BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NDOA HAINA DOA-INSPEKTA HARUNI October, 28, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 6:39 PM

Ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao hivi leo wanaweza kujiita “wakongwe”.Kwa miaka nenda rudi wamekuwepo katika “game”.Jina lake anaitwa Inspekta Haruni…jina la kisanii likiwa limelifunika jina lake halisi la.Tangu enzi za Gangwe Mob(pale alikuwa na mwenzake Luteni Kalama)

Hivi karibuni ametangaza kujitoa katika kundi la Wanaume Halisi lililo chini ya Sir Juma Nature.Lakini kabla ya kujitoa gumzo kuelekea upande wake lilikuwa kuhusu wimbo wake wa hivi karibuni uitwao Ndoa Haina Doa.

Wimbo huu ni majibu ya wazi kwenda kwa MwanaFA ambaye hivi karibuni umekuwa sio tu msemo maarufu bali “kisingizio” cha vijana wengi kuhusu ndoa au mahusiano ya kudumu.Wimbo wa MwanaFA unaitwa Bado Nipo Nipo akiwa amemshirikisha mrembo Flaviana Matata katika kiitikio(chorus).Unaweza kuusikiliza wimbo wa MwanaFA kwa kubonyeza hapa na kisha kuusikiliza wimbo wa Ndoa Haina Doa kwa kubonyeza player hapo chini.



 

40 Responses to “NDOA HAINA DOA-INSPEKTA HARUNI”

  1. binti-mzuri Says:

    huyu bwana mie nilikua nammind,ila siku izi cjui vipi vipi yani! mara kamjibu ‘hamna mwaka wa shetani’ wanaume family,saivi naona kamjibu mwanafa.huyu huyu akaimba bolingo and rnb huyu huyu saivi anafoka foka … mzee vp?tujibu basi!mana unayuyumba kama nyumba ya ufinyanzi

  2. nchekube Says:

    mmmmmmmmmhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!, huko mjini kazi ipo.

  3. kahindi Says:

    Anaitwa babu kisanii…namfagilia sana,haswa ule wimbo wake uitwao asali wa moyo…..wewe ndiye asali wangu wa moyo rafiki na faraja yangu kaza moyo….babu uko juu m2 wangu…aminiaaaaaaaaaaaaaaa

  4. Mama wa Kichagga Says:

    Harun,

    Safi san kwa kurekebisha upupu. Mtu ataamuaje kudai jamii yote haifai?

    Asante sana tena sana kwa kusafisha na kukuza hadhi za kinamama.

    Asiyependa kitu jua hana na hajui uzuri wake.

    Nyimbo yako ina maana na itadumu. Hongera sana na endelea kutupatia nyimbo zenye kuheshimu jinsia zote na zenye kukuza hadhi na kuitunza jamii.

  5. Ed Says:

    Inspector huyo bwana, kwanza alitoka na watoto wa geti kali wa aina mbali mbali, kisha akatoka na Nasma. Huyu jamaa i think ana fit kwenye mipasho.
    Tanzania bongo flava bado sana, we have many years to crunch international standards.
    Few days niliona mtoto mmoja hapa kijichora tatu like hardcore, reason eti na yeye ni MC. Muulize DMX kama umc unalipa wakati uko kwenye 40s au 50s. Hii ni short term career. I think mwana FA know that, thats why he hedge through academics.

  6. solange Says:

    huyu bwana mie simuelewagi kabisaaaa, taarabu zingekufaa sana, huumizi kichwa kutunga za unasubiri kujibu za wenzaki, mhh sasa kujitoa tena huko na uliingia kwa siupidi 120,haya bwana kama ulivyosema wewe mambo ya maslahi.

  7. sellanda Says:

    huyu nae akaimbe mipasho tu anasubiri watu wajenge daraja yeye apite kiulaini.

  8. KT Says:

    Inspector Haroun nakuunga mkono kwa kujibu wimbo wa mwana FA, hilo ni jambo la kawaida katika sanaa pale unapoona wewe kama msanii mtu mwingine anapotosha jamii. Na pia mimi ni mmoja kati ya mashabiki wako wakubwa especially style yako ya kughani inanifurahisha sana, nikikumbuka enzi za Gangwe nyimbo kama ‘Ngangari Kinona’, Mtoto wa Get Kali n.k.Lakini mzee kwa kitendo chako cha kujitoa Wanaume Halisi ni wazi umepoteza mwelekeo sasa. Nikicheki namna Gangwe ilivyosambaratika haina tofauti na jinsi ambavyo umechomoka Wanaume Halisi. Unatuambia kuwa umeona kuwa ndani ya kundi unakosa nafasi ya kufanya mambo yako ya sanaa zaidi..huu ni UBINAFSI. Ni UBINAFSI huo huo uliokufanya kipindi kile ukawa unatoa nyimbo mwenyewe bila kumshirikisha Luteni Kalama mpaka Luteni akaona haina maana ya kuwa kwenye kundi. Na nikiangalia kitendo cha wewe kujitoa Wanaume na kujibu wimbo wa Temba wa Mwaka wa shetani naona kama unajikanganya mwenyewe na inadhihirisha unafiki wako ulivyo..hufai kuwa katika kundi lolote, wewe kwa jinsi ulivo inabidi ubakie solo artist…sio mtajiunga kwenye kundi mnatupa midadi washabiki wenu halafu mara ghafla hata bado hamjafanya kitu cha maana mnasambaratika…umeniboa sana BABU.

  9. PETER MAGANGA Says:

    babu uko juu sana mimi nakukubali sana mkubwa,endelea kukamulisha watu na kujitoa kwako kiumeni ni hatua nzuri maana mustakabali wa kundi hilo sasa hivi hawaeleweki cjui ndo mwaka wa shetani? mimi cjui nakutakia mafanikio kwa sana tu

  10. Nangali Nangali Says:

    babu uko juu sana tena matawi ya mkaratusi

  11. Matty Says:

    me too namuona kakaa kimipasho mipasho!!!!!!!!!!!!!

  12. gisela Says:

    mdau wa kwanza’binti-mzuri’ mbona kanye west ana rap na kuimba?

  13. Matty Says:

    Heeee wadau BC kardui kwa kasi naona duuu maoni ya leo leo haya au???safi sana lakini!

  14. majita Says:

    Haya tukimaliza comments zoote tumshikie bango Edwin Ndaki na tumuulize “KAKA EDO UTAOA LINI?” nasubiri jibu Ndaki

  15. Goal Getter Says:

    Hana lolote huyu mtu kazi yake ni kujibu nyimbo za wenzie eti umemgusa huu wimbo wa Mwana Fa mbona hakuwa na wazo la kutunga wimbo kusifia hiyo ndoa kabla anasubiri wenzie waumize kichwa then yeye atumie kujibu nyimbo hizo kama ngazi kupanda juu, nawaunga mkono Sellanda,Ed kwa maoni yao. Mama wa Kichagga hujui maudhui ya wimbo wa Mwana Fa nakushauri ukaurudie kuusikiliza tena huu wimbo wa Fa, halafu ndio ucomment pia jifunze kiswahili, eti “Asiyependa kitu jua hana na hajui uzuri wake” ilitakiwa uandike “Asiyependa kitu elewa/tambua kuwa hana na hajui uzuri wake” Kiswahili siyo MBEGE jifunze kiswahili au ungeandika kwa kichagga tungetafuta mkalimani hapa hapa BC.

  16. Goal Getter Says:

    Nakushauri ukaimbe taarabu Babu Haroun mwenzako Hammer Q anapeta kama kawaida pia ukitaka ushauri zaidi wa fani hii yupo Mzee Yussufu hana hiyana katika kukupa ushauri au mama lao Hadija kopa hana choyo pia, Ukishindwa nenda Zanzibar au Lamu kama siyo Tanga kwani huko ndiko jikoni kwenye mapishi ya kweli ya muziki wa mwambao wa taarabu kwani mashairi ya majibizano unaonekana unayamudu, BIG UP MWANA FA wewe ndio kichwa kwani tungo zako zinafikisha ujumbe kwa jamii keep it up bro!

  17. Matty Says:

    hahahahahaha Majita na wewe unaoa lini?????au bado upo upo kwanza????????????ur so fun guy nimevunjika mbavu lakini!

  18. Hombiz Says:

    MwanaFA kuumbua wanawake wasiojiheshimu “vicheche” hajakosea. Na Inspecta Haruni kutetea wanawake wanaojiheshimu na wanaoheshimu ndoa zao naye hajakosea pia.
    MwanaFA kusema ukimegewa demu wako nawe tafuta mnyoge ummegee, hapo kachemsha. Hayo siyo maadili. Nionavyo mimi, ukimegewa demu wako, mteme, kama wewe ni safi.
    Wakati huo huo, kuoa sio fashion. Hiyo inatakiwa kuwa ni life time commitment. Hivyo basi, huwezi kuingia kwenye ndoa kichwa kichwa. Ni wajibu wa wanandoa wote kupendana, kuheshimiana na kushirikiana kwenye shida na raha ktk ndoa. Mawasiliano hai ni lazima yawepo ili ndoa iweze kustawi. La sivyo kuna kuumia na kulia kilio cha mbwa mdomo juuuuu..wuu..wuu…wuuuuuuu!
    NB: Wanaume nasi ni vema tujifunze kupitia nyimbo hizi. Sio mwanamke tu anayeweza kuwa kicheche! Wanaume “womanizers” nao wapo wengi. Hawa nao wanatakiwa kubadili tabia zao na kuwa waadilifu kwa wapenzi wao na waache tabia ya kutamani na kutembea na wapenzi na wake za watu! Otherwise, mtajikuta mwisho wa siku mnaluka maji na kukanyaga moto!
    Wasanii tumieni Bongo flava kujenga na si kubomoa!
    Good luck to both artists

  19. EDWIN NDAKI Says:

    Majita Majita mi naona tuanze na wewe vipi bado upo upo nini?

    MAJITA mi msaidi wa Cardinal Pengo kazi yangu kufungisha tu ndoa..

    Ila naomba BC afanye mahojiano na Majita ……aaaaaaaaaa aaaaaa wasuuuuu

    KUHUSU BABU INSPECTOR..

    Ningeshangaa kuona anaendela kuwepo kundi ila sishangai kuona kajitoa..Temba alisema ..Gangwe mob hawajapatana kiana wanajifanya wapo pamoja.

    Nasikia Inspector anampangowa kujinga na Zanzibar Morden Taarab.. Habari ndiyo hiyo

  20. binti-mzuri Says:

    gisella please dont compare inspector haroun na kanye west, wako viwango tofauti japo both wanajitahidi kufanya wayafanyayo kwa viwango vyao.. but they are in total different levels!

  21. halima Says:

    Hombiz big up kwa kutoa maelezo yasiyofungamana na upande wowote. inspector na wewe umezidi kuhangaika kama kuku kakosa banda mmmhhhhh

  22. star Says:

    Huyu kijana aende shule jamani hii miziki bila shule ni upotezaji wa muda na nguvu…

    na usikuse muziki ya Bongo halipi kabisa…kijana nenda shule..

  23. star Says:

    Ed: comment yako ya 5. ni ya maendeleo sana keep it up…

  24. mtu Says:

    mi naona babu yuko makini sana, kwani amewatetea kina dada ambao mwana fa, amewapaka choo kinoma, ukweli ni kwamba uzinzi tunaufanya iweje mwana, awalaumu wanawake tu. Hii inaonyesha kasumba ya jamii yetu iliyokithiri ya kukandamiza mwanamke. Inabidi tubadilike msikilizeni babu vizuri, nyimbo imejaa elimu, maisha, mawaidha nk.

  25. mtu Says:

    “siyo mabinti peke yao, kila kiumbe ni dhaifu”, “BINADAMU HAWATIMII, WAPO WANAOFANYA MAOVU, NA WAPO WAAMINIFU”, “Haujui tamu ya ndoa, usiwape mabinti doa”, “Ukiuza ukwezi, basi utakula dafu”, “Chaguo lako kuishi msela” sasa iweje uwapake wanawake? “aliyezoea uzinzi, kwake ndoa ni lawama”, “huhisi ndoa itambana”. Mi sitaki kusema sana kwani nyimbo hii haihitaji mganga wa kienyeji ili kuielewa, na nina imani kinadada popote wanapo isikiliza nyimbo hii basi wanafarijika. wanawake hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeee

  26. mtu Says:

    “demu wako akikuita boyfriend haimanishi uko peke yako”, je boyfriend wako akikuita darling, inamaanisha uko peke yako?, “Usiseme unamwamini mwanamke, hata kama unamtania”, jamani sijui kama ni mimi tu, ninayeona kama mwana fa, (yule aliyeimba mimi na binti damdam,) leo mabinti wamempa mafanikio kwa kununua muziki wake, sasa anawavua nguo hadharani hata mama zake. we mwana fa, hebu rudia maadili yako. Mama zetu wanastahili heshma bwana.

  27. mtu Says:

    We binti mzuri, unajua kuwa uzuri wa binti ni tabia?, na je unajua kama tabia ni ufahamu wa ulimwengu dunia, pamoja na kujifahamu wewe mwenyewe kama mwanamke?. Sasa huo utafauti wa levels za Kanye na Babu zipi? wote wanafanya muziki sawa, kuimba na kurap. Au unalinganisha level ya Marekani na Tanzania? Tunamsikiliza Kanye bongo kwasababu Marekani wametawala tamaduni za dunia, lakini siyo eti wao wanaujumbe kutoka mbinguni, lahasha bali ujumbe wa maisha yao ya kila siku, kama tu ilivyo babu na mwana fa, na maisha yetu ya kibongo. kuwa binti ehhh, teeh teeh

  28. mtu Says:

    Goal getter? Hivi wewe ni mwalimu wa kiswahili anzisha tuition basi utufundishe kiswahili? Goal getter? hivi nini maana ya jina lako? mi natafsiri, wewe ni mmoja kati ya ‘wa ukimegewa demu wako na wewe tafuta demu wa mnyonge ummegee au?. Swali lako kwa mama wa kichaga naomba likurudie, je maudhui ya wimbo wa mwana fa umeyaelewa, au bado upoupo tu? Nyimbo nzima ya mwana, ni ya kuburudisha tena utunzi ulikuwa ‘influenced na ulevi’, “usimwamini mwanamke hata kama unamtania”, “ngoja nzeeke zeeke kwanza halafu ndo mniulize ntaoa lini?” we unafikiri kuna shule hapo? Nyimbo ya babu, inafundisha na kuelimisha, “kila binadamu ni dhaifu” YAANI WANAWAKE NA WANAUME, NA SIYO WANAWAKE TU NDO DHAIFU. Big up mama wa kichaga!!!

  29. binti-mzuri Says:

    ‘mtu’ umetumwa na babu haruni mwenyewe nini,mbona umevamia watu ghafla. anyways, what i meant with that comment ni kwamba those two musicians are different. hata prof jay na inspecta pia wako different,even though they both rap bongoflava, they are in total different levels. ni kama kuwa na wanafunzi wawili darasani,wote wanasoma masomo sawa,ila wako katika level tofauti kimaendeleo.

    inspecta yupo succesful,but not as succesful as kanye west. its as simple as that! tukatae tukubali. ishu sio kua marekani,hapa dar yenyewe kabeba awards ngapi, pale kilimanjaro awards? muziki wake bomba,ila naona kama sometimes hana sense of direction. he should stick to something. au ahamie taarabu kama kaka ED alivoshauri!

  30. halima Says:

    duhhhhh kazi kweli kweli

  31. KBC Says:

    BABU na FA wote wanangu..Both Songs are Good..kila moja inakupa Mtazamo ya Watu wengi ktk jamii yetu..KUJIBU HOJA sio KOSA kama una VIGEZO VYA MSINGI..inaMaanisha Jamii inasikiliza kila kinachosemwa na Wasanii..Sio kwamba HAROOUN hawezi kutunga nyimbo..His Body of work speak for its self..FA mwenyewe anatambua..na wala Hii sio BEEF..Jus Different Opinion..Actually now that there is NDOA HAINA DOA..watu wanaisikiliza BADO NIPO NIPO zaidi..na kuzichambua zote mbili..BIG UP BABU+FA..Keep ON!!

  32. Ebwana sio siri Mwana FA mimi binafsi miaka yote toka nianze kufuatilia nyimbo zake nilishamkubali siku nyingi kwamba yeye ni mwanafalsafa kweli kwasababu maudhui ya nyimbo zake kweli ni zenye kubeba ujumbe wenye hekima haswa! Lakini hii track imenishangaza sana na sitaki kuamini kama kweli mashairi yake yaliandikwa na yeye mwana~FA! Kiukweli huyu Inspector Haroun simlaumu hata kidogo alichokifanya ndicho kinachotakiwa ktk jamii wewe kama mwana fasihi wa kweli huwezi kufumbia macho upotofu unaofundishwa ktl mashairi ya wimbo huu! Fuatilia mistari halafu utagundua kwa mashairi yanatushawishi kupotoka kiimani juu ya mahusiano na tunaambiwa mpenzi wako akienda nje na wewe ufanye hivyohivyo kujenga heshima jamani inakubalika kweli hii? Haikubaliki popote ktk imani zote tulipinge ili awe makini next time aje na track zenye akili!

  33. mtu Says:

    Binti mzuri, ujue jina lako lina maana nzito sana, usiwe na hasira kwani ‘patience’ ni sehemu ya uzuri. Naomba uelewe kuwa Mimi simtetei Babu, na wala hajanituma bali natetea hoja za Babu, Halafu kutetea hoja sio lazima wewe uwe umefungamana na hoja hiyo, naimani hata wewe una msupport tu Mwana japo hukubaliani na hoja zake za “usimwambie mwanamke unamwamini hata kama una mtania”. Binti mzuri inahitaji mtu kutoa hoja ili wengine wajibu, na tunapojibu siokama tumetumwa na watu, bali ndivyo jamii inavyoelimshwa.

  34. mtu Says:

    Muheshimiwa Nassir naona hapo tuko kwenye boat moja, mimi nilimekuwa mpenzi wa tungo za Mwana kwa muda mrefu, kijana ana akili, ametulia na anajua kughani. Ila siyo ajabu kwa alilolifanya, kwani wahenga husema mgema ukimsifia, tembo……….., Sikuhizi Mwana amekuwa dictator, kwani anatoa hoja ya kuburudisha jamii, ambayo ni potofu halafu anafunga mabano ya mjadala anaposema “hamuwezi kuwa hamjalewa”. Yaani tukitaka kumshauri akomae katika ndoa, au azibe masikio, basi tumelewa. Yaani tukae kimya wakati yeye anawadhalilisha wanawake na kupotosha jamii?
    Dogo mwana rudi kwenye mstari, kwani walio kufikisha hapo ulipo ni wanawake kwani ndio walikuwa mashabiki wako wakubwa.

  35. mtu Says:

    Hombiz unadarubini kali wewe, tuko pamoja, Big up!!

  36. Bob Sambeke Says:

    Babu Unatisha We Komaa,Nadhani hawakujui wanaukudis na kukwambia umekwisha na uimbe taharabu! Wangejue wacngethubutu kukudiss….Kwani Wanaokula kuku bangi nawajua Ooh,Endeleza Libeneke Inspector ur da bomb…..Ona Mtoto wa Geti Kali,Ngangali,Binti kisura,Heka heka za ticha,Asali wa moyo,nje ndani,Wape vidonge nk..Bado tu hamja mkubali tu kwamba jamma anatisha ebu wadau mtoe props za kutosha kwa msela na co dis wakati mnajua jamaa yupo juu…

  37. nunku Says:

    nionavyo mm fasihi hukamilishwa na pande2 ambazo uwepo wazo huiamsha jamii na kuikumbusha ilipo,majibizano ya FA na BABU si ndo uhalisi wa fasihi yenyewe? mi naona acheni kulumbana ila julishaneni makubwa yaliyo ktk pande hizo mbili.
    msinihukumu kwa maoni yangu kwani cwakatazi kudis,ila mngekuwa nyie mnadisiwa kwenye kazi zenu mngejisikia vp?kitu kikikuboa unaachana nacho kuna wengine wanakihitaji. hapa ni mahala pa comment sio dis mmeelewa?
    mnatuboa na madis yenu.

  38. buddaboo Says:

    mtu.
    mwisho wa siku tunataka mziki mzuri.ukiskiliza vizuri hizi nyimbo zote mbili bila kuwa na upande utagundua ya MwanaFA ipo kisanii zaidi kuliko ya Inspector.ni kweli MwanaFA amesema vitu vingine huwezi kuvichukua,lakini siku zote kwenye mziki vitu vingi vinasemwa,pengine kuvutia usikilizaji ama kufurahisha,hasa kwenye rap..sikiliza wasanii wote wazuri duniani..na wakati mwingine ni maoni yake binafsi.ilikuwa haki ya Inspector kujibu,ndio fasihi ilivyo,lakini sitaki kuamini unakubali kajibu sawasawa…hakujibu hoja,anaongea kitu kingine kabisa.FA anaelezea sababu zake kwa nini hataki kuoa,yeye amekomaa kwenye kusema FA amedhalilisha wanandoa na ye ni mwanandoa ndo maana ameamua kujibu.wapi amedhalilishwa mwanandoa mle?mbona asijibu ule wa Bushoke mume bwege basi tujue anatetea ndoa yake kuwa mbona wengine wanaoa na sio mabwege??ingefaa angejibu binti labda nae aseme kwa nini hataki kuolewa tungemuelewa,uwanja upo wazi..Inspector?
    jinsi breakdown ya FA ilivyokuwa,ilikuwa inajengwa na facts tupu…alisema mambo mengi yanayotokea kweli mtaani.mtu unanukuu tu mistari inayomshambulia,mbona hunukuu ‘watu na akili zao washajichuuza na wakalia’,’alilala na bibi arusi siku 1 kabla…..”napata wakati mgumu washkaji wanapolia kwa uchungu kwni mi nna maumivu yangu nasema tu na moyo wangu’,’sikatazi watu kuoa na hata nikiwakataza neno langu sio sheria’..’staki kuoa sababu staki kulia najipanga nisiharibu staki mje kunihurumia’ and so on and so forth..how can u dare linganisha hizo nyimbo mbili?sana sana Inspector ameonyesha tu mwisho wa uwezo wake wa kufikiri kwa kuingilia mlango wa kutokea.angalia mwisho wa siku who’s atleast making money kwenye hizo nyimbo kati yao wawili..kama una urafiki na Inspector mwambie ajipange afanye mziki.sishangai FA anavyogoma kuongelea wimbo wa ‘babu’ yake huyo.

  39. Simba Dume Says:

    buddaboo nimefurahi kwa maelezo yako kwani umeweka wazi kabisa ukweli wa mambo kuhusu tofauti zilizopo kati ya nyimbo hizi mbili. ninaungana nawe kuwa wimbo wa MwanaFA unamaudhui tofauti na ambavyo Inspekta Haroun alivyoutafsiri. ukifuatilia historia ya muziki ya wanamuziki hawa wawili utaona ukweli kuwa Inspekta amekuwa katika fani muda mrefu sana kuliko MwanaFA. MwanaFA amepata mafanikio sana kuliko Inspekta katika fani nk. Mbali ya kufanya vizuri katika fani MwanaFA alikwenda shule wakati tayari yuko juu kwenye fani, jambo ambalo linahitaji mtu makini kuweza kufanya hivyo hususan pale unapokuwa juu.
    Ukiangalia historia ya Inspekta ni problem tu, kila anakokwenda hawezi kukaa na wenzie, inawezekana ana “roho ya kwanini” hataki mtu mwingine apate, ila yeye, hataki kuamini kuwa MwanaFA yuko juu, hataki kuamini kuwa Mh. Temba ni zaidi yake…sasa haya kama hajayang’amua yatamtesa sana.
    Ninamshauri kuwa awe mbunifu iliaweze kujenga utambulisho wake ambao utakuwa endelevu na hatimaye kumpatia tija.
    Mimi binafsi hadi leo ninausikiliza wimbo wa MwanaFA kila siku kwani upo katika No. 1 kwenye chati yangu ya nyimbo za bongo. Wimbo wa imspekta nimeupiga chini kwa maana hajafanya kazi ya kuumiza kichwa, alichofanya ni kama ku-copy kazi ya msanii mwingine.
    MwanaFA, huna haja ya kujibu any part ya wimbo wa Inspekta ninakuamini kama Mwanazuoni wa Falsafa, kiuwezo wa kufikiri uko ahead of him by far. ‘Aige na hii’


Leave a reply to star Cancel reply