BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“SIJAOA”-REGINALD MENGI February, 11, 2009

Filed under: Magazeti,Mahusiano/Jamii — bongocelebrity @ 3:21 PM

mengi

Miongoni mwa habari za watu maarufu ambazo bila shaka zimegubika vichwa vya wengi wiki hii ni ile ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP,Reginald Mengi kukanusha taarifa za gazeti moja kwamba amefunga ndoa mpya na mwanamke mmoja wa jijini Dar-es-salaam(Lilian Kimaro) na kulaumu uandishi wa habari unaokwenda kinyume na misingi ya taaluma hiyo.Kwa habari zaidi unaweza kubonyeza hapa.

Pia unaweza kubonyeza hapa ili kuona baadhi ya maswali ambayo waandishi wa habari walimbana nayo Mengi lakini akakwepa kwa kigezo kwamba wakatafute wenyewe ukweli!

Photo/Venance Nestory

Advertisements
 

MAUNDA ZORRO February, 10, 2009

Filed under: Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 11:06 PM

maundabc

Anaitwa Maunda Zorro.Anatokea kwenye ile ile familia ya kina Zorro ambayo tunaweza kabisa kuiita “Music Family”.Tangu alipoingia rasmi kwenye fani ameshaachia nyimbo kadhaa ambazo sio tu zimeshika chati bali zimethibitisha kipaji alichonacho.Pamoja na uthibitisho wa kipaji,lipo swali ambalo bado sijalipatia majibu pamoja na kujaribu kulifanyia utafiti mara kadhaa;Hivi uimbaji(naongelea uimbaji mahiri ambao wengi tunaweza kukubaliana kwamba hapo sawa) ni kipaji mtu anazaliwa nacho au ni kitu ambacho yeyote anaweza kujifunza?Na mazingira anayokulia mtu yana mchango wa kiasi gani katika kipaji?

Miongoni mwa nyimbo hizo ni huu hapa unaokwenda kwa jina Nataka Niwe Wako


Photo/A.Mrisho.

 

ETI HUYU NI NANI? February, 9, 2009

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 8:27 PM

pres-kbc

 

JK AKIAGA SHINYANGA February, 8, 2009

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 2:11 PM

jk-shybcKwa heri kaka…uje tena!

jkshy2bc

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na baadhi ya wakazi wa mji wa shinyanga muda mfupi baada ya kuwahutubia katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa michezo wa Kambarage mjini humo jana.Rais Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete tayari wamerejea jijini Dar es Salaam(picha na Freddy Maro)

 

MASIMANGO-MBARAKA MWINSHEHE February, 5, 2009

Filed under: Burudani,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 9:32 PM

masimangoNahisi ni kama juzi tu tulikuwa tunaongelea sikukuu za xmas na kisha mwaka mpya.Ile kutahamaki,mwezi wa kwanza ulishaisha na wa pili ndio unaelekea katikati.Ukizingatia kwamba huu ni mwezi mfupi kuliko yote,utagundua kwamba siku zaenda yakhe!Tayari mbio za kutimiza malengo ya mwaka huu zishaanza kushika kasi.Kazi kwelikweli.

Ni mwaka mgumu.Ni mwaka ambao unanukia kila hali ya uchumi ulioyumba.Wachumi na wanasiasa wanakiri.Kama mpaka leo hujapoteza kazi yako basi unamshukuru aliye juu na huna budi kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili “panga” likipita basi uwe salama.Joto hili la uchumi likija kukolea na huku kwetu ambapo bajeti zetu zinakuwa sio bajeti bila wahisani,nahisi itakuwa patashika nguo kuchanika.Mola atuepushe maana bila hivyo…dah!

Ukosefu wa kazi ni chanzo cha umasikini.Ni chanzo cha manyanyaso.Ukiwa huna chako,ni rahisi sana kunyanyaswa hapa duniani.Watakupa na kisha kukusemea pembeni.Wakikuona unaelekea upande walipo,wengine wanaweza hata kutoka mbio kabisa.Watakupa majina.Utaitwa “Kikosi cha Mizinga”.Ukiingia baa utaona jinsi watu wanavyokaa kimya kama sio kwenda maliwatoni kwa dharura.Usishangae mialiko ikawa inakupita.Mkono mtupu haulambwi.

Visa kama hivyo ndivyo vilivyomfanya Mbaraka Mwinshehe aimbe wimbo wake maarufu wa Masimango.Usikilize hapo chini na kisha unipe tafakari yako.Je unadhani uamuzi wa Mbaraka wa kuondoka kwa sababu ya masimango ni sahihi?Ungekuwa wewe ungefanyaje?Je imeshawahi kukutokea?Ilikuwaje?Nakutakia wikiendi Njema.Pata Burudani.


 

MPOTO ASAKA NAULI YA KWENDA IKULU February, 4, 2009

Filed under: Burudani,Mahusiano/Jamii,Mawazo/Tafakuri,Sanaa/Maonyesho,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 8:00 PM

mrishompotobc

UMAHIRI wa Mrisho Mpoto umekuwa ukiwakuna wengi hasa anapokuwa jukwaani akidondosha mashairi yake na mwaka jana alifanikiwa kushinda moja ya tuzo kubwa katika sanaa kwa Afrika ijulikanayo kama Slam, ambayo ilikuwa inashikiliwa na mmoja wa wasanii mahiri aitwaye, Steff H2K kutoka Mauritius.

Ushindi wa Mpoto umemfanya apate nafasi ya kushiriki fainali za tuzo za Slam za dunia, ambazo zinafanyika nchini Ufaransa Machi, mwaka huu lakini hiyo haitoshi wala haimzuii yeye kuendelea kusaka nauli ya kwenda Ikulu.

Baada ya kuwa ameshiriki katika wimbo wa ‘Salamu Zangu’ na kuweza kuchukua nafasi kubwa huku akimfunika mmliki wa wimbo huo Irene Sanga, Mpoto ameamua kuibukia upande wa pili na kutoa wimbo wa ‘Nikipata Nauli’.

[Usikilize wimbo “Nikipata Nauli” kwa kubonyeza player hapo chini kisha ndio uendelee kusoma makala hii hapo chini]JM

(more…)

 

NINI KILIMLIZA WAZIRI MKUU? February, 2, 2009

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar,Uandishi — bongocelebrity @ 8:51 PM

pindabcWiki iliyopita kuna kitu cha nadra kidogo kilitokea nchini Tanzania.Ni kitendo cha Waziri Mkuu,Mizengo Pinda,kububujikwa na machozi bungeni.Baada ya hapo kumezuka mijadala mbalimbali likiwemo swali ambalo kimsingi sio rahisi sana kulijibu.Swali ni kama linavyoonekana katika kichwa cha habari hapo juu;Nini kilimliza Waziri Mkuu?

Sambamba na swali hilo,wapo watu lukuki,akiwemo Ansbert Ngurumo,wanaouliza msururu wa maswali ya msingi;Je Waziri Mkuu aliwalilia albino?Je aliililia serikali?Je alijililia mwenyewe?Na Ndimara Tegambwage anajadili je Waziri Mkuu akilia ndio kumaanisha kwamba serikali nzima imelia?Wewe unasemaje?