wanae wamejiweka sana marekani.

  7. DUNDA GALDEN Says:

    NDUGU JAMAA NA MARAFIKI MLIOFIWA POENI SANA NDIO KAZI YA MUNGU HIYOOO


Leave a comment