BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“SIJAOA”-REGINALD MENGI February, 11, 2009

Filed under: Magazeti,Mahusiano/Jamii — bongocelebrity @ 3:21 PM

mengi

Miongoni mwa habari za watu maarufu ambazo bila shaka zimegubika vichwa vya wengi wiki hii ni ile ya Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP,Reginald Mengi kukanusha taarifa za gazeti moja kwamba amefunga ndoa mpya na mwanamke mmoja wa jijini Dar-es-salaam(Lilian Kimaro) na kulaumu uandishi wa habari unaokwenda kinyume na misingi ya taaluma hiyo.Kwa habari zaidi unaweza kubonyeza hapa.

Pia unaweza kubonyeza hapa ili kuona baadhi ya maswali ambayo waandishi wa habari walimbana nayo Mengi lakini akakwepa kwa kigezo kwamba wakatafute wenyewe ukweli!

Photo/Venance Nestory

Advertisements
 

MPOTO ASAKA NAULI YA KWENDA IKULU February, 4, 2009

Filed under: Burudani,Mahusiano/Jamii,Mawazo/Tafakuri,Sanaa/Maonyesho,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 8:00 PM

mrishompotobc

UMAHIRI wa Mrisho Mpoto umekuwa ukiwakuna wengi hasa anapokuwa jukwaani akidondosha mashairi yake na mwaka jana alifanikiwa kushinda moja ya tuzo kubwa katika sanaa kwa Afrika ijulikanayo kama Slam, ambayo ilikuwa inashikiliwa na mmoja wa wasanii mahiri aitwaye, Steff H2K kutoka Mauritius.

Ushindi wa Mpoto umemfanya apate nafasi ya kushiriki fainali za tuzo za Slam za dunia, ambazo zinafanyika nchini Ufaransa Machi, mwaka huu lakini hiyo haitoshi wala haimzuii yeye kuendelea kusaka nauli ya kwenda Ikulu.

Baada ya kuwa ameshiriki katika wimbo wa ‘Salamu Zangu’ na kuweza kuchukua nafasi kubwa huku akimfunika mmliki wa wimbo huo Irene Sanga, Mpoto ameamua kuibukia upande wa pili na kutoa wimbo wa ‘Nikipata Nauli’.

[Usikilize wimbo “Nikipata Nauli” kwa kubonyeza player hapo chini kisha ndio uendelee kusoma makala hii hapo chini]JM

(more…)

 

UNITY ENTERTAINMENT November, 11, 2008

Filed under: BC Investigative,Burudani,Mahusiano/Jamii,Muziki — bongocelebrity @ 7:54 PM
Tags: , ,

Hivi karibuni tulipotambulisha single mpya ya AY inayokwenda kwa jina Freeze, palitokea mabishano makali sana kuhusiana na kama ni kweli AY ni established artist ambaye ana mpaka ofisi yake inayohusiana na suala zima la burudani na muziki. Umuhimu wa elimu ya darasani (formal education) pia ulizua gumzo.Nadhani wote tunakubaliana kwamba elimu siku zote ni suala muhimu na lisilofaa kubezwa hata kidogo.Kama mtu ana nafasi na uwezo kusoma tunamshauri afanye hivyo!

Lakini pia kulikuwepo na maelezo tofauti tofauti kuhusiana na kuwepo au kutokuwepo kwa ofisi ya AY na sehemu ilipo.BC iliamua kuwatuma baadhi ya wanachama wakereketwa ili kujaribu kupata undani kidogo wa suala hili.Tuliamua kufanya hivi ili kuwapatieni ukweli baada ya kuona kuna maelezo mengi yanayopingana au kupishana.

Ukweli ni kwamba AY anamiliki kampuni inayokwenda kwa jina la Unity Entertainment Company Limited.Ipo Mikocheni kwa Nyerere,Rose Garden Road pale Jued Business Centre Wing B 2nd Floor. Kampuni hiyo inajishughulisha na Event Coordination and Organizing(kuandaa na kuratibu matukio) na pia ni Events Booking Agency.BC pia ilifanikiwa kupata picha kadhaa za ofisi hiyo kama unavyoziona hapo chini.

BC inapenda kumpongeza AY kwa ujasiriamali na umakini huu katika masuala ya muziki na burudani.Ni matumaini yetu kwamba wengine nao watafuata nyayo za AY.

unity1bc

Unity Ent.

unity2bc

Unity Tanzania

unity-entertainmentbc

 

BALOZI WA REDDS ARUDISHA TAJI August, 9, 2008

Filed under: Blogs,Mahusiano/Jamii,Miss Tanzania,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:13 PM

BALOZI wa REDDS Angela Luballa(pichani) leo aliwashangaza watu alipoamua kurejesha taji hilo wiki moja tangu avalishwe.
Luballa ambaye pia alishika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema kuwa imani yake haimruhusu kuwa Balozi wa REDDS.
“Imani yangu kwa Yesu ni kubwa mno na hainiruhusu mimi kuwakilisha REDDS, hivyo nimeamua kurejesha taji na zawadi za fedha nilizopewa,” alisema Luballa.Tembelea blog ya Lukwangule kwa undani zaidi wa habari hii ambayo kwa vyovyote vile itazua mjadala.Kipi kinakubalika kwa Yesu na kipi hakikubaliki?Imani ni nini hasa?Je ni kweli hakuna shinikizo?Bonyeza hapa.

 

MISS GLOBAL PUBLISHERS 2008 August, 5, 2008

Filed under: Mahusiano/Jamii,Miss Tanzania,Urembo,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 2:23 PM

Sambamba na shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2008,palikuwepo pia mchakato ulioendeshwa na kampuni ya Global Publishers ili kumpata mrembo ambaye watu mbalimbali waliona ndiye mwenye mvuto zaidi ya wengine.Tutakuwa hatukosei sana tukisema kwamba zoezi hilo lilikuwa ni kama vile kutafuta mrembo ambaye ni People’s Choice.Aliyeibuka mshindi katika hilo ni mrembo Kelly Kamwelu(pichani) ambaye ndiye Miss Ilala 2008.BC inampongeza na kumtakia kila la kheri.

Photo/GP

 

SALAMU ZANGU-IRENE SANGA ft MRISHO MPOTO na ELIDADI MSANGI July, 24, 2008

Filed under: Bongo Reality TV,Burudani,Mahusiano/Jamii,Muziki,Weekend Special — bongocelebrity @ 9:05 PM

Irene Sanga(kushoto) akiwa jukwaani na Elidadi Msangi.

Kama ikitokea ukawa umechoshwa na kusikiliza nyimbo au miziki inayoelemea upande mmoja tu(mara nyingi upande wa mapenzi) basi hutojutia kubadilisha frequency na kusikiliza wimbo uitwao Salamu Zangu ukiwa ni utunzi mahiri wa msanii Irene Sanga ambaye ameuimba wimbo huo kwa kuwashirikisha msanii maarufu wa mashairi,Mrisho Mpoto na Elidadi Msangi. Salamu Zangu ni mojawapo ya vibao ambavyo vilitokea kupendwa sana nchini Tanzania na kimebakia kuwa gumzo mpaka hivi leo.

Akiongea na BC hivi karibuni, Irene Sanga,alisema aliamua kutunga au kuandika mashairi kama unavyoweza kuyasikia katika wimbo huu,baada ya kukerwa na jinsi ambavyo wasanii wengi wa muziki wanavyokuwa wameegemea zaidi upande wa nyimbo za kimapenzi peke yake na hivyo kusahau kabisa pande zingine za maisha ya jamii kwa mfano umasikini,uonevu nk.Kwake yeye,anasema, muziki au sanaa sio chombo cha kuburudisha tu bali kuonya,kukosoa,kukumbusha nk.

Mshairi Mrisho Mpoto akituma Salamu zake kwa mjomba.

Wimbo huu umo ndani ya albamu iitwayo “Utandawazi” ambayo Irene anasema bado hajaamua kuitoa rasmi sokoni kutokana na sababu mbalimbali.Nyimbo zingine ndani ya albamu hiyo ni kama vile Utandawazi(inayobeba jina la albamu), Pangisheni,Maureen,Usivunje,Ndoto,Afrika Yote na huu Salamu Zangu/Salamu kwa Mjomba.Albamu hiyo imetengenezwa ndani ya Mawingu Studio jijini Dar-es-salaam.

Wimbo huu ambao leo ndio unatupa burudani ya wiki ni ombi rasmi kutoka kwa Pius Mikongoti.Pata Burudani.Wikiendi Njema.

Picha zote na Bob Sankofa.

 

KEISHA July, 14, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Mahusiano/Jamii — bongocelebrity @ 9:58 PM

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Khadija Shaban a.k.a Keisha.Binti huyu hivi karibuni alikaririwa akielezea masikitiko yake juu ya kuuawa kwa ma-albino nchini Tanzania kutokana na imani za kishirikina.Keisha anasoma nchini Uganda.

Photo/Global Publishers.