BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NI KICHEKO TU KWA FRANCIS CHEKA March, 3, 2008

Filed under: Burudani,Michezo,Ndondi/Ngumi — bongocelebrity @ 2:31 PM

 

Pichani ni bondia Francis Cheka(kushoto) na Mbwana Matumla(aliyeipa mgongo kamera) walipokuwa wakipambana mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar-es-salaam.

Bondia Francis Cheka alimshinda Matumla kwa knock-out katika raundi ya kumi na hivyo kufanikiwa kutwaa ubingwa wa UBO(Universal Boxing Association) kanda ya Afrika.Kwa ushindi huo Cheka hivi sasa anahesabika kuwa “mbabe” wa familia ya kina Matumla kwani aliwahi pia kumtwanga bondia maarufu kutoka familia hiyo,Rashid Matumla.

Photo credits:Global Publishers

 

5 Responses to “NI KICHEKO TU KWA FRANCIS CHEKA”

  1. Hahahaaaaaaa Cheka cheka sana kaka akina matumla wamekwisha tena hao, walilewa misifa haooooooooooooo. kwisha habari yao
    Asante Cheka Francis wa Moro kasoro bahari.

  2. Je Cheka unaweza kumpiga Amir Khan kijana mdogo? , kama waweza njoo mi ntakudhamini hehehe

  3. Nyau Says:

    Haha ha! Rashidi jana alikua anahojiwa anasingizia Cheka anatumia uchawi?! duh wabongo bwana hawakubali kushindwa! ingekua hivyo Tyson angekua mnageria. Haha! nilishuhudia papmbano nafikiri mazoezi ni muhimu, hata kama si mtu wa Cheka Jabu zake mwanangu UTACHEKA hahaha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  4. jomaeli Says:

    mnapigana bila sababu za msingi

  5. festo Says:

    Siri ya mafanikio ni kuongeza juhudi na kujifunza makosa kwa waliyoshindwa,cheka yupo taiti zaidi,sasa kina matumla wamlete ndugu yao mwengine.


Leave a comment