BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SALAMU ZA FA KUTOKA COVENTRY February, 16, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Elimu na Maendeleo,Muziki — bongocelebrity @ 2:33 PM

fabc1

Hakuna ubishi kwamba kijana Hamis Mwinjuma au maarufu kama MwanaFalsafa(MwanaFA) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao wamefanikiwa.MwanaFA amefanikiwa sio tu kufikisha ujumbe alioukusudia kwa jamii bali pia kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yake kupitia muziki.Miziki yake imekuwa ikiimbwa na watu wa rika mbalimbali.Hayo nayo ni mafanikio.

Pamoja na mafanikio ya kimuziki au kisanii aliyonayo MwanaFA,anabakia kuwa mfano wa kuigwa linapokuja suala zima la elimu,muziki na maisha.Hivi karibuni alithibitisha hilo pale alipoamua kurejea tena shule.Safari hii ameelekea nchini Uingereza.

Nini kinamsukuma kijana huyu katika nyanja ya elimu? Na je hivi karibuni alipoachia wimbo unaokwenda kwa jina “Msiache Kuongea” alikuwa anamjibu Inspekta Haruni?Anazungumziaje maisha ya nchini Uingereza?Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi na MwanaFA

BC: Pamoja na mafanikio mazuri katika muziki kule Bongo bado umeamua kurudi tena shule.Nini kinakusukuma?Hapo UK umeenda kusomea nini na katika chuo gani?

FA: Kuna mengi yanafanya nifanye nnachofanya.Lakini kubwa na la msingi zaidi ni kuwa na nguzo nyingine kwa ajili ya maisha ninayoishi(Plan B).Kama unavyojua muziki pamoja na kuwa unakwenda vizuri lakini hautabiriki sana.Ni ngumu kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kwa angalau miaka 10 ijayo.

Na zaidi ni kuwa naona kama kuna muda mwingi kama msanii wa kibongo nakuwa naupoteza kwa kutofanya chochote baada ya kurekodi(ambayo sio kila siku),kufanya shows(mara nyingi huwa weekends),matangazo(mara chache kama una bahati) na interviews ambazo nazo sio kila siku.Kwa hiyo kwenye wiki kunakuwa na muda mwingi unaenda bure ambao nimeona ni vyema nikautumia kufanya kitu kitakachozalisha.
Hapa UK nasoma Msc Finance na nipo Coventry University.

BC: Una mpango gani na muziki kwa hivi sasa?Kama utaendeleza muziki na shule vilevile,lini labda wapenzi watarajie albamu yako mpya? (more…)

 

NALIVUA PENDO-MWASITI February, 1, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Single/Mpya — bongocelebrity @ 10:30 PM

mwasitibc

Mojawapo ya mambo mazuri ambayo yanatokea nchini Tanzania hivi leo ni kuibuliwa kwa vipaji mbalimbali miongoni mwa vijana na kitu kinachoitwa Tanzania House of Talent (THT).Kama umewahi kuhudhuria shughuli ambapo miongoni mwa watoa burudani walikuwa ni vijana wanaotokea THT bila shaka utakubaliana nasi tunaposema kwamba vipaji vipo nchini Tanzania.Kinachotakiwa ni uongozi na mikakati mizuri ya kuviboresha na kuvionyesha ulimwenguni.

Miongoni mwa vipaji vilivyowahi kuibuliwa na THT ni mwanadada Mwasiti(pichani).Msikilize hapa katika wimbo wake mpya uitwao Nalivua Pendo kwa kubonyeza hapo chini.Kazi nzuri Mwasiti!


 

HAINA NGWASU-INSPEKTA HARUNI January, 29, 2009

Filed under: Bongo Flava,Bongo Fleva,Burudani,Muziki,Single/Mpya — bongocelebrity @ 7:43 PM

inspektabc1

Bila ubishi Inspekta Haruni ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava ambao wanastahili na wana haki kabisa ya kujiweka katika lile kundi la “wakongwe katika fani”.Pia Inspekta anadumu katika lile kundi la “wataalamu wa vina(mashairi) na tunzi ambazo baada ya kutoka hewani hugeuka zikawa misemo ya mitaani.

Kama hukubaliani name,basi jaribu kuusikiliza kwanza wimbo mpya kutoka kwa Inspekta unaokwenda kwa jina la Haina Ngwasu kwa kubonyeza player hapo chini.

Na kama jadi mpya ya wasanii wa bongo flava mashairi ya wimbo huu yanaelekea kuwa “ujumbe” kwenda kwa mtu fulani au watu fulani?Mawazo yangu.Sikiliza na wewe utuambie.Pata burudani.

Photo/Ahmad Michuzi


 

NJOO-PROF.JAY ft KLEPTOMANIACS January, 21, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Single/Mpya — bongocelebrity @ 8:05 PM

prof-jay-bc1

Wakubwa wanapopiga kelele kuhusiana na sera za Jumuiya ya Afrika Mashariki,vijana wao wanafanya kazi.Wanashirikiana bila kusita katika kazi zao,hususani za kisanii.Sio kwamba nafananisha siasa na sanaa..hapana…nasema tu!Pengine kuna lolote wakubwa wanaweza kujifunza kutoka kwa vijana?Sina uhakika.

Ushirikiano ninaouongelea hapa ni ule wa Prof.Jay(a.k.a Red Carpert) katika single mpya iitwayo Njoo.Katika wimbo huu ambao umo katika albamu yake ya Aluta Kontinua(kama hujanunua kopi yako halali,fanya hivyo)Prof.Jay amewashirikisha wasanii kutoka Nairobi, Kenya wanaokwenda kwa jina la Depicto/D.E.P(jina kamili Collins Majale) na Nyashinski(jina kamili Nyamari Ongegu) na Munkiri(jina kamili Robert Manyasa) kutoka kundi linalojiita Kleptomaniacs.Wimbo huu umerekodiwa jijini Nairobi chini ya Producer Msyoka.

Hebu sikiliza jinsi hali inavyokuwa Kiswahili cha Dar kinapokutana na kile cha Nairobi.Patamu.Pata burudani.

Picha kwa hisani ya DJ Choka.


 

MSIACHE KUONGEA-MwanaFA ft LADY JAY DEE

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Single/Mpya — bongocelebrity @ 8:00 PM

mwanafabc10Ukishakuwa na umaarufu fulani ni wazi kwamba unakuwa kipenzi cha vyombo vya habari.Yaweza kuwa kwa mazuri au kwa mabaya.Watu hupenda kusikia mtu maarufu fulani kafanya nini,anapanga kufanya nini nk.

Mbali na vyombo vya habari,mitaani pia(labda kupitia walichokisoma gazetini au kukisikia redioni) maneno huwa hayaishi.Huko nako ni mwendo mdundo.Aidha kupewa “ushauri wa bure” au maneno yaliyojaa chuki binafsi na yenye nia ya kumuangamiza mtu.Ndio maisha yalivyo.

jide-komandobcLakini maneno yakizidi huwa yanaweza kuwa kero.Na hali ikifikia hapo,basi sio vibaya kukumbushana kwamba hapo sipo na mambo kama hayo.Maisha lazima yawe na uwiano.Kukumbushana tunapoteleza,kusifia inapobidi na siku zote kuwezeshana.

Sikiliza wimbo huu mpya kutoka kwa MwanaFA akiwa ameshirikiana na Lady Jay Dee.Wimbo unaitwa Msiache Kuongea. Katika chorus sikiliza kwa makini kwanini Jide na FA wanasema Msiache Kuongea.Kisha sikiliza kwa makini mashairi yaliyomo.Kazi nzuri FA na Jide.



 

I AM A PROFFESSIONAL- FID Q January, 15, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Muziki,Sanaa/Maonyesho — bongocelebrity @ 1:17 PM

fid-qbc

Bongo,Bongo…ooh Bongo!Kila kukicha watu wanazidi kuwa wabunifu na wagunduzi. Kila siku akili zinazidi kuchemka, bongo zinazidi kutenda kinachotakiwa kutendwa.

Kama bado huamini kwamba Bongo inazidi kuja juu kwa ubunifu,basi jaribu kwanza kutizama hapo chini video mpya kutoka kwa Fareed Kubanda aka Fid Q(pichani) iitwayo I AM A PROFFESSIONAL ambayo ni single ya tatu kutoka kwenye albamu yake iitwayo Darwinz Naitmea.Kutoka kwetu hakuna la ziada bali pongezi kwa Fid Q kwa ubunifu na uchapa kazi.


 

THE MAKING OF “SAUTI YA GHETTO” January, 5, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Muziki — bongocelebrity @ 12:11 PM

Bila shaka utakubaliana nasi tukisema kwamba viwango vya ubora wa video za miziki kutoka Tanzania vimekuwa vikipanda siku baada ya siku.Siku hizi video nyingi zinakuwa zinaonyesha sio tu uhalisia bali pia zinabeba maudhui mazima ya nyimbo husika.Kwa hilo ni lazima tuwapongeze wasanii na pia waongozaji au watengenezaji wa video hizo.

Hali hiyo ndiyo tuliyoishuhudia hivi karibuni tulipotembelea kambi ya Prof.Jay wakati wa kutengeneza video yake ya wimbo Sauti ya Ghetto ambao umekuwa ukikamata mawimbi ya radio nchini Tanzania kwa muda sasa.Video hiyo inatarajiwa kutoka rasmi mwishoni mwa wiki hii.Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka katika shooting hiyo.Unaweza kuusikiliza wimbo huo kwa kubonyeza player hapa chini.


prof-jay-dj-choka-bc1

Prof.Jay(kushoto) akiwa na DJ Choka.

making-video-sauti-ya-gettobc

Sauti ya Ghetto:The Making

prof-jay-making-video-sauti-ya-gettobc

Prof Jay akiunguruma kutokea Ghetto.Hapo ni maeneo ya Magomeni Kagera.

 

WAPI BESTA? January, 4, 2009

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 6:15 PM

bestabc1

Msomaji wetu mmoja ametuandikia akitaka kujua alipo mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,Besta(pichani) kwani hajamsikia kwa muda mrefu.Ukweli ni kwamba hata sisi hatuna jibu la uhakika ingawa fununu tulizonazo ni kwamba Besta alirejea nchini Uganda kumalizia masomo yake aliyokuwa ameyakatisha.Alikuwa anasomea masuala ya Habari na Tekinolojia.Besta aliwahi kutamba sana na wimbo wake Kati Yetu ambao unaweza kuutizama kwenye video hapo chini.Kama kuna mtu ambaye ana habari za uhakika zaidi,tusaidiane tafadhali.