BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

Ze Comedy waibuka kama Original Comedy na kuteka nchi October, 17, 2008

Filed under: Burudani — bongocelebrity @ 9:27 AM
Kundi la Original Comedy wakiwa katika Studio za TBC1 wakati wa mazoezi ya onesho lao ambalo limepokelewa kwa shangwe na washabiki wao toka warudi hewani wiki mbili zilizopita. Hivi sasa hakuna anayetumia jina lake alilokuwa anatumia EATV bali sasa wana No-Name 1 hadi 7. Kesho Original Comedy wanafanya onesho lao la kwanza la wazi katika ukumbi wa Diamond Jubilee

Kundi la Original Comedy wakiwa katika Studio za TBC1 wakati wa mazoezi ya onesho lao ambalo limepokelewa kwa shangwe na washabiki wao toka warudi hewani wiki mbili zilizopita. Hivi sasa hakuna anayetumia jina lake alilokuwa anatumia EATV bali sasa wana No-Name 1 hadi 7. Kesho Original Comedy wanafanya onesho lao la kwanza la wazi katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Kipindi cha kwanza cha kundi hilo kilirushwa na televisheni ya taifa TBC1 huku kikionyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa kulikuwa na vituko vya aina mbalimbali. Kundi hilo limekuja na sura mpya baada ya majina yote ya wasani hao kubadiliwa huku na jina lakipindi chenyewe likibadilika kutoka ze Comedy hadi Comedy Original. Baadhi ya washabiki wa kipindi hicho wameelezea kufurahishwa kwao na kurejea kwa maonyesho ya kundi hilo na kusema afadhali watapata muda wa kufurahisha pindi wanapokuwa majumbani kwao. Picha kwa hisani ya issamichuzi.blogspot.com

 

51 Responses to “Ze Comedy waibuka kama Original Comedy na kuteka nchi”

  1. Edwin Ndaki Says:

    Bc kwanza nashukuru kwa kurejea kwako ingawa bado nina swali BC timu upepo unaenda vema?

    Maana leo tumenyimwa haki yetu.Unajua mazoea ni kama SHERIA.

    Leo ijumaa nilijua nikitua tu hapa lazima nikutane na songi la kusindikiza wiki endi yangu.

    Lakini naamini mtakuwa na sababu nzuri kuhusu ili..ila naamaini kwa kusikia hiki kilio utafidia kesho kutuwekea songiiiii au j3 haitagomba.

    wiki endi njema wadau

    tutafika tu

  2. Anna G Says:

    waoooooo commedd so good to saw u again.big up

  3. halima Says:

    Aisee hawa jamaa wanatisha ile shoo ya wimbo wa rose muhando nibebe, ilikuwa funika lakini wadau mbona kama kuna mtu mmoja hayupo hapo (Vengu) mwenye kufahamu habari zake anifahamishe tafadhali.

  4. Frateline Says:

    Hi Guys kutoka helsinki-Finland

    Ninawapongeza BC kwa kufikisha maoni yetu kwa hawa vijana maana tuliwashauri hata wakiingia bila majina sura zao tiyari ni trade mark, hawa vijana kwa kweli wamekamilika na katika fani hiyo ya comedy wanapatia kabisa, yaani ninawafananishi kabisa kama comedians wa marekani ambao wamekuwa wanawaingiza wagombea Urais wa Marekani hasa hasa kuna dada mmoja anaigiza kama Sarah Palin anayegombea umakamu wa Rais kwa tiketi ya Maccain,

    Ushauri kwa vijana, watumie fani yao kutoa elimu na kupambana na rushwa wasijipendekeze kwa watu wanaojifanya ni CCM kumbe ni mafisadi tu, vijana chapa kazi, kumbukeni, ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni maana waweza kumfananisha na nduguyo, hakuna utani kazi, mimi ninawatakia kila kheli ktk kazi zetu

    Frateline

  5. aisha Says:

    Mimi siwa fagilii ata kidogo ila mtu mmoja tu tangu zamani nampenda mcheshi na anajua kazi seki basi nampa big

  6. binti-mzuri Says:

    yes! patamu hapo

  7. Hombiz Says:

    good for you guys. Keep your heads up!
    All the best!

  8. Matty Says:

    Welcome back!!!!!!!!!! seems that mmekuja kutushika thoughhhhhhh tutafika!

  9. PANDU Says:

    Hawana jipya hawa…wanaganga njaa tu.

  10. BLACKMANNEN Says:

    Watanzania wengi ni watundu wa kuyatafuta maisha. Hili ni jambo linalotia moyo sana kwa wapenda maendeleo wote. Lakini kuna watu wengine, wenye roho za kutu wanaorudisha nyuma maendeleo ya wenzao kama walivyofanya EATV kwa vijana hawa wa “Ze Comedy” ambao leo hii wanaitwa “Orijino Komedy”.

    EATV wananikumbusha simulizi moja niliyosimuliwa kuwa, kulikuwepo mtu mmoja aliyekuwa na shamba lake na vifaa vyote vizuri vya kulimia shamba, lakini hakuwa na wakulima.

    Kwa bahati nzuri, ambayo hakuitegemea, mwenye shamba huyu, alipata wakulima wazuri, na stadi sana, waliokuwa wanaifahamu sana, kazi ya shamba. Mwenye shamba huyu, aliwachukua wakulima hao, na wao, kwa kujituma na umahiri waliokuwa nao, waliimudu kazi ya shamba, kuliko hata mwenye shamba alivyotegemea.

    Baada ya kupata mavuno mazuri, Bwana shamba huyu, akawasahau wakulima wake, kuwagawia japo kidogo masalia ya mazao aliyokuwa akipata shambani mwake. Badala yake alianza vitimbwi na kuwageuzia kibao wakulima wake, kwa kuwapakazia hili nalile. Alikuwa akiamini kuwa wakulima hao wasingemwacha, kwa vile aliamini kuwa hakukuwa na shamba lingine kubwa na zuri lenye rutuba nzuri kama shamba lake.

    Mwenye shamba huyu aliamini kuwa, kutokana na vimakombo vidogo alivyokuwa akiwagawia wakulima hao, wasingeweza kumwacha, na kama wangemwacha, alipanga kuwanyima vijimakombo vyake, ili njaa yao iwarudishe kwake, ama wafe na njaa kule waendako. Akawanyang’anya hadi mavazi yao ya kazi.

    Orijino Komedy, wameuthibitishia umma wa Kitanzania kuwa, mkulima stadi, haishi na wala hafi kwa njaa ya kukosa vijimakombo vya Bwana mwenye shamba. Orijino Komedy, wamemwachia kila kitu EATV achukue, akidhani kuwa kwa kung’ang’ania majina yao, ndiyo atawaua. Sasa EATV, wanaaibika mbele ya umma zima la Kitanzania, kwa kuonyesha roho zao za korosho, zenye nia ya kuwarudisha nyuma watu watundu (Ze Comedy) wajitumao kujitafutia maisha. Hongereni sana “Orijino Komedy” na karibuni tena machoni petu, tunawapenda sana.

    This Is Black=Blackmannen

  11. Farid Says:

    Picha sio bora kama walivyokuwa EATV pili lile tangazo la Daktari Bingwa na Changudoa halina mantiki na ni baya kwa malezi kwani kipindi kinapendwa sana na watoto na tangazo halieleweki maana yake nini hasa. Litolewe

  12. Kunza Says:

    Kuna advt sijui ya dr na cd inabore kichiz

  13. shubi Says:

    KARIBU SANA ILA VENGU YUKO WAPI?

  14. bambucha Says:

    eti mbona mmoja hajaonekana yule anae penda kuwaigiza wachaga????????/ tunamiss sana. hongereni sana kwa kazi njema.

  15. Mswahilina Says:

    Mkuu Jeff wa BC,
    Hawa ni wachovu wa kuchoka na kuchakaa.
    Hawana kitu tena.

    Tusubiri tuone hatima yao maana Fisadi Manji amewamaliza.

  16. Dunda Galden Says:

    BC VIPI? KULIKONI KAMA MNAHITAJI MSAADA WA KIUFUNDI TUPO
    KWANI SISI NI WENZENU PIA MSIUCHUNE JAMAANI
    NATUMAI TUNAJULISHANA KWA KILA HATUA KULIKONI

  17. Uncle mimi ! Says:

    vijana wanajitahidi sana!lakini yabidi wawe huru kwani wakikubali kuingiliwa basi watakuwa wamejimaliza wenyewe!sipendi wafadhili wanaojiingiza ingiza kwani wanatishia uhuru na ubunifu wa vijana kwani wengi wao wana some political affiliation!nafikiri wamenielewa sasa! kuwasaidia ni kuwa wasiogope kutoa hata kibwagizo cha raisi kupigwa mawe!si mmeona hata Bush anaigizwa?

  18. bestinox Says:

    Duh hawa jamaa full full mizuka…Wamerudi tena???I hope watakuja na mizuka ya ajabu hasa ukizingatia waliwekwewa zengwe siku za katikati!!!

  19. mleba Says:

    mimi siwakubali hata kidogo,kwasababu kila wanachokitoa wanachukua kwenye matukio ya kila siku.kama vile bungeni,kifo cha wangwe – sina haja ya kuendelea sana kwasababu wote mnajua.

    kwa maana nyingine baada ya muda mfupi watu wengi watajitokeza kufanya shughuli kama yao kwasababu ni rahisi sana kuugiza kitu ambacho kimesha tokea(jamani nina zungumza kama mwalimu wa waigizaji).kumfanya mwezio kichekesho sio ubunifu.

    jamani ubunifu katika dhana ya uigizaji nikubuni kitu ambacho ni kipya watu wakakipokea na kukikubali.sio kuigiza kifo cha chacha wangwe au kumuigiza muheshimiwa spika mambo anayo yafanya bungeni.

    kwahiyo watavuma sana lakini ni kwa muda tu.na watu wengi watajitokeza kuwaiga kwasababu ni rahisi sana kufanya hivyo – kiuigizaji.

    halafu kwa taarifa yenu muigizaji huwa abadilishi jina,ukiangalia hata wenzetu e.g bill cosby,mr.cooper e.t.c

    unapobadilisha jina unabadilisha mizizi ya wewe kupendwa na hiyo ina tokana na umasikini.wanatakiwa wawe na uwezo wa kurekodi michezo yao na kuwauzia tv mbalimbali ivyo ndio inavyo takiwa kwa sababu kama umaarufu wanao tayari.

    ushauri – original comedy wakitaka wasipotee haraka ni razima waanze kutunga hadithi au kichekesho e.t.c. yao wenyewe na sio kilasiku kukaa kutwa nzima wanaangalia tv alafu wanakuja kuyarudia yale yote katika mtindo wa kiuchekeshaji.hawata dumu kwenye fani.

    watuwengi walionzisha vikundi vyao kama hivi uko ulaya havipo tena

  20. BLACKMANNEN Says:

    Watanzania wenzangu wachangia mada za hapa BC, nawaomba tusiwe wachoyo wa fadhila. Tuwe tukiwapongeza Watanzania wenzetu wabunifu wa mambo ya aina zote, wanaotuletea maendeleo na kuiweka Tanzania katika ramani za nchi zinazojulikana Afrika na duniani kote.

    Maneno kama, “nawafagilia, wanatisha, nawazimia, wadau, changudoa, wachovu, ngangari, mafisadi” ni wabunifu wetu, wa kiswahili wameyaleta maneno haya, katika kuikuza lugha yetu ya kiswahili.

    “Bongo”=Tanzania, ni wabunifu wetu wa mambo, wameibatiza jina jipya, lisilo rasmi nchi yetu Tanzania. Kwa maendeleo ya mawasilano na maelewano yaliyochangiwa na wabunifu hawa, Tanzania sasa, tupo mbali sana ukilinganisha na nchi zingine za Kiafrika na hata za Ulaya, kama vile Albania na Kosovo, pia huko Asia, Kirgizistan, Afghanistan na Mongolia.

    Tunapopata kikundi cha wabunifu kama “Orijino Komedy”, Akudo, Twangapepeta, waimbaji wa nyimbo za mipasho, Injili na wengine, hata wawakilishi wetu BBA, ni vizuri kuwapa moyo, badala ya kuwashambulia kwa maneno ya kejeli na madharau na hata kuwaingilia katika mambo yao binafsi yanayopingwa katika misingi ya haki za binadamu.

    Watanzania, tukumbuke tulikotoka. Filamu ya kwanza ya Kitanzania (1974)-Fimbo ya Mnyonge, kila mtu aliipenda na kuisifia. Michezo ya Redio-RTD (Kina Upara), na pia, akina Pwagu Na Pwaguzi, wasanii wake tuliwapenda sana, japo tulikuwa hatuwaoni machoni petu, ila kuwasikia redioni tu. Je, mshikamano na upendo wetu wa Kitanzania, vimeenda wapi siku hizi? Au kwa vile siasa yetu wakati ule ilikuwa ya “Jamaa Na Kujitegemea”, tulijaliana zaidi kuliko sasa?

    Nimelazimika kuandika gazeti zima hapa, kutokana na jinsi ambavyo, mimi inaniumiza roho sana, tunapowashambulia wasanii wetu watundu wa kufanya mambo mbalimbali katika kujiinua kimaisha kwa njia ya kuwaburudisha, kuwaelisha na kutoa changa moto kwa wengine, kwa kutumia vipaji vyao katika kujikwamua katika hali ngumu ya maisha iliyoikumba nchi yetu na dunia yote.

    Willy Smith na mkewe, walipokuja Tanzania, kila mtu alikuwa akiwasifia. Mtu aliyejaribu kuwalinganisha Willy Smith na akina “Masanja Mkandamizaji” wetu, alishambuliwa kama vile katamka neno la kashifa fulani Serikalini.

    Tujitahidi kurekebishana na kuelimishana, kwa njia ya kistaarabu. Tunapoona mwenzetu ametereza katika shughuli zake za kisanii, tusimshambulie, mbona sioni mashambulizi makali kwa Taifa Stars, kama ilivyokuwa kwa LaToya wetu? Nchi yetu bado changa, hicho tunachokipata, japo kidogo, nawaomba tujivunie na hichohicho.

    This Is Black=Blackmannen

  21. zyb Says:

    Kwakweli wananipa mashaka sana sababu kuna wakati huwa nashindwa kujua kama wanatufundisha nini!!!!!!!! ETI TANGAZO LA CHANGUDOA, AU DAKTARI MTOA MIMBA!!!!!! Afadhali lile la house girl ukimuangalia kwa makini linachekesha. TOENI HAYO MATANGAZO MAWILI HARAKA MAANA WATEJA WENU WAKUBWA NI WATOTO. Otherwise msibweteke maana wenzenu FUTUHI wanajaribu kuelimisha zaidi jamii of which ndo kitu tunachotarajia kutoka ktk hizi comedy.

  22. Mary Mkwaya Malamo Says:

    Show imetulia but…., yale matangazo yenu “Madada poa” na “daktari bingwa wa kutoa mimba” siyapendiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!….!

  23. BROM Says:

    Washkaji wako tit.jamaa wanavipaji.eatv walidhani wanawaharibia ila wamejiharibia wao kwa sababu sisi ndio watazamaji kutuondolea hawa jamaa wametuboa.TBC big up.original comedy is wounderfull

  24. kahindi Says:

    Haha hahaaa…unayejiita Anna G hapo no 2….lugha za watu ngumu…kama vipi we andika tu kiswahili….na nyie orijino komedy,tafadhali toeni hayo matangazo yenu ya kutoa mimba sijui na ni eti vile…changudoa,hayana mafunzo yoyote..mtu wangu SEKI kama ni ubunifu pale ni ZERO…

  25. dj valle Says:

    very nice guys,for coming back,realy its back in bussines,even bony and kitambi are happy now.

  26. 1234 Says:

    Ana G saw ni past tense ya see sasa mbona hueleweki jaman ulisoma wapi weye???

  27. binti-mzuri Says:

    kahindi shosti kahindi..hayaa!mi simooo!lol ila nachekaaa tuu kwa raha zangu

    blackmannen shusha mambo,umeongea vipointi pointi apo naona

  28. luck_lady Says:

    niliwapenda sana hawa vijana but now naona kama wanapotea vile coz hawatupi tulivyokuwa tunapata.

    they have to be very carefuly ili wasije wakafika wao omega na wakabaki midomo wazi na watu wanao wapa vichwa wakawakibia.

    wamshukuru Mh. Mengi coz amewatoa na wakakubalika sasa wasijifanye wajanja sasa, wasije wakarudi huku wanalia.

    chaoooooooo!!!!

  29. kahindi Says:

    bint mzuri we cheka tu shosti ila huo ndio ukweli….haha am coming to bukobaaaaaaaa

  30. binti-mzuri Says:

    luck lady ‘mh mengi’?yule nae kawa mheshimiwa lini,au kisa kuwa tajiri?

  31. Ibin Says:

    Anna G, usituletee habari za ‘Mimi Maimuna’. Lugha kama haipandi waachie wenye uwelewa noyo.

  32. halima Says:

    hahaaaa kahindi umenichekesha kweli hizi lugha bwana Anna G hongera kwa kuwa saw comedy. Kwi kwi kwi

  33. halima Says:

    wewe mleba mimi sioni ulichoongea cha msingi, kwani hata wakiigiza kitu kilichotokea kinachotakiwa ni ujumbe uwe umefika acha roho mbaya mmmh

  34. Ebwana si mchezo yaani jamaa wapo fresh! Ni talent kweli sio ubabaishaji tuliwa~miss sana! “hey guyz welcom back!!!” wishing u al da best!

  35. chapombe Says:

    tusubiri tuone huu ujio wao mpya maana mi nina wasiwasi kwamba wanaweza kufisadiwa kwasababu tayari wana maadui

  36. bdo Says:

    sijui lakini je wameishapata haki miliki tayari au ndoa ikivunjika muanze kutumbua na habari zenu kuwa mnaonewa, maana biashara haifanyiki majukwaani kama siasa, hii ni art sio mnaanza kutafuta wanasiasa ku-solve issue zen, fuateni ushauri wa no.19 hapo juu, uzeni kazi mkiwa huru, TBC1 wakiwatimua mtatusumbua kuhamia ch.10, au agape TV

  37. kahindi Says:

    hahaaaaaaaa hahaaa bdo umenichekesha…agape Tv ???? unamtafuta Mungu maneno weye…

  38. kaboka Says:

    Heshima vijana tanguliza kwanza mbele..anaimba afande sele,nadhani amerudia mashairi ya wimbo wa zamani kidogo,Hivyo nawashauri hawa vijana wausikilize kwa makini huo wimbo watapata ujumbe wangu.

  39. Oya washkaji vipi JK mnamuogopa au vipi? Mbona hamjamuonesha alivyopopolewa mawe? Kama vipi fanyeni mpango mtupe laivu!

  40. MM Says:

    Mleba ndugu yangu umeongea pointi nzuri tu na kuwashauri hao original comedy vizuri tu…

    Ila naona kuna watu wengi humu ndani hawajakulewa na wanadhani mtu akitoa `constructive criticsm` ni jambo mbaya.. wewe ni mtalaam wa sanaa..

    mimi kakuunga mkono hawa the Original comedy kama hawatakuwa wabunifu zaidi kundi leo sasa hivi litakufa… nadhani pia waombe ushauri wa wataalam wa sanaa ili mambo yao yaende vizuri.. BLACKMAN hata kama mtu anakipaji cha sanaa lazima akiendeleze kitaalam sio local kama hao original comedy wanavyotaka kufanya… mimi nawaona they just too local na hawana professionalism ktk kazi yao..ila ngoja tusubiri how long they will last..

  41. sisterTZ Says:

    kaka BLACKMAN kutoa critism sio roho mbaya ni njia moja wapo wa kuwasaidia hao wasanii kujiendeleza upo hapo? Wadau endeleni tu kukosoa maana ukikosolewa ndio unajifunza zaidi..maana mtu anayekusifia hana jipya

  42. bibi umeme Says:

    nyie watu mnanichekesha kweli when correcting people’s english……..someone should also start correcting people’s kiswahili, coz that’s our language that we should master english is a second…….all in all Big up comedy, i never watched it much in EATV and am not going to start with TBC but equally i cant discredit what u guys do, also am glad tht fellow TZ are representing big time..

  43. gebo arajiga Says:

    Kwa kweli sasa hivi naona wameanza kuchemsha hawa ndugu mchezo wa last week ulikuwa ni mbaya wala hakuvutia au mnasemaji ndugu zangu.

    From Arusha.

  44. BLACKMANNEN Says:

    Kwako wewe “Nassor Jangwa”, comment nr.39!!!

    Sijakuelewa maana yako ya kusema kuwa “…JK mnamuogopa au……..”.

    Kama nia yako ni kutaka kuleta hapa mada za kushabikia uhalifu, mimi nakushauri utafute sehemu nyingine, sio hapa BC.

    Kushambuliwa kwa msafara wa Rais wa nchi yetu mawe, huko Mbeya, ni kitendo cha kulaaniwa vikali na wapenda Amani na Utulivu wa nchi yo yote, mahali popote duniani, bila kuangalia rangi, dini na wala itikadi za kisiasa. Tushukuru kwamba silaha zilizotumika na washambuliaji hao katika uhalifu mkubwa huo, ni hafifu na hazikupoteza maisha ya mtu.

    Vitendo kama hivi, vya kushambuliwa misafara ya viongozi, tumeviona huko Pakistan, ambapo matokeo yake baadaye, vimetufanya kumpoteza kiongozi shupavu wa watetea wanyonge Mwana Mama Benazir Bhutto, kwa kuuliwa na wahalifu kama hawa. Katika hali ya namna hii, kwa nchi yetu Tanzania, ni kuhatarisha Amani na Utulivu wetu, tuliojijengea tangu kupatikana kwa Uhuru wa nchi yetu.

    Pia, ni aibu na unafiki mkubwa mbele ya umma, kwa kiongozi yeyote kuvitumia vitendo vya uhalifu huo wa Mbeya, ili kujinufaisha na kujitafutia umaarufu wa kisiasa, badala ya kukemea uhalifu huo kwa nguvu zote.

    Kwa miaka mingi, Watanzania, tunapotokewa na tendo baya lihusulo nchi yetu Tanzania, tumekuwa tukiweka pembeni itikadi zetu za kisiasa na dini. Tumekuwa tukishirikiana na kuwa na mshikamano mkubwa, katika kuilinda Amani na Utulivu wa nchi yetu Tanzania.

    Je, utamaduni wetu huo umepotelea wapi siku hizi? Kwa maoni yangu mimi naona kuwa, viongozi wengi wa serikali na vyama vya siasa Tanzania, baada ya kifo cha Baba Wa Taifa (Mwl. Nyerere – RIP), wametawaliwa na tamaa, ubinafsi na ulafi wa madaraka kila upande.

    Ndiyo maana, kila mmoja, serikalini na viongozi wa vyama vyote vya siasa Tanzania, wanajitahidi kutumia njia chafu na hata kupindisha ukweli wa kitendo kibaya kama hiki cha kushambuliwa kiongozi wa nchi yetu, kionekane kuwa ni cha kisiasa, cha watu wachache, wahuni na walevi.

    Ni kweli, kuna watu wengine hutumia balaa kama hili, katika kujinufaisha kisiasa kwa kuyatumia matatizo ya kiuchumi ambayo nchi yetu, na nchi zingine duniani zimeathirika. Ni mimi na wewe tunaotakiwa kuwa macho na watu hao.

    Nawaomba Walinzi wa Rais wetu sasa waelewe kuwa nchi yetu imeingiliwa na watu wabaya, kutoka ndani ya nchi yetu, na nje ya Tanzania. Wasiwe na simile katika kuwashughulikia papo hapo watu aina hii wanapowaona na hali ya ajabu ajabu, kabla ya wao kutimiza nia zao wanazokusudia kuzifanya.

    Washambulizi hawa, kama wangemfanyia Rais wa Marekani, kama sio kuuliwa hapo hapo, wangesoteshwa Quantanamo Bay miaka kibao bila kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kujielezaa au kujitetea. Walinzi wa Rais wetu, tumieni utaalamu wenu mlioupata katika kazi yenu. Kwa hali ilivyo Tanzania sasa, ni rahisi maadui wa nchi yetu na maadui wa viongozi wetu, kujipenyeza na kuwatumia watu wetu ama wao wenyewe kujifanya Watanzania ili kutimiza nia zao mbaya. Kwa hiyo Bw. Nassor Jangwa, jaribu kulielewa hili.

    This Is Black=Blackmannen

  45. binti-mzuri Says:

    nassor yani wewe umenichekesha,lol!,bc oyee.. yani we unataka waigize jK ana’popolewa’ mawe?loool kakanguu wewe,unapotea hapo

  46. Jamani jifunzeni kiingereza,inasikitisha kusoma watu munaandika kiswanglish kabisa hata hakina sense mfano good to saw you ze comedy again!munaaibisha wengine jamani

  47. Harisa Says:

    mimi nawafagilia sana the ORIGINAL COMEDY!!!!!!! kazeni buti hao juu wanajifanya eti hamna mpya ni wazushi tu kwani mengi nani? tena mmefanya vizuri sana kuondoka wakati mpo kwenye chat, hao wanaosema eti mtarudi kwa vilio kwa mengi hawamjui waulizeni wafanyakazi wa IPP wanavyopewa mishahara midogo na mambo kibaoo! BOY’ZZZ keep it uppp!!! my bro’s ndiyo ajira hiyo

  48. mshauri Says:

    SIDHANI KAMA KUNA HAJA YA ORIGINAL COMEDY KUTOA KICHEKESHO ETI CHA MSAFARA WA RAIS KUPIGWA MAWE! JE, HICHO KITENDO KINAFURAHISHA? HATA KAMA KUNA MAKOSA YA RAIS JK NAFIKIRI NJIA YA KUMREKEBISHA SI KWA KUUPIGA MSAFARA WAKE MAWE. NI UAMUZI WA KIJINGA NA SI WA BUSARA HATA KIDOGO. KWA HIYO HAKUKUWA NA HAJA YA OC KUTUMIA UOVU HUO KUWACHEKESHA WATU. NI HAYO TU!

  49. bosco Says:

    na wa pongeza kwa sana……..endeleeeni kufanya mambo

  50. Amani kwako Blackmanne! Ni kweli maandishi yangu yanaonekana kama ni ushabiki kwa kitendo kilichofanyika lakini la hasha! Sikumaanisha hivyo! “im sorry 4 that!” nilichotaka haswa jamaa walieke hewani na kulizungumzia swala lile ktk mtazamo wao kama ze commedy! Mara nyingi wamejitahidi kuonesha matukio kama lile la kiongozi wetu kwa mfano kule mara ktk ule uchaguzi ulioleta athari kubwa za kujeruhiwa kwa baadhi ya wananchi au kiongozi Bwana Komba na wengine wengi sio tu kuburudisha lakini kuelimisha au kukosoa kwa mtazamo wao! shukrani sana!


Leave a reply to bdo Cancel reply