BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MANENO MANENO-DDC MLIMANI PARK February, 12, 2009

Filed under: Burudani,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:44 PM

sikinde

Katika medani ya soka nchini Tanzania,inaaminika kwamba kama wewe sio mshabiki wa Yanga(Watoto wa Jangwani) basi ni mshabiki wa Simba(Wekundu wa Msimbazi).Hivyo ndivyo ambavyo imekuwa tangu enzi na enzi.

Kwa upande wa muziki wa dansi,inaaminika kabisa kwamba kama wewe sio mnazi wa Sikinde basi ni wa Msondo.Utashi na ushindani uliopo katika muziki wa dansi ni sawa kabisa na ule uliokuwepo katika soka la bongo.

Haishangazi basi kusikia kwamba uvumi ulipoenea jijini Dar-es-salaam mapema wiki hii kwamba DDC Mlimani Park Orchestra imesambaratika,habari hiyo haikuwa nzuri hata kidogo kwa mashabiki wa muziki nchini Tanzania achilia mbali wanazi wa Sikinde.Hakuna ambaye alitaka kuamini kwamba inawezekana ikawepo Msondo bila Sikinde.

Lakini sio kweli kwamba Sikinde ndio imefikia tamati.Kilichotokea ni kwamba kumekuwepo hali ya kutoelewana katika mambo fulani fulani baina ya uongozi wa DDC(Shirika la Maendeleo la Dar-es-salaam) ambao ndio walikuwa wamiliki wa bendi hiyo na hivyo kuitwa “DDC Mlimani Park Orchestra).Matokeo yake ni kwamba bendi hiyo,kuanzia tarehe 1 Machi mwaka huu itaanza kujiendesha yenyewe bila usimamizi wala udhamini wa DDC.Na kuanzia hapo watajulikana kama Mlimani Park Orchestra. Kwa hiyo mashabiki wa muziki wa dansi,Sikinde bado ipo!

Naam baada ya ufafanuzi huo,leo ni mwanzo wa weekend.Hapa kwetu BC ni kama jadi.Ni wakati wa zilipendwa.Wiki hii kwa upande wangu binafsi imekuwa ngumu kidogo.Imekuwa na maudhi ya haja.Si unajua inavyokuwa pale unapomthamini mtu na kujaribu kumtendea kila aina ya wema unaoweza lakini yeye akakuona kama kinyesi tu?Inaudhi eenh?Basi hali hiyo ndiyo iliyonikumba.Ni vurumai za maisha ambazo kwa kweli huwa natamani zingekuwa na suluhisho la kudumu!

Bahati nzuri ni kwamba zipo nyimbo kama hii ya leo ya Maneno Maneno kutoka kwao wana Sikinde,ambayo inaweza kusaidia pindi joto la nyikani linapojiri.Hakuna haja ya maneno.Inafikia mahala lazima utulie na kumuachia Mola.Usikilize wimbo huu kwa makini lakini wakati huo huo usisahau “kujirusha”.Kibao hiki kitabakia kuwa mojawapo ya kumbukumbu nzuri za Sikinde wakiwa kama DDC Mlimani Park Orchestra.Tunawatakia kila la kheri katika safari yao mpya kama Mlimani Park Orchestra.Tunaamini kwamba Sikinde will always be Sikinde.Ciao


Picha ni kundi zima la wanamuziki wa Mlimani Park Orchestra kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar mapema wiki hii.Picha na John Bukuku.


 

7 Responses to “MANENO MANENO-DDC MLIMANI PARK”

  1. kabwe makanika Says:

    Ni kweli kama ulivyosema hapo kuwa sikinde na msondo ngoma kwetu sisi wa wakati ule tunachukulia kama simba na yanga. kulikuwa na ushabiki wa kupindukia wewe kama sio nginde basi lazima ungekuwa msondo. ni bendi ambazo tunapaswa kujivunia kwa kuwa hata haya maendeleo ya muziki wa sasa imetokana na kazi kubwa za bendi hizi.

    Wimbo huu unanikumbusha mbali sana, wakati huo tungo zilikuwa na maana sana na ziligusa maisha na isia za watu.wakati mwingine mtu ungeweza kuepukana na kuondokana na msongo kwa kusikiliza nyimbo kama hizi. asante bc kwa kutukumbuka vijana wa wakati huo.

  2. Edwin Ndaki Says:

    BC pole sana na maswahiba yalikusibu juma hili..Si unakumbuka Msondo Ngoma Music Band wanakwambia Kaza Moyo!

    Ila kweli nimefurahi kuona NGINDE hawajafa…maana mimi ni MNAZI wa MSONDO..waache waendelee kuvuta vuta..ila wanajua kuwa Msondo ukubwa dawa tuliyaona hayo zamani ndio maana mapema tukachukua vyetu..lol..

    Kila la kheri wazalendo woote hapa..

    tutafika tu

  3. Rahma Says:

    BC,asante sana kwa wimbo huu.Ni kweli kabisa maneno maneno hayana msingi.Na aliyekuudhi ashindwe na alegeelegee kabisa.wikiendi njema wadau

  4. […] In other news, BongoCelebrity has a Swahili story on DDC Mlimani Park Orchestra that you can find here. […]

  5. DUNDA GALDEN Says:

    HOME SICK IN WEEEEEKKK NENDA SAFI BC WADAU NAWATAKIENI WIKI END NJEMAA

  6. SM Says:

    Pole BC. Basi wewe ni mtu mzuri saaana. na huyo mtu lazima ni mtu mbaya saana. tenda wema uende zako usisubiri shukurani.

  7. Mattylda Says:

    Pole sana Bc,japokuwa nimechelewa kurusha pole lakini zikufikie,usijali walimwengu hao ninawakemea ktk jina la yesu hakika watashindwa na kulegea!

    mimi ndo wa kale jamani nazimika na flag maneno maneno mhhh kazi nzuri!


Leave a comment