Kabla ya makundi ya muziki kama vile Wanaume TMK,Das Nundaz,Nako2Nako,East Coast na mengineyo kuibuka au hata kutambulika kwenye anga za muziki nchini Tanzania yalikuwepo makundi ambayo hivi leo wengi tunakubaliana kwamba hao ndio waanzilishi wa kinachoonekana hivi leo kuwa kama vuguvugu la vijana katika kupigania haki yao ya msingi ya kujielezea(freedom of expression) katika jamii kupitia sanaa ya muziki.
Miongoni mwa makundi hayo ni lile lililotamba sana na kujulikana kama Kwanza Unit.Miongoni mwa wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo ni KBC au KSingo(pichani) kama alivyojulikana wakati ule na hata hivi sasa.Mbali na Kwanza Unit,wengi bado mtakuwa mnamkumbuka kama mpigania haki za Wana Hip Hop na pia miongoni mwa wanamuziki waliojitolea sana katika kuhakikisha kwamba Hip Hop ya Tanzania inaeleweka na kukubalika.Pia wengine mtamkumbuka kama DJ pale Clouds FM katika Dr.Beat.
Tukiwa bado katika kuhakikisha kwamba historia ya vuguvugu hilo na kwa ujumla historia nzima ya muziki tunaouita “wa kizazi kipya” hivi leo,haipotei na inawekwa vyema mtandaoni,hivi karibuni tulifanya mahojiano na KBC kama utakavyoyasoma hivi punde.
Je unakumbuka Kwanza Unit ilianzishwa mwaka gani?Nini yalikuwa malengo ya mwanzoni?Leo hii KBC akiangalia nyuma anaona tofauti gani au maendeleo ya aina gani katika muziki wa kizazi kipya?Nini ushauri wake kuhusu masuala ya haki miliki na utawala wa biashara ya muziki?Kwa maoni yake,nani anachangia kudidimiza muziki?Ni producer au Radio DJ?
Ili kupata majibu ya maswali hayo na mengineyo mengi,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo ambayo pia yana Swanglish ya aina yake katika kuleta au kuchanganya ladha kiaina; (more…)
Recent Comments