BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TUMEHAMA/WE HAVE MOVED February, 24, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 9:00 PM

movedbc

Tumehamia katika makazi mapya.Kututembelea Bonyeza Hapa

We have moved to our brand new house.To visit us,please Click Here.

 

LIYUMBA AINGIA MITINI! February, 19, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 8:55 PM

Zimetanda habari za kushtua kidogo.Habari zinapasha kwamba mtuhumiwa Amatus Liyumba(pichani) ametoweka,hajulikani aliko na heka heka za kumsaka kwa udi na uvumba ndio zimeshaanza? Waliomdhamini wameshaanza kukiona cha moto.Ilikuwaje?Kaenda wapi?Ni kweli?Bonyeza hapa kujua zaidi.

 

HONGERA MR AND MRS MALUWE. February, 16, 2009

Filed under: Familia,Watangazaji — bongocelebrity @ 6:57 PM

maluwe

Majuzi wakati ulimwengu unasheherekea sikukuu ya wapendanao,mtangazaji maarufu nchini Tanzania,Michael Maluwe alihitimisha siku hiyo kwa kufunga ndoa na kipenzi chake Diana katika Kanisa Katoliki Parokia ya Msimbazi jijini Dar-es-salaam.

Pichani ni Michael na Diana wakati wa tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa Sunset uliopo Mbezi jijini Dar-es-salaam.BC inawatakia ndoa bora yenye Baraka na maelewano tele.

Picha hii ni kwa hisani ya Father Kidevu ambaye kama unamuhitaji kwa shughuli yako unaweza kumpata kupitia simu yake namba +255 755 373999.

 

SALAMU ZA FA KUTOKA COVENTRY

Filed under: Bongo Fleva,Burudani,Elimu na Maendeleo,Muziki — bongocelebrity @ 2:33 PM

fabc1

Hakuna ubishi kwamba kijana Hamis Mwinjuma au maarufu kama MwanaFalsafa(MwanaFA) ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao wamefanikiwa.MwanaFA amefanikiwa sio tu kufikisha ujumbe alioukusudia kwa jamii bali pia kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yake kupitia muziki.Miziki yake imekuwa ikiimbwa na watu wa rika mbalimbali.Hayo nayo ni mafanikio.

Pamoja na mafanikio ya kimuziki au kisanii aliyonayo MwanaFA,anabakia kuwa mfano wa kuigwa linapokuja suala zima la elimu,muziki na maisha.Hivi karibuni alithibitisha hilo pale alipoamua kurejea tena shule.Safari hii ameelekea nchini Uingereza.

Nini kinamsukuma kijana huyu katika nyanja ya elimu? Na je hivi karibuni alipoachia wimbo unaokwenda kwa jina “Msiache Kuongea” alikuwa anamjibu Inspekta Haruni?Anazungumziaje maisha ya nchini Uingereza?Fuatana nasi katika mahojiano haya mafupi na MwanaFA

BC: Pamoja na mafanikio mazuri katika muziki kule Bongo bado umeamua kurudi tena shule.Nini kinakusukuma?Hapo UK umeenda kusomea nini na katika chuo gani?

FA: Kuna mengi yanafanya nifanye nnachofanya.Lakini kubwa na la msingi zaidi ni kuwa na nguzo nyingine kwa ajili ya maisha ninayoishi(Plan B).Kama unavyojua muziki pamoja na kuwa unakwenda vizuri lakini hautabiriki sana.Ni ngumu kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja kwa angalau miaka 10 ijayo.

Na zaidi ni kuwa naona kama kuna muda mwingi kama msanii wa kibongo nakuwa naupoteza kwa kutofanya chochote baada ya kurekodi(ambayo sio kila siku),kufanya shows(mara nyingi huwa weekends),matangazo(mara chache kama una bahati) na interviews ambazo nazo sio kila siku.Kwa hiyo kwenye wiki kunakuwa na muda mwingi unaenda bure ambao nimeona ni vyema nikautumia kufanya kitu kitakachozalisha.
Hapa UK nasoma Msc Finance na nipo Coventry University.

BC: Una mpango gani na muziki kwa hivi sasa?Kama utaendeleza muziki na shule vilevile,lini labda wapenzi watarajie albamu yako mpya? (more…)

 

HAPPY VALENTINE’S DAY February, 14, 2009

Filed under: Sikukuu — bongocelebrity @ 10:03 AM

valentino

Leo ni siku ya wapendanao duniani au maarufu kama Valentine’s Day.Ni sikukuu ambayo zamani ilikuwa ya “kimagharibi” zaidi kabla ya kuenea ulimwenguni kote.Sina mengi sana zaidi ya kuwaambieni wasomaji na watembeleaji wote wa BC kwamba tunawapenda na tunawatakia sikukuu njema.Enjoy!

 

MANENO MANENO-DDC MLIMANI PARK February, 12, 2009

Filed under: Burudani,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:44 PM

sikinde

Katika medani ya soka nchini Tanzania,inaaminika kwamba kama wewe sio mshabiki wa Yanga(Watoto wa Jangwani) basi ni mshabiki wa Simba(Wekundu wa Msimbazi).Hivyo ndivyo ambavyo imekuwa tangu enzi na enzi.

Kwa upande wa muziki wa dansi,inaaminika kabisa kwamba kama wewe sio mnazi wa Sikinde basi ni wa Msondo.Utashi na ushindani uliopo katika muziki wa dansi ni sawa kabisa na ule uliokuwepo katika soka la bongo.

Haishangazi basi kusikia kwamba uvumi ulipoenea jijini Dar-es-salaam mapema wiki hii kwamba DDC Mlimani Park Orchestra imesambaratika,habari hiyo haikuwa nzuri hata kidogo kwa mashabiki wa muziki nchini Tanzania achilia mbali wanazi wa Sikinde.Hakuna ambaye alitaka kuamini kwamba inawezekana ikawepo Msondo bila Sikinde.

Lakini sio kweli kwamba Sikinde ndio imefikia tamati.Kilichotokea ni kwamba kumekuwepo hali ya kutoelewana katika mambo fulani fulani baina ya uongozi wa DDC(Shirika la Maendeleo la Dar-es-salaam) ambao ndio walikuwa wamiliki wa bendi hiyo na hivyo kuitwa “DDC Mlimani Park Orchestra).Matokeo yake ni kwamba bendi hiyo,kuanzia tarehe 1 Machi mwaka huu itaanza kujiendesha yenyewe bila usimamizi wala udhamini wa DDC.Na kuanzia hapo watajulikana kama Mlimani Park Orchestra. Kwa hiyo mashabiki wa muziki wa dansi,Sikinde bado ipo!

Naam baada ya ufafanuzi huo,leo ni mwanzo wa weekend.Hapa kwetu BC ni kama jadi.Ni wakati wa zilipendwa.Wiki hii kwa upande wangu binafsi imekuwa ngumu kidogo.Imekuwa na maudhi ya haja.Si unajua inavyokuwa pale unapomthamini mtu na kujaribu kumtendea kila aina ya wema unaoweza lakini yeye akakuona kama kinyesi tu?Inaudhi eenh?Basi hali hiyo ndiyo iliyonikumba.Ni vurumai za maisha ambazo kwa kweli huwa natamani zingekuwa na suluhisho la kudumu!

Bahati nzuri ni kwamba zipo nyimbo kama hii ya leo ya Maneno Maneno kutoka kwao wana Sikinde,ambayo inaweza kusaidia pindi joto la nyikani linapojiri.Hakuna haja ya maneno.Inafikia mahala lazima utulie na kumuachia Mola.Usikilize wimbo huu kwa makini lakini wakati huo huo usisahau “kujirusha”.Kibao hiki kitabakia kuwa mojawapo ya kumbukumbu nzuri za Sikinde wakiwa kama DDC Mlimani Park Orchestra.Tunawatakia kila la kheri katika safari yao mpya kama Mlimani Park Orchestra.Tunaamini kwamba Sikinde will always be Sikinde.Ciao


Picha ni kundi zima la wanamuziki wa Mlimani Park Orchestra kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar mapema wiki hii.Picha na John Bukuku.


 

MSIBA BOSTON,USA

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 1:27 PM
Tags:

Ndugu,Jamaa na Marafiki,

Tunapenda kuwajulisha ya kuwa Mzee Leonard NJ Merere ambaye pia ni baba mzazi wa ndugu zetu Naomi na Jacob[JJ] Merere wa Boston-Masachusetts amefariki dunia siku ya Jumanne [Feb 10th 2009] asubuhi hapa Boston,USA.

Marehemu alikuwa  na umri wa miaka 73, ameacha mjane,watoto watatu na wajukuu wanne.

Taratibu na mipango ya  kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Dar es salaam kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa watoto wake huko Boston-Masachusetts.

Kila mmoja wetu anaombwa kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha kusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi.

Gharama za kuhifadhi mwili,kusafirisha mwili,Jeneza pamoja na ticket ya atakaye kwenda pamoja na mwili ni dola elfu ishirini[$.20,000].

Ni mzigo mkubwa sana ambao kila mmoja wetu anombwa kusadia ili kukamilisha shughuli hii hasa ukizingatia ya kuwa kwa kadri mwili unavyokaa funeral-home ndio gharama zinavyozidi kuongezeka.

Mwili utasafirishwa punde zitakapopatikana fedha za kulipia gharama.

Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account ya wafiwa kama ifuatavyo:

NAOMI  MERERE

BANK OF AMERICA,

ROUTE NUMBER :011000138

ACCOUNT NUMBER:009441233628

Au kwa adress hii:

Jacob & Anna Merere

510 Skylinedrive suite # 11

Dracut,MA 01826.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao:

Jacob & Anna Merere [JJ]-978-726-2227 au 978-957-2153.

Naomi Merere-978-413-3722 au 978-632-9823.

Juma Malika-781-244-7353

Saimon Twalipo-978-423-1192

Pastor Abisalom Nasua-214-554-7381

Email-Adress:- RambiRambi@Yahoo.com

Tafadhali chukua muda kuwafariji wafiwa na kuwaombea

Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa kuwasaidia familia Merere !

Mbarikiwe,

Mch.Abisalum Nasua,

Jackson Mollel

Michango-Kwa Niaba ya Marafiki wa Familia ya Merere.


 

“SIJAOA”-REGINALD MENGI February, 11, 2009

Filed under: Magazeti,Mahusiano/Jamii — bongocelebrity @ 3:21 PM

mengi

Miongoni mwa habari za watu maarufu ambazo bila shaka zimegubika vichwa vya wengi wiki hii ni ile ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP,Reginald Mengi kukanusha taarifa za gazeti moja kwamba amefunga ndoa mpya na mwanamke mmoja wa jijini Dar-es-salaam(Lilian Kimaro) na kulaumu uandishi wa habari unaokwenda kinyume na misingi ya taaluma hiyo.Kwa habari zaidi unaweza kubonyeza hapa.

Pia unaweza kubonyeza hapa ili kuona baadhi ya maswali ambayo waandishi wa habari walimbana nayo Mengi lakini akakwepa kwa kigezo kwamba wakatafute wenyewe ukweli!

Photo/Venance Nestory

 

MAUNDA ZORRO February, 10, 2009

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 11:06 PM

maundabc

Anaitwa Maunda Zorro.Anatokea kwenye ile ile familia ya kina Zorro ambayo tunaweza kabisa kuiita “Music Family”.Tangu alipoingia rasmi kwenye fani ameshaachia nyimbo kadhaa ambazo sio tu zimeshika chati bali zimethibitisha kipaji alichonacho.Pamoja na uthibitisho wa kipaji,lipo swali ambalo bado sijalipatia majibu pamoja na kujaribu kulifanyia utafiti mara kadhaa;Hivi uimbaji(naongelea uimbaji mahiri ambao wengi tunaweza kukubaliana kwamba hapo sawa) ni kipaji mtu anazaliwa nacho au ni kitu ambacho yeyote anaweza kujifunza?Na mazingira anayokulia mtu yana mchango wa kiasi gani katika kipaji?

Miongoni mwa nyimbo hizo ni huu hapa unaokwenda kwa jina Nataka Niwe Wako


Photo/A.Mrisho.

 

ETI HUYU NI NANI? February, 9, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 8:27 PM

pres-kbc